Nsekela na siri ya miaka minne ya utendaji kazi uliotukuka

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakizindua tawi la benki hiyo Zanzibar na huduma ya Al Barakah inayofata misingi ya dini ya Kiislamu.

Abdulmajid Nsekela alipochu­kua usukani wa Benki ya CRDB mwaka 2018, si wote walitambua kuwa huo ulikuwa mwanzo wa safari ya mabadiliko kwa benki hiyo kubwa zaidi ya Tanzania.

Kwa hakika, wengine waliweza kupokea uteuzi wake kwa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Mtend­aji Mkuu wa Benki ya CRDB kwa mashaka fulani.

Pasi na shaka, fikra kama za Thomaso zilikuwa sahihi: Kuvaa viatu vya mtangulizi wake, ambaye aliiongoza benki kwa miongo miwili, si kazi rahisi kama kutem­bea katika bustani.

Lakini kutokea hapo hadi kufikia mwaka 2022, mambo yamebadi­lika na takwimu za benki hiyo zinadhihirisha kila kitu.

Ni jambo lililo wazi kuwa benki hiyo yenye uzoefu wa aina yake imetekeleza ipasavyo mpango wake mkakati wa miaka mitano ulioanza 2018 hadi 2022.

Kuanzia kwenye ukwasi wa mali na faida na kiwango cha mikopo chechefu hadi jumla ya mikopo na malipo ya awali, Benki ya CRDB imekua kwa kasi katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Takwimu zinambeba Nsekela linapokuja suala la kutathmini ongezeko la idadi ya mawakala wa Benki ya CRDB, uwekezaji katika miradi ya jamii na uwezeshaji wa miradi ya kimkakati, amana za mteja, mapato kwa kila hisa, kupunguza viwango vya mikopo chechefu na kuwezesha vikundi maalum miongoni mwa mambo mengine.


Mali

Ukiangalia taarifa za fedha za benki hiyo zinaonyesha kuwa kati­ka miaka minne iliyopita kume­kuwa na uboreshaji mkubwa wa ukubwa wa mali za Benki ya CRDB ambao uliongezeka kwa takriban asilimia 50 kutoka Sh5.902 trilioni mwaka 2017 hadi Sh8.817 trilioni 2021. Kwa hakika, uboreshaji huo unafikia hadi asilimia 80 endapo tu takwimu za mwaka 2022 zitaz­ingatiwa ambapo benki hiyo ili­funga robo ya tatu ya mwaka 2022 kwa jumla ya Sh10.5 trilioni za mali.

Hii ina maana kwamba Benki ya CRDB inashikilia nafasi yake kama mkopeshaji mkubwa wa Tanzania.


Amana za wateja

Mwaka 2017, Benki ya CRDB ili­kuwa na amana za Sh4.326 tril­ioni kutoka kwa wateja wake lakini kiasi hicho kilipanda kwa asilimia 50 katika kipindi cha miaka minne na kufikia Sh6.49 trilioni Desemba, 2021. Kiasi hicho kilipanda zaidi hadi Sh7.113 trilioni mwisho wa robo ya tatu ya mwaka 2022.


Faida na gawio

Wanahisa wa Benki ya CRDB Plc lazima wafurahie mwenendo wa benki yao katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Licha ya Sh34 bilioni pekee kuwa ndiyo faida halisi mwaka 2017, kiasi hicho kiliongezeka hadi kufikia Sh268 bilioni mwaka 2021, ongezeko la asilimia 644.

Ongezeko la faida lilitokana na vyanzo vya mapato vitokanavyo na riba na vile visivyotokana na riba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa mwaka 2022.

Ongezeko hili lilienda sambam­ba na fedha ambazo wanahisa hupokea kama gawio.

Ingawa kiasi cha Sh8 pekee kili­lipwa kwa kila hisa mwaka 2019 kama gawio kutokana na faida ya benki ya 2018, kiasi hicho kili­panda hadi kufikia Sh17 kwa kila hisa, Sh22 kwa kila hisa na Sh36 kwa kila hisa katika miaka ya 2020, 2021 na 2022 mtawalia.


Mikopo

Kulingana na biashara mama inayofanywa na benki hiyo, kia­si cha mikopo ya Benki ya CRDB kiliongezeka hadi kufikia Sh5.04 trilioni mwishoni mwa Desemba, 2021. Hilo liliashiria ongezeko la asilimia 74.18 ikilinganishwa na Sh2.893 trilioni zilizopatikana hadi mwishoni mwa mwaka 2017.

Kiasi hicho kimeongezeka zaidi na kufikia Sh6.1 trilioni hadi kufikia mwisho wa robo ya tatu ya mwaka 2022. Hii inaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka minne, miko­po ya Benki ya CRDB imepanda kwa asilimia 110 ikilinganishwa na kiwango cha mwaka 2017.


Mbuyu hatimaye umeanguka

Kwa uongozi wake uliojaa busara, Benki ya CRDB, chini ya Nsekela, imeweza kuongeza kiasi cha mikopo na wakati huo huo, kusimamia ubora wa mikopo kwa ufanisi.

Hali hii imesababisha kushuka kwa viwango vya mikopo chechefu ambayo ilikuwa kikwazo kwa ben­ki hiyo siku za nyuma.

Wakati vitabu vya benki hiyo vikionyesha kiwango kikubwa cha mikopo chechefu cha Sh393.295 bilioni mwaka 2017, kiasi hicho kilishuka kwa zaidi ya nusu hadi Sh175 bilioni tu mwishoni mwa mwaka 2021.

Ikiwa ni asilimia ya jumla ya mikopo ghafi, mikopo chechefu ili­shuka kutoka asilimia 12.6 mwaka 2017 hadi asilimia 3.3 tu mwishoni mwa mwaka 2021. Kwa hakika, tak­wimu za siku za karibuni zinaweka makadirio ya walau asilimia 3.2.

Hii ina maana kwamba viwango vya mikopo chechefu kwa sasa viko ndani ya kizingiti cha udhibiti cha si zaidi ya asilimia tano.


Mapato kwa mwaka

Mapato kwa kila hisa yame­ongezeka kutoka Sh13.9 mwaka 2017 hadi Sh102.67 mwaka 2021 huku uwiano wa gharama kwa mapato pia ukiimarika kwa kiasi kikubwa. Kwa upande wa uwiano wa gharama kwa mapato ulifikia asilimia 66.7 mwaka 2017 lakini umeongezeka hadi asilimia 55.3 mwaka 2021.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Makamu wa Rais wa Ukanda wa Afrika wa International Finance Corporation, Sergio Pimenta (kulia)wakikabidhiana makubaliano ya pamoja ya kibiashara

Mfumo mkuu wa benki na mawakala wa benki

Katika miaka minne iliyopita ya Nsekela katika uongozi wa Benki ya CRDB, idadi ya ofisi za mawaka­la wa benki hiyo imeongezeka kutoka 5,000 pekee mwaka 2018 hadi 25,000 hivi sasa. Kwa ubu­nifu zaidi, mawakala hao kwa sasa wamejengewa uwezo kiasi cha kuwafungulia akaunti za benki wateja wapya hivyo kuwaondolea adha wateja kufunga safari hadi kwenye tawi la benki.

Chini ya Nsekela, Benki ya CRDB imeboresha mfumo wake wa kibenki ili kuongeza ufanisi katika matawi yote ya benki.

"Utekelezaji wa hili ulifanywa kulingana na mkakati wetu wa muda wa kati ambao unategemea mabadiliko ya kidijitali," Nsekela alisema hivi karibuni.

Kupitia mifumo yake ya kidiji­tali, Benki ya CRDB sasa inaende­sha bidhaa ya SimAccount ambayo inawawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo, wanaojulikana kama Wamachinga, kupata miko­po ya papo kwa papo moja kwa moja kupitia simu zao.

Mfumo huo pia unaruhusu wafanyakazi wanaolipwa misha­hara kupokea Salary Advance (malipo ya mshahara) pamoja na Boom Advance (malipo ya miko­po) na Pension Advance (malipo ya pensheni) kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na wastaafu mtawalia.


Uimarishaji wa biashara baada ya UVIKO-19

Kwa kutambua umuhimu wa kuwezesha vikundi mbalimbali vya kijamii kiuchumi, Benki ya CRDB imechukua hatua kadhaa kusaid­ia wafanyabiashara wanaofufua biashara zao baada ya UVIKO-19.

Mipango hiyo ni pamoja na kupunguza riba ya mikopo kwa sekta ya kilimo na mnyororo wake wa thamani kutoka asilimia 20 hadi asilimia tisa pekee mwaka huu. Wakati huo huo, viwango vya riba ya mikopo binafsi vimepun­gua kutoka asilimia 16 hadi 13.

Kwa kushirikiana na baadhi ya washirika wake, wakiwemo AfDB, AGF, USAID, DFC na FC, Benki ya CRDB pia imefanya maboresho kadhaa ya mikopo inayotolewa kwa vikundi maalum, wakiwemo wanawake wajasiriamali.

Kutokana na hali hiyo, idadi ya wateja wa benki hiyo imeongezeka kutoka milioni tatu mwaka 2018 hadi milioni nne kwa sasa.


Miradi ya kimkakati yenye maslahi kwa Taifa

Wakati ikiendelea na shughuli zake za msingi za kutoa mikopo kwa sekta ya uzalishaji, Benki ya CRDB pia imekuwa ikishiriki kika­milifu katika kuwezesha miradi ya kimkakati ya Tanzania ambayo inatekelezwa na Serikali na sekta binafsi.

Mbali na kuwezesha sekta ya viwanda, nishati, madini, utalii na miundombinu miongoni mwa mambo mengine, Benki ya CRDB pia imeshiriki kikamilifu katika kuwezesha ujenzi wa Bwawa la Umeme wa Maji la Nyerere la MW 2,115 na ujenzi unaoendelea wa njia ya Reli ya Kisasa (SGR).


Kuingia DRC

Baada ya kufanya vyema katika vigezo vyote, Nsekela ameiongoza Benki ya CRDB kuingia katika soko la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo ipo katika hatua za mwisho kuanza kutoa huduma nchini humo. Pamoja na mkakati wa biashara, uwekezaji huu unalenga kukuza chapa ya benki na kumtangaza kama taasisi kinara wa huduma za kibenki nda­ni na nje ya mipaka ya Tanzania.

"Tutaanza na Sh70 bilioni kama mtaji….Tunatazamia pia kuingia Zambia, Malawi, Comoro, Uganda na Kenya," Nsekela aliwaambia washiriki wakati wa ufunguzi wa makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu. Rais Samia Suluhu Hassan akipamba hafla hiyo.

Kuingia kwa benki hiyo nchini DRC kunaungwa mkono na taasisi za kifedha zinazotambulika duni­ani zikiwemo Norfund ya Norway na The Investment Fund for Devel­oping Countries (IFU) ya Denmark.

"Washirika hawa wawili wana mawazo sawa na ya Benki ya CRDB hasa juu ya mkakati na ubunifu, mabadiliko ya tabianchi na masu­ala ya ushirikishwaji wa kijinsia," Nsekela alisema wakati wa maho­jiano hivi karibuni.

Novemba 2021, benki hiyo ilian­dika historia chini ya Nsekela kwa kuwa taasisi ya fedha ya kwanza kwa Afrika Mashariki kuidhinish­wa na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa uliopo Korea Kusini.

Benki pia imeanzisha ushiriki­ano na wafadhili wa kibiashara wa Ufaransa, Propaco na Shiri­ka la Maendeleo la Kimataifa la Marekani.

Kutokana na utendaji kazi ulio­tukuka katika benki hiyo, Nsekela amejipatia yeye na benki hiyo tuzo kadhaa ikiwa ni pamoja na benki bora zaidi ya jarida la Euromoney nchini Tanzania ambayo ilitunuki­wa Julai mwaka huu.

"Tumefurahishwa na kutambu­liwa kwetu na Euromoney ambao unatutia moyo kufanya kazi kwa bidii zaidi na kutoa kilicho bora kwa wateja wetu," Nsekela alisema baada ya kupokea tuzo hiyo huko London, mji mkuu wa Uingereza mwezi Julai.

Majaji hao wa Euromoney walisema katika taarifa yao kwamba Benki ya CRDB iliibuka mshindi baada ya kuwashinda wenzao katika soko la ndani kuto­kana na uwekezaji wa benki hiyo katika njia za kisasa za kidijitali na kufanya vizuri katika ujumuishaji wa kifedha.

Mwaka jana, benki hiyo pia ili­tajwa kuwa benki bora zaidi ya kibunifu nchini na Global Finance na Jumuiya ya Ulaya ya Utafiti wa Ubora, benki bora zaidi soko­ni. Kwa ujumla benki hiyo yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam imeshinda tuzo 20 za nda­ni na kimataifa tangu 2018.