Namna TIRA inavyoweka mazingira bora ya uwekezaji katika sekta ya bima

Dk Baghayo Saqware, Kamishna wa Bima Tanzania.

Sekta ya bima ni muhimu sana katika kukuza uchumi na kuimarisha mazingira ya biashara. Sekta hii ina jukumu muhimu katika kukuza ustawi wa kifedha wa jamii na uchumi kwa ujumla. Aidha, uwekezaji katika sekta hii unaleta manufaa mengi ambayo yanahitaji kutiliwa mkazo.

Uwekezaji katika sekta ya bima husaidia kukuza uchu¬mi kwa kuongeza uwezo wa kifedha wa watu binafsi na biashara. Hii husababisha kuongezeka kwa matumizi na uwekezaji, na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi.

Katika biashara, bima ni muhimu sana. Inawapa ulinzi dhidi ya hatari za biashara, kama vile uharibifu wa mali au madai ya fidia. Kwa kuwekeza katika bima, biashara zinaweza kuhakikisha kuwa zin-aendelea kufanya kazi hata baada ya kukumbwa na matatizo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kwamba sekta ya bima inakuwa na mazingira bora ya uwekezaji, ambayo yameongeza imani kwa wawekezaji na kuimarisha sekta hiyo kwa ujumla.


Jukumu la bima katika sekta ya biashara

Bima ni chombo muhimu katika usimamizi wa hatari. Biashara zinakabiliwa na hatari nyingi kama vile majanga ya asili, moto, wizi, na hata kufilisika. Kupitia sera za bima, wamiliki wa biashara wanaweza kupunguza athari za kifedha zinazoweza kutokea kutokana na hatari hizo.

Hii siyo tu kwamba inaongeza utulivu katika biashara lakini pia inachochea ujasiriamali na uwekezaji mpya, kwa kuwa wawekezaji wanakuwa na uhakika kwamba uwekezaji wao una ulinzi wa kifedha. Leo katika ukurusa huu, Kamishna wa Bima Tanzania, Dk Baghayo Saqware anatueleza namna TIRA inavyoweka mazingira bora ya uwekezaji katika sekta ya bima. Karibu.

TIRA inafanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya bima inakuwa na mazingira bora ya uwekezaji. Tumefanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali, wakiwemo Serikali, kampuni za bima na wateja ili kuhakikisha tunaboresha mfumo mzima wa bima nchini. Hapa kuna baadhi ya hatua ambazo tumechukua.

Kuboresha mfumo wa kisheria: Tumeanzisha na kurekebisha sheria na kanuni zinazohusu bima ili ziweze kukidhi mahitaji ya sasa ya soko na wawekezaji. Sheria hizi mpya zimeweka misingi mizuri ya uwazi, uwajibikaji, na ushindani katika sekta ya bima. Hii imechangia kuongezeka kwa watoa huduma za bima kutoka 1324 mwaka 2022 hadi kufikia 1507 mwaka 2023.

Kuimarisha usimamizi na udhibiti: Tumeweka mifumo ya usimamizi na udhibi¬ti inayohakikisha kwamba kakampuni za bima zinazingatia viwango vya juu vya utoaji wa huduma. Hii inaju-muisha ukaguzi wa mara kwa mara wa kampuni za bima na kuhakikisha kwamba zina mitaji ya kutosha na zinatoa huduma bora kwa wateja wao. Mamlaka imetoa Muongozo wa Uwekezaji na Usimamiaji Ukwasi ambapo Kulingana na Kanuni Na. 20 (a), kampuni ya bima iliyopata hasara kubwa inaweza kuruhusiwa kuchukua Amana ya Dhama kulingana na Miongozo.

Kuhamasisha uelewa wa bima: Tumefanya kampeni za elimu kwa umma ili kuonge¬za uelewa wa umuhimu wa bima. Hii imekuwa ikisaidia kuondoa mitazamo hasi na kuongeza idadi ya watu wana-otumia huduma za bima. Mfa¬no watumiaji wa hoduma za bima wameongezeka kutoka milioni 6 mwaka 2021 mpaka watumiaji milioni 12.1 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 100. Pia Mamlaka imetangaza fursa za uwekezaji katika Bima ambapo iliku-tana na Kampuni kubwa Nne za Bima za nchini India hasa katika maeneo ya bima za afya na kilimo.

Kuweka mifumo ya kidijitali: Tumeanzisha mifumo ya kidijitali inayorahisisha utoaji wa huduma za bima. Hii inajumuisha matumizi ya teknolojia katika michakato ya kutoa bima, kufanya malipo, na kushughulikia madai ya bima. Mifumo kama vile TIRAMIS na ORS imeongeza ufanisi na uwazi katika sekta ya bima.

Kushirikiana na wadau: Tumejenga ushirikiano mzuri na wadau mbalimbali kama vile serikali, taasisi za kifedha, na mashirika yasiyo ya kiserikali. Ushirikiano huu umesaidia kuleta maboresho makubwa katika sekta ya bima na kuweka mazingira bora kwa wawekezaji.

Kuna hatua nyingine maalum ambazo TIRA imechukua ili kuvutia wawekezaji zaidi katika sekta ya bima. Hatua hizo ni; kuanzisha motisha kwa wawekezaji. Tumekuwa tukitoa taarifa na takwimu za soko ili wawekezaji wapate picha kamili ya fursa zilizopo katika sekta ya bima, taarifa hizi licha ya kuzizindua rasmi pia zinapatikana kwenye tovuti ya Mamlaka. Pia, tumeanzisha mifumo ya kutoa leseni kwa haraka na kwa uwazi ili kupunguza urasimu na kuwawezesha wawekezaji kuanza shughuli zao kwa haraka.

Vilevile, tumeweka mifumo ya usuluhishi wa migogoro ambayo inasaidia kutatua migogoro inayoweza kutokea kati ya wateja na makampuni ya bima kwa haraka na kwa haki kwa kupitia Kamati yake ya Utekelezaji wa Sheria. Hii imeongeza imani ya wawekezaji na wateja katika mfumo wetu wa bima.

Hatua hizi z i m e l e t a ma t o k e o c h a n ya sana. T u m e -shuhudia ongezeko kubwa la wawekezaji wanaovutiwa kuwekeza katika sekta ya bima. Pia, idadi ya wananchi wanaotumia huduma za bima imeongezeka, na kiwango cha malalamiko kimepungua kutokana na uboreshaji wa huduma.

Zaidi ya hayo, kampuni za bima zimeweza kuongeza mitaji na kupanua huduma zao, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi mfano kwa mwaka 2022 Sekta ya bima imechangia pato la Taifa kwa mfano asilimia 1.99 ikilinganganishwa na mwaka 2021 a m b a p o sekta ili¬changia asilimia 1.68.

Uwekezaji katika sekta ya bima ni muhimu kwa ustawi wa kifedha wa watu bin¬afsi, biashara, na jamii kwa ujumla. Kupitia bima, tuna-jenga mazingira salama na yenye ustahimilivu, ambayo ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya uchumi na jamii. Kwa hiyo, ni muhimu kuwekeza katika kukuza na kubore¬sha sekta hii ili kuleta manufaa kwa wote.

Ni wazi kwamba juhudi za TIRA katika kuimarisha sekta ya bima nchini Tanzania zimeleta mafanikio makubwa. Kwa kuboresha sheria na kanuni, kuongeza uwazi na uwajibikaji na kuhamasisha uelewa wa bima, TIRA imeweza kuweka mazingira bora ya uwekezaji ambayo yanavutia wawekezaji wapya na kuchangia katika maendeleo ya sekta ya bima na uchumi wa taifa kwa ujumla.