Siku ya Kisukari Duniani: Umepima kiwango cha sukari katika damu yako?

Chumba cha huduma za figo katika Hospitali ya Shree Hindu Mandal.

Ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza yanayoongoza kwa kusababisha idadi kubwa ya vifo kwa binadamu. Kisukari ni ugonjwa sugu unaoathiri uwezo wa mwili kusaga na kutumia chakula kinacholiwa.  


Chakula kinapoliwa hubadilishwa kuwa sukari (glucose) ambayo mwili hutumia kama nishati. Kawaida viwango vya sukari hudhibitiwa kwa uangalifu, hata hivyo, kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari, udhibiti huu hupotea.


Jedwali hapa chini linaonyesha idadi ya watu wanaoishi na kisukari na idadi ambayo inakadiriwa kuongezeka katika miaka ijayo.


Mwaka

kidunia  (umri miaka 20-79)

Afrika (umri mika 20-79)

2021

537 milioni

24 milioni

2030

  1. milioni

33 milioni

2045

783 milioni 

55 milioni


Nchini Tanzania, kwa mujibu wa Shirika la Afrya Duniani (WHO) mwaka 2012, kiwango cha maambukizi ya kisukari kilikuwa asilimia 9.1.

Siku ya kisukari duniani


Siku ya Kisukari Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Novemba 14 ili kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo. Kauli mbiu ya mwaka 2021 hadi 2023 ni “Upatikanaji wa huduma za kisukari” ambapo umuhimu wa elimu ya kisukari hutolewa kwa watoa huduma wote wa afya, watu wenye kisukari na jamii ili kuruhusu kinga kwa kuhimiza maisha bora na kutoa vipimo vya mapema na usimamizi sahihi kwa wagonjwa wa kisukari.


Kuna aina nyingi za kisukari lakini zinazojulikana zaidi ni; aina ya kwanza, aina ya pili na kisukari wakati wa ujauzito.  


Kisukari aina ya kwanza husababishwa na hali ya kingamwili ambapo kongosho hushindwa kutoa insulin-homoni muhimu ambayo inaruhusu mwili kuchukua na kutumia glukosi. Kinga ya kisukari cha aina hii kwa sasa haijulikani.


Kisukari aina ya pili husababishwa na mtindo wa maisha hususani matumizi ya vyakula visivyofaa ambavyo husababisha mtu kupata ugonjwa huu, uzito wa mwili, kiwango cha shughuli za kimwili na historia ya familia. Kwa hivyo, aina hii inaweza kuzuiwa kwa kurekebisha mtindo wa maisha mapema.

Chumba cha huduma za macho katika Hospitali ya Shree Hindu Mandal

Kisukari wakati wa ujauzito kinaweza kutokea kwa wanawake wajawazito ambao hapo awali hawakujulikana kuwa na kisukari. Mtoto pia yuko katika hatari ya kunenepa kupita kiasi na kupata kisukari. Akina mama wenye hali hii wanaweza kupata nafuu baada ya kujifungua, lakini uwezekano wa kupata kisukari baadaye ni mkubwa zaidi kwao.


Hatua za kuzuia kisukari ni pamoja na kuishi mtindo wa maisha unaozingatia afya, kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara na kula vyakula vyenye afya visivyo na sukari, wanga na mafuta mengi.


Inashauriwa kufanya mazoezi kwa dakika 30-45 mara tatu hadi tano kwa wiki. Watu walio katika hatari kubwa zaidi kama vile walio na historia ya ugonjwa huo katika familia zao, mafuta mengi, uzito mkubwa kupita kiasi mara nyingi wanahitaji mpango binafsi wa lishe. Katika Hospitali ya Shree Hindu Mandal mtaalamu wa lishe hutoa huduma hii bila malipo.


Vipimo na usimamizi


Vipimo vya mapema ni muhimu, na ni gharama nafuu. Kipimo rahisi cha sukari kwenye damu kinaweza kusaidia kugundua ugonjwa wa sukari. Ukipata dalili zozote za kawaida za kisukari (zilizoonyeshwa kwenye jedwali hapa chini) unapaswa kuonana na mtaalamu wa afya. Katika kituo kilichotajwa hapo juu, kuna timu ya madaktari nane wanaofanya kazi muda wote ambao wanaweza kupatikana mara kwa mara na kwa urahisi.

                Dalili za Kisukari

Kwenda haja ndogo mara kwa mara

Kupata ganzi kwenye miguu ama mikono

Kupata kiu mara kwa mara

Kuwa na njaa kupita kiasi

Kupungua uzito

Uchovu uliopitiliza

Mdomo kuwa mkavu

Kuwa na uono hafifu


Kama sehemu ya tathmini ya mtu mwenye kisukari, matatizo mbalimbali yanahitaji kuchunguzwa na kushughulikiwa. Haya ni pamoja na matatizo ya figo, macho, moyo na mishipa ya damu, maambukizi, neva, meno, viwango vya cholesto pamoja na majeraha ya muda mrefu ya miguu.

Hospitali hiyo hutoa huduma hizi kwa wanaolipa pesa taslimu pamoja na wateja walio na bima.


Wakati wa kutibu watu wenye ugonjwa wa kisukari, mbinu za kitaalamu ni muhimu. Wagonjwa “wanawezeshwa" kwa kupewa ushauri na usaidizi ili waweze kudhibiti kiwango chao cha sukari kwenye damu, kuwa na mbinu sahihi za mtindo wa maisha, kufuata ushauri wa dawa (za kunywa au insulini) na kuzuia matatizo yanayoweza kutokea kutokana na udhibiti mdogo wa sukari kwenye damu.


Moja kati ya ushauri muhimu kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari ni huduma ya miguu. Kila tatizo hugunduliwa na kudhibitiwa na wataalam husika kwa kushirikiana na wataalamu wa homoni za mzunguko wa damu (endocrinologists) na wataalamu wa lishe.


Hospitali ya Shree Hindu Mandal na huduma za kisukari


Hospitali ya Shree Hindu Mandal, Dar es Salaam ni moja ya hospitali zinazotoa huduma ya kina ya matibabu ya kisukari. Hospitali hiyo imekuwa nguzo muhimu katika utoaji huduma za uchunguzi, ushauri na udhibiti wa kisukari na matatizo yanayosababishwa na ugonjwa huo nchini.


Mganga wa hospitali hiyo, Dk Thuraiya Hashim anasema Hospitali ya Shree Hindu Mandal inapokea wagonjwa wengi wa kisukari kutokana na mbinu yake ya kipekee ya kudhibiti ugonjwa huo na matatizo yake. Anasema wanatoa huduma za uchunguzi na ushauri kwa wagonjwa wa rika zote katika siku saba kwa wiki jambo ambalo limewavutia wagonjwa wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini.


Dk Thuraiya anasema kisukari husababishwa na aina ya mtindo wa maisha katika jamii zetu: "Kisukari ni ugonjwa unaotokana na jinsi tunavyoishi maisha yetu, kutokana na uchaguzi wa vyakula na vinywaji, na ikiwa tunajumuisha au kutojumuisha mazoezi ya kutosha kila siku. Huenda tusiweze kubadilisha historia ya familia zetu na magonjwa sugu, lakini kwa hakika tuna uwezo wa kuboresha aina yetu za maisha”.


Ili kuhakikisha kuwa wagonjwa wanapata huduma wanazohitaji, Hospitali ya Shree Hindu Mandal ina idara maalumu za lishe, magonjwa ya moyo, macho na figo. Madaktari pia hutoa ushauri juu ya utunzaji wa miguu kwa wagonjwa ili kuzuia hatari ya kupata vidonda vya muda mrefu vya miguu.


Akifafanua kuhusu vidonda vya miguu vinavyosababishwa na kisukari, Dk Thuraiya anasema tatizo hili hutokana na wagonjwa wa kisukari kupata majeraha madogo kwenye miguu ambayo yakipata maambukizi huweza kuwa makubwa kwa haraka zaidi.


"Vidonda vya miguu vya kisukari ni tatizo kubwa miongoni mwa wagonjwa wa kisukari, wengi wao hupelekea kukatwa miguu yao. Kwa hiyo, kuzuia kwa kutoa huduma sahihi ya miguu kwa wagonjwa hawa ni bora zaidi" Anasema Dk Thuraiya.


Shida nyingine ambayo imesahaulika ni matatizo ya macho. Uchunguzi wa mara kwa mara wa macho ni mbinu muhimu pamoja na kuzuia kiwango cha sukari kwenye damu.


Mara nyingi, hospitali hupokea wagonjwa wa kisukari ambao pia wana matatizo mengine ambayo bado hajayafahamika kama vile mishipa ya fahamu, macho, figo na moyo.


Aidha, hospitali hiyo pia inatoa huduma za matunzo ya wagonjwa majumbani kwa wagonjwa wote ili kuhakikisha wanafuata utaratibu na matunzo jinsi wanavyoshauriwa na madaktari wao. Kupitia huduma zake za kisasa, Hospitali ya Shree Hindu Mandal imefanikiwa kusaidia maelfu ya wagonjwa wa kisukari nchini.


Dk Thuraiya anashauri kwamba ili kujikinga na ugonjwa wa kisukari tunapaswa kufanya vipimo vya afya zetu mara kwa mara na kutafuta ushauri wa kitaalamu kuhusu ugonjwa huo na jinsi ya kuboresha tabia za maisha.


Ikiwa tayari umegunduliwa na ugonjwa wa kisukari ni muhimu kuwa na kliniki za ufuatiliaji wa mara kwa mara na daktari wako ili kuhakikisha kuwa uko kwenye njia sahihi ya kudhibiti ugonjwa huo ili kuboresha ubora wa maisha yako.