Pongezi kwa viwanda bora vya Kitanzania kwa kutunukiwa tuzo za tano za KAIZEN

What you need to know:
Mashindano ya 5 na sherehe za tuzo za KAIZEN Tanzania zilifanyika jijini Dar es Salaam Februari 4 hadi 5, 2021. Tangu 2013, Wizara ya Viwanda na Biashara na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) wamekuwa wakitekeleza mradi unaoangazia Uimarishaji wa Viwanda vya Kati kupitia Uboreshaji wa Ubora na tija (KAIZEN) ili kuchochea ukuaji wa viwanda nchini. Mashindano ya tuzo na sherehe zilifanyika kama moja ya shughuli za mradi huu.
Mashindano ya 5 na sherehe za tuzo za KAIZEN Tanzania zilifanyika jijini Dar es Salaam Februari 4 hadi 5, 2021. Tangu 2013, Wizara ya Viwanda na Biashara na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) wamekuwa wakitekeleza mradi unaoangazia Uimarishaji wa Viwanda vya Kati kupitia Uboreshaji wa Ubora na tija (KAIZEN) ili kuchochea ukuaji wa viwanda nchini. Mashindano ya tuzo na sherehe zilifanyika kama moja ya shughuli za mradi huu.
Viwanda 13 vilichaguliwa kutoka katika mashindano ya mkoa, na katika fainali, na kisha kati ya hivyo, viwanda viwili vilichaguliwa: kiwanda kimoja kilichaguliwa kutoka katika kipengele cha viwanda vya chini na kati na vingine kutoka katika vikubwa vikubwa. Viwanda hivyo vilitunukiwa tuzo kama “Viwanda Bora” katika mashindano hayo.
Viwanda bora vilivyochaguliwa vitapewa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano yanayokuja ya Tuzo ya KAIZEN Afrika 2021 wakati wa Mkutano wa Mwaka wa KAIZEN Afrika 2021 (AKAC 2021) ambao utafanyika kwa pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA), Wizara ya Viwanda na Biashara, na JICA Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Inatarajiwa kwamba viwanda vilivyochaguliwa vya Tanzania vitawasilisha shughuli na mafanikio yao ya KAIZEN kwa wawakilishi kutoka nchi zingine za Kiafrika katika AKAC 2021, na hivyo kueneza kazi zao bora kwa bara lote la Afrika.
Hapa, tunatoa maelezo mafupi ya viwanda viwili tulivyovichagua:
Cultural Crafts Consultant & Design Co. Ltd (CRACODE) – Kiwanda bora cha chini na kati
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007, kiwanda hiki kimekuwa kikitengeneza kwa mikono bidhaa zitokanazo na pamba kama vitambaa, mazulia, mifuko n.k Bidhaa hizi ni kwa ajili ya matumizi ya watu binafsi (pamoja na watalii), serikali, hoteli, na taasisi binafsi. Kiwanda hiki kimeanza kutekeleza KAIZEN katika shughuli zake tangu Juni 2019.
Hapo awali, walikabiliwa na changamoto kama vile kiwango duni cha uzalishaji kutokana na mazingira duni ya kazi. Hakukuwa na chumba cha mikutano, hakukuwapo chumba cha kubadilishia nguo, n.k Hali hii iliwawia vigumu wafanyakazi kutafuta malighafi na vifaa vya kufanya kazi kwa wakati. Kwa kuongezea, hali hii iliwaweka wafanyakazi wote na kiwanda katika hatari zaidi.
Hata matukio ya ajali katika kiwanda hiko, yalikuwa yakitokea kwa wastani wa mara moja kwa mwezi.Kulingana na hali hii, kiwanda kiliamua kuanza kutumia njia ya KAIZEN kukabiliana na changamoto zilizokuwa mbele yao. Kupitia KAIZEN, kiwanda kilitumia njia za 5S katika shughuli zake. Matokeo yake, mazingira ya kazi yaliboreshwa maradufu.
Sehemu za kutembea zilitengwa, mashine ziliwekwa katika sehemu nzuri, na muda wa kutafuta vifaa vya kufanyia kazi ulipungua. Hatua hizi zote zilisababisha kuongezeka kwa asilimia 10 ya kiwango cha uzalishaji wa kila mwezi. Hivi sasa, kiwanda kinajaribu kutengeneza Taratibu za Viwango vya Uendeshaji (SOP) ili kuongeza ufanisi wa mchakato wa uzalishaji na kuimarisha ubora wa bidhaa. Wana maono ya kukuza masoko mapya kupitia uboreshaji zaidi wa tija na ubora kulingana na shughuli zinazoendelea za KAIZEN.
KIOO Ltd – Kiwanda bora kikubwa
KIOO Limited ni kiwanda kikubwa zaidi Afrika Mashariki kinachozalisha chupa za glasi. Bidhaa zake ni za matumizi ya nyumbani na kuuzwa kwa nchi zingine za Afrika Mashariki kama Kenya, Uganda, Rwanda, n.k Kiwanda hicho kimeanza kutekeleza shughuli za KAIZEN tangu Juni 2018.
Mwanzoni, waliangalia hali ya sasa ili kubaini na kuweka vipaumbele katika mambo matatu muhimu zaidi, ambayo ni:- uboreshaji wa tija za bidhaa za mbao, upunguzaji wa taka za trei za karatasi, na kupunguza dosari za bidhaa. Kulingana na uchanganuzi huo, timu tatu za KAIZEN ziliundwa kama kikosi kazi cha kushughulikia masuala hayo.
Kila timu ya KAIZEN ilitambua / ilichagua eneo husika kwa kutumia takwimu za namba na njia ya utatuzi wa changamoto za kitafiti. Kilichotokea ni kuwa, kiwanda kimeongeza tija ya uzalishaji wa bidhaa za mbao kwa asilimia 50, imepunguza taka kwa asilimia 10, na imepunguza dosari/hitilafu kwa asilimia 24. Kila maboresho hutoa matokeo mazuri kwa mustakabali wa hali ya kifedha wa kiwanda (k.v. mauzo, faida, mtiririko wa fedha) vile vile.
Kiwanda hicho kimepanga kuendelea na shughuli hizo na hatua zingine za kukabiliana na changamoto kwa sababu inalenga kufikia maboresho zaidi kwa maeneo hayo. Wakati huo huo, kiwanda kinatafuta uwezekano mwingine wa kutekeleza shughuli za KAIZEN, na kimepanga kutumia falsafa za KAIZEN kwa wadau wao. Kiwanda hicho kinatazamia kuwa kuwa kiwanda kinachoongoza cha KAIZEN nchini.
Kuhusu JICA (Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan)
Ni shirika lilioanzishwa kisheria kusimamia Misaada ya Maendeleo kwa Nchi za Nje (ODA) ya Japan. Ni mojawapo ya mashirika makubwa zaidi ya misaada duniani linalosaidia maendeleo ya uchumi katika nchi zinazoendelea katika maeneo tofauti duniani.
Hapa nchini, JICA imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Tanzania kwa zaidi ya miaka 50 katika sekta nyingi tangu 1962.
Mkutano wa Mwaka wa KAIZEN wa Afrika (AKAC)
AKAC ni mkutano mkubwa zaidi wa kimataifa kwa ajili ya KAIZEN barani Afrika, ambao unaundwa na mkutano na mashindano ya shughuli za KAIZEN (yaani Tuzo ya Afrika KAIZEN). Umekuwa ukiandaliwa kila mwaka tangu 2016 na kwa pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (AUDA) - Ushirikiano Mpya wa Maendeleo ya Afrika (AUDA-NEPAD) na JICA.

Tangu mwishoni mwa miaka ya 2000, JICA ilikuwa tayari imeanza kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo ya sekta binafsi barani Afrika ikianzisha “KAIZEN”. Maendeleo ya sekta binafsi ni moja ya mambo muhimu kwa ukuaji wa viwanda, na kutengeneza ajira na kazi zenye staha. Kwa maendeleo zaidi ya shughuli za KAIZEN katika bara la Afrika, JICA na AUDA-NEPAD kwa pamoja walibuni “Mpango wa KAIZEN wa Afrika” (AKI), na AKAC ni moja ya shughuli za msingi za AKI. AKI inajaribu kutekeleza KAIZEN kwa biashara za kati zaidi ya 18,000 na zaidi ya watu 280,000 katika nchi 25 za Afrika hapo baadaye.