Mazao jamii ya kunde na maajabu yake katika kilimo na lishe

Mazao jamii ya kunde yanazalisha mafuta ya kula yanayotumiwa na binad­amu na wanyama. Mimea hiyo inatofautiana katika maumbile na jambo hilo ndilo linalosababisha kuwapo kwa aina nyingi za jamii ya kunde.

Mazao hayo yana faida za kiafya na lishe. Pia yana­saidia katika ukuzaji wa mazao mengine kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kurekebisha kiwango cha naitrojeni katika udongo. Pia inaelezwa yanasaidia kukabiliana na gesi cha­fuzi, yanaimarisha rutuba na yanatumia kiasi kidogo cha maji kuliko mazao men­gine.

Kwa miaka zaidi ya mitano, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limekuwa likihimiza utumiaji wa njia za kisasa za kilimo na zile zinazohimili mabadiliko ya tabianchi na teknolojia katika mazao ya maharag­we, mahindi na mihogo, chini ya Programu ya Pamo­ja ya Kigoma.

Wakulima wa wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko wamethibitisha ongezeko la mavuno ya mazao jamii ya kunde baada ya kupatiwa ujuzi unaotakiwa juu ya namna ya kutumia mbegu za aina mbalimbali na kuchangan­ya mazao hayo na mengine kama vile mahindi. Wapo waliosema mavuno yalion­gezeka kwa kutoka kg 95 kwa ekari mpaka kg 400 huku kiwango cha uwekaji mbegu nacho kikipungua kutoka kg 90 kwa ekari hadi kg 32.

Umoja wa Mataifa kupitia Mradi wa Pamoja wa Kigo­ma pia unaendelea kufanya kazi na taasisi za Serikali kama vile Taasisi ya Uta­fiti wa Kilimo (TARI), Taa­sisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI) na Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Kanembwa, katika kusaidia ongezeko la uzalishaji wa mbegu bora za maharagwe ili kuwezesha upatikanaji.. Vilevile mradi umeshiriki­ana na waalimu wa shule za msingi kwa kujumuisha dhana ya kilimo bora cha maharagwe katika masomo ya elimu ya kujitegemea.


Theresia Massoy, Ofisa Kilimo–FAO Tanzania.