Serikali ya awamu ya sita inavyofanya mapinduzi katika ujenzi, ukarabati wa barabara Manyarakatika Manyara

Mwonekano wa daraja la Magara ambalo limejengwa katika eneo la Magara umbali wa Km 21 kutoka Mbuyu wa Mjerumani katika barabara kuu ya Babati – Arusha.

Uimarishwaji wa miundombinu na uboreshaji wa sekta ya usafiri ni baadhi ya mihimili inayopewa umuhimu nchini katika kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kuwa ya uchumi wa kati na viwanda.

Kwa sasa hali ya uboreshaji wa miundombinu hii ni nzuri ukilin­ganisha na miaka kadhaa iliyo­pita kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara zinazounganisha mikoa, wilaya na miji ambazo zimesaidia katika utekelezaji wa shughuli mbalim­bali za uwekezaji.

Wachumi wanaeleza kuwa ili Taifa lolote liweze kujikwamua kiuchumi ni lazima pamoja na mambo mengine liboreshe sekta ya usafiri kuanzia ndani na nje ya miji ili kurahisisha usafirishaji na kuchangia maendeleo kama ina­vyofanyika kwa sasa hapa nchini kupitia Wakala wa Barabara Tan­zania (TANROADS).

TANROADS ni Wakala chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambayo iliundwa chini ya kifungu 3 (1) cha Sheria ya Wakala (Sura 245) na kuanza kazi mwezi Julai, 2000. Kila mkoa una ofisi ya TAN­ROADS ambayo imepewa jukumu la kusimamia mtandao wa baraba­ra wa mkoa husika.

TANROADS Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Serikali ime­kuwa mstari wa mbele na mhi­mili mkubwa katika uboreshaji wa sekta ya barabara katika Mkoa huo kitu ambacho kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani sasa hivi kuna miradi mingi ya barabara ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwenye Mkoa huo.

Manyara ikiwa ni moja ya mikoa inayokua kwa kasi katika nyanja ya utalii, biashara, kilimo na madini inamahitaji makubwa ya barabara zenye ubora ili kurahisisha shu­ghuli hizo.

Ili kukidhi mahitaji hayo, TAN­ROADS Mkoa wa Manyara imeku­wa ikijidhatiti kuhakikisha mkoa huo unaunganishwa na barabara za lami kwenye maeneo yote.

Katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, TANROADS Mkoa wa Manyara imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa barabara jambo ambalo lime­saidia kufungua fursa nyingi za kiuchumi.

TANROADS Mkoa wa Manyara inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa Km 1,657, kati ya hizo Km 207 ni barabara kuu na Km 1,450 ni barabara za Mkoa.

Kilometa 207 za barabara kuu zote ni za lami na Km 51 za barabara za Mkoa ni za lami na kufanya jumla ya barabara za lami kuwa Km 258 (sawa na asilimia 16) na zilizobaki Km 1,399 (sawa na asilimia 84) ni za changarawe. Barabara zote ziko katika hali ya kuridhisha na zinapitika wakati wote wa mwaka.

Mafanikio ya TANROADS Mkoa wa Manyara katika kipindi cha uon­gozi wa Rais Dk Samia

Kuanza ujenzi wa barabara, seh­emu ya Mbulu – Garbabi (Km 25) kwa kiwango cha lami

Serikali kupitia TANROADS imeingia mkataba na mkanda­rasi M/s Jiangxi Geo Engineering (Group) Corporation kutoka China Juni 30, 2022 kwa ajili ya utekelez­aji wa mradi wa ujenzi wa baraba­ra, sehemu ya Mbulu-Garbabi (Km 25) kwa kiwango cha lami ambao unagharimu zaidi ya Sh 35.17 bil­ioni. Mradi huo ni wa miezi 18.

Mpaka sasa Mkandarasi huyo anaendelea na uwekaji wa mata­baka ya chini ya barabara pamoja na ujenzi wa makalvati. Aidha ujenzi wa nyumba za wasimamizi wa mradi, ofisi pamoja na maabara ya vifaa vya ujenzi umekamilika. Kwa ujumla utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 20.

Ujenzi wa sehemu ya pili (Lot 2) barabara ya Labay-Haydom (Km 25)

Kwa kipande cha Labay-Hay­dom Km 25 mkataba ulisainiwa Mei 19, 2023 kati ya Serikali na Mkandarasi M/s Jiangxi Geo Engineering Co Ltd kutoka Chi­na. Ujenzi wa barabara hii unata­rajiwa kufanyika kwa utaratibu wa usanifu na ujenzi (design and build) ambapo mkandarasi ame­kwishaanza zoezi la usanifu.

Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Mji wa Dongobesh

Katika kipindi cha miaka miwili cha Serikali ya awamu ya sita TAN­ROADS Mkoa wa Manyara imejen­ga Km 3.2 za barabara kwa kiwan­go cha lami eneo la Dongobesh Mjini kwa gharama ya Sh 2.11 bil­ioni. Barabara hii ni muhimu kwa wakazi wa Mji wa Dongobesh na Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Miradi inayotekelezwa kwa kush­irikisha wabia kwa utaratibu wa EPC+ Financing

Katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilitoa kibali kwa TAN­ROADS Mkoa wa Manyara cha kutangaza miradi saba ambayo itatekelezwa kwa utaratibu wa Engineering, Procure­ment, Construction and Financing (EPC+F).

Katika Mkoa wa Man­yara kuna miradi mitatu ya ujenzi wa barabara kwa uta­ratibu wa EPC+ Financing. Miradi hiyo ina jumla ya Km 515 zikihusisha Wilaya ya Mbulu, Simanjiro na Kite­to. Miradi hiyo ni; Arusha-Kibaya-Kongwa Junction (Km 493), Handeni-Kiber­ashi-Kijungu-Njoro-Olbo­lot-Mrijo Chini-Dalai-Bicha -Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (Km 460) na Karatu – Mbulu – Hay­dom – Sibiti River – Lalago – Maswa (Km 389). Hatua ya utekelezaji wa miradi hii ni kama ifuatavyo;

Mradi wa Barabara ya Aru­sha - Kibaya - Kongwa (Km 493)

Katika Mradi huu Mkoa wa Manyara una jumla ya Km 332.1 kati ya Losinyai na Dosidosi katika Wila­ya za Simanjiro na Kiteto mtawalia. Kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina ilitekelezwa na Mhandisi Mshauri M/S. CHEIL ENGI­NEERING CO.LTD (South Korea) akishirikiana na M/S Inter-Consult Ltd (Tanza­nia) na kukamilika mwezi Desemba, 2019.

Mradi huu utarahisi­sha usafiri wa watu na usafirishaji wa mazao na mifugo hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi kwani unaunganisha mikoa mitatu kwa maana ya Arusha, Man­yara na Dodoma.

Utekelezaji

Mkataba wa ujenzi kati ya Serikali na Mkandarasi ulisainiwa tarehe 16 Juni, 2023. Mkandarasi yupo katika maandalizi ya kuanza kazi na anatarajia kukabid­hiwa uwanda wa kazi (site) ndani ya mwezi Agosti 2023.

Mradi wa Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Njoro – Olbolot – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (Km 460)

Katika mradi huu Mkoa wa Manyara una Km 120 kuanzia Kiberashi (Mpak­ani na Tanga) hadi Olbolot (Mpakani na Dodoma).

Mradi huu utajenga barabara ambayo ni kiun­ganishi kati ya bandari ya Tanga na nchi za jirani kama vile Burundi, Uganda na Congo hivyo kufungua fursa mbalimbali katika mikoa na nchi za jirani.

Pia mradi huu utarahisi­sha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao na mifugo hivyo kuchochea shughuli za kiu­chumi kwani unaunganisha mikoa minne kwa maana ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida.

Utekelezaji

Mkataba wa ujenzi kati ya Serikali na Mkandarasi ulisainiwa tarehe 16 Juni, 2023. Mkandarasi yupo katika maandalizi ya kuanza kazi na anatarajia kukabid­hiwa uwanda wa kazi (site) ndani ya mwezi Agosti 2023.

Mradi wa Barabara ya Kara­tu – Mbulu – Haydom – Sibi­ti River – Lalago – Maswa (Km 389)

Katika barabara ya Kili­mapunda - Kidarafa yenye Km 113 ndani ya Mkoa wetu wa Manyara, mradi huo uta­jumuisha Km 63 kwani Km 50 zinatekelezwa kwa kutu­mia fedha za ndani kwenye miradi ya Mbulu – Garbabi na Labay – Haydom.

Mradi huu utajen­ga barabara ambayo ni muhimu sana na maarufu kwa jina la Serengeti South­ern Bypass na utarahisisha shughuli za Utalii, Usafiri na Usafirishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao na mifugo hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi kwani unaunganisha mkoa wa Manyara na kanda ya ziwa kupitia mikoa minne kwa maana ya Arusha, Manyara, Singida na Simiyu.

Utekelezaji

Mkataba wa ujenzi kati ya Serikali na mkandarasi ulisainiwa tarehe 16 Juni, 2023. Mkandarasi yupo katika maandalizi ya kuan­za kazi na ujenzi utaanza wakati wowote kutoka sasa. Aidha, mkandarasi ataka­bidhiwa uwanda wa kazi (site) ndani ya mwezi Agosti 2023.

Usimikaji wa taa za baraba­rani maeneo ya miji

Katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita, TANROADS Mkoa wa Manyara imesimika taa za barabarani katika Makao Makuu ya Mkoa, Wilaya na Miji midogo. Jumla ya taa 398 zimesimikwa kwa gharama ya Sh 1.7 bilioni.

Maboresho ya Kituo cha Mizani Mdori

Kutokana na ongezeko la idadi ya magari ya usafirish­aji, TANROADS Mkoa wa Manyara imefanya upanuzi wa Kituo cha Mizani Mdori kwa kujenga mizani mpya, kufanya maboresho ya eneo la kuingia na kutoka magari na eneo la kuegesha magari yaliyozidi uzito (parking). Ujenzi huu umegharimu jumla ya Sh 1.2 bilioni.

Ujenzi wa Daraja la Magara

Mradi huu wa ujenzi wa daraja la Magara ni utekelezaji wa Ilani ya Uch­aguzi ya Chama cha Mapin­duzi (CCM) ya mwaka 2015. Daraja la Magara limejen­gwa katika eneo la Magara umbali wa Km 21 kutoka Mbuyu wa Mjerumani kati­ka barabara kuu ya Baba­ti - Arusha ili kuwezesha kuvuka Mto Magara katika barabara ya Mbuyu wa Mje­rumani - Mbulu (Km 50.5).

Barabara hii inaungani­sha barabara kuu ya Dodo­ma-Babati-Arusha ambayo ni sehemu ya barabara ya Capetown-Cairo maarufu kama Great North Road na barabara ya Karatu-Mbu­lu-Haydom-Sibiti-Lalago-Maswa inayojulikana kama Serengeti Bypass.

Katika kipindi cha miaka miwili ya awamu ya sita, Serikali kupitia TANROADS Mkoa wa Manyara imeka­milisha ujenzi wa daraja la Magara (M 84) pamoja na barabara unganishi katika hilo (upande wa Mbulu) yenye urefu wa Km 2.7 kwa gharama ya Sh 12.6 bilioni.

Upanuzi na maboresho ya maeneo korofi katika Mlima Magara

Katika kipindi cha mia­ka miwili cha Serikali ya awamu ya sita TANROADS Mkoa wa Manyara imefanya upanuzi na maboresho ya maeneo korofi katika Mlima Magara yenye urefu wa Km 2 kwa gharama ya Sh 1.6 bil­ioni.

Upanuzi wa barabara seh­emu ya Mlima Dabil kati­ka barabara ya Dareda-Dongobesh na ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Orkesumet

Katika kipindi cha mia­ka miwili cha Serikali ya awamu ya sita, TANROADS Mkoa wa Manyara imefan­ya maboresho ya upanuzi wa barabara na ujenzi kwa kiwango cha lami katika Mlima Dabil yenye urefu wa Km 3.3 na ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Orkesumet Mjini yenye urefu wa Km 1.0. Gharama za miradi hiyo ni Sh 3.1 bilioni.