Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Strategis insurance yaungana na Vitality Health International kuhamasisha mtindo bora wa maisha kiafya

Dar es Salaam. Kampuni ya Strategis Insurance imeingia makubaliano na Vitality Health International ya kutoa bidhaa bora ya bima nchini.

Ushirikiano huo unalenga kuboresha afya na ustawi wa Watanzania. Bidhaa hiyo ya afya yenye upekee nchini imebuniwa mahsusi kusaidia kampuni na taasisi mbalimbali kuimarisha afya za wafanyakazi wao kupitia sera zao za bima.

Pia, utoaji wa huduma za bima ya afya chini ya ushirikiano huo ni wa hadhi ya juu kwa kuwa umejikita kuleta matokeo bora ya afya za watu huku ukiendelea kuboresha na kulinda maisha yao.


Vitality health international ni nani?

Vitality Health International inamilikiwa na kampuni ya bima ya Afrika Kusini iliyoshinda tuzo nyingi, Discovery, ambayo ilianzisha mfumo wa huduma za bima wa ubia huko Afrika Kusini, ambao umeleta mageuzi katika sekta ya bima ambapo umejengwa katika utaratibu wa kuwapa zawadi watu wanaotunza afya zao kwa mtindo wa maisha yenye afya, na kujenga ushirikiano wenye mafanikio duniani kote na kampuni kubwa za bima.

Leo, Kampuni ya Discovery inaendesha shughuli zake katika masoko zaidi ya 40, na kubadili maisha ya zaidi ya watu milioni 35 duniani kote. Tangu k u a n z i s h w a kwake Januari 2022, Vitality Health International imeendelea kujijengea heshima kwa kuleta bidhaa zabima ya afya ambazo ni chachu ya k u i m a r i s h a afya za vikundi vya waajiriwa barani Afrika.

Mbali na Tanzania, kampuni hiyo ya bima ya afya tayari imetanua wigo wake kufikia katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ghana, Kenya, Msumbiji, Nigeria na Zambia.

Strategis ni mshirika wa bima ya afya nchini wa Vitality Health International, ambaye amekua kinara wa kutoa huduma bora ya bima ya afya kwa waTanzania.

Vitality Health International inalenga kutoa bima bora ya afya nchini wakati huo huo ikiendelea na ufikishaji huduma kama hizo katika nchi nyingine barani Afrika.

Ikijengwa katika misingi ya ubora, kujitoa na uwajibikaji, Strategis Insurance inatoa huduma zake katika mikoa yote nchini Tanzania,

na pia huduma zake zinayafikia mataifa mbalimbali.

Kwa pamoja, Vitality Health International na Strategis wamejitolea kuimarisha ubora wa maisha ya watu barani Afrika na kuufanya ushirikiano uliopo uwe na faida kwa pande zote mbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Strategis Insurance (upande wa bima ya afya), Dk Malav Manek, anasema: ‘ Tunaamini ushirikiano huu utaleta mabadiliko makubwa kupitia mfumo wake unaotumia teknolojia na kutoa rejesho au zawadi kwa wale wateja ambao watakua wameonesha kiwango kizuri cha mtindo wa Maisha kinachowaepusha na maradhi yasiyo ya kuambukizwa .”

Mfumo wa bima ya afya ya pamoja wa Vitality Health International umejikita kwenye mpango wa kisayansi wa kubadilisha tabia ambao umethibitishwa kupitia utafiti huru kuweza kuleta matokeo bora ya afya.

Mpango huo tayari umejumuishwa katika mfumo wa bima ya afya

wa Vitality Health International. Mpango huu mahiri wa kubadilisha tabia unachanganya chambuzi za data, zawadi na motisha, ambazo huwahimiza watu moja kwa moja kufanya machaguo bora

zaidi.

Mfumo huo wa bima ya afya ya pamoja huwezesha wafanyakazi, waajiri na kampuni ya Vitality Health International kugawana kwa pamoja thamani na faida za mtindo wa maisha unaozingatia afya kwa kupunguza gharama za huduma za afya kwa waajiri na wafanyakazi, huku ikipunguza hatari za madai ya bima kwa Vitality Health International.

Waajiri hurudishiwa hadi asilimia 10 ya fedha zao kwa kuwahimiza wafanyakazi wao kufanya mazoezi na kuishi mtindo mzuri wa maisha, ambao huanza kazi pale wanachama wanapokamilisha Tathmini ya Afya ya Vitality, hatua hiyo inaongeza mafao ya waajiriwa ambao ni wagonjwa wasiolazwa nchini kufikia hadi Dola za Marekani 100, kutegemeana na ukamilifu wa tathmini ya afya ya Vitality na ushirikiano chanya utakaotolewa katika programu za Vitality.

Wafanyakazi wa kampuni mbalimbali wanaweza kushinda zawadi kabambe za kila wiki kwa kukamilisha malengo yao ya kila wiki (ikiwa ni pamoja na malengo yao binafsi, yale ya kiakili, siha na mtindo wa maisha), wafanyakazi watajinyakulia zawadi au wanaweza kutumia kiasi cha zawadi walichopata kama mchango wa chanjo za magonjwa kwa wenye uhitaji..

Mkurugenzi Mtendaji wa Vitality Health International, Emma Knox, anasema: “Msingi wa Mfumo wa Bima ya Afya ya Pamoja wa Vitality upo katika kuwatuza watu kwa mtindo bora wa maisha unaozingatia afya zaidi, ambao unaboresha ustawi wao wa kimwili na kiakili, unaokuza uzalishaji na kupunguza hatari za bima ya afya kwa waajiri. Kupitia mfumo huu, Vitality Health International inachangia katika kujenga jamii yenye afya bora kwa kuhakikisha kampuni mbalimbali na wafanyakazi wao wanabaki na mtindo wa maisha unao fanya wawe na afya njema.”

Programu ya Vitality pia huwezesha Vitality Health International kuendesha semina mbalimbali kwa waajiri.Wigo mpana wa mafao ya bima za afyaIkijengwa kwa msingi wa mahitaji ya kipekee ya kila soko inakofanyia kazi, Vitality Health International imebuni wigo mpana wa mafao ya bima za afya inayoanzia hapa nchini, barani Afrika na duniani kote (ukiondoa Marekani), iliyopangwa kulingana na mahitaji na bajeti ya kila mwajiri.

Vitality Health International inayo machaguo matano ya bima ya afya, yenye vipengele mbalimbali kwa mafao yote. Waajiri wanaweza kuchagua wafanyakazi wao kujumuishwa ndani ya Programu ya Vitality inayowafaa Zaidi.

"Kupitia program hii , sio kwamba tumedhamiria kuongeza na kukuza upatikanaji wa bima peke yake bali tunahamasisha mtindo mzuri wa maisha kwa wateja wetu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kupunguza na kuzuia uongezekaji wa magonjwa yasiyoambukiza’’ anahitimisha Dk Manek Malav