T-MARC Tanzania: Ufahamu wa elimu ya hedhi na hedhi salama ni jambo la msingi kwa Taifa


pedipic

Hedhi kwa wanawake ni jambo lisilozungumzwa hadharani katika jamii nyingi Tanzania kutokana na imani za kidini na kitamaduni.

Hedhi kwa wanawake ni jambo lisilozungumzwa hadharani katika jamii nyingi Tanzania kutokana na imani za kidini na kitamaduni.

Vivyo hivyo ushiriki wa wanaume katika suala la hedhi lina pande mbili, baadhi wanaunga mkono na wengine wanapinga na kuona kwamba ni suala la siri na jinsia moja.

Licha ya kuwepo kwa kampeni na harakati nyingi katika jamii kupitia vyombo vya habari bado uelewa na mwamko wa hedhi salama ni mdogo.

Kampeni hizi zimeibua hisia tofauti miongoni mwa jamii kwani wapo ambao wanachukizwa wakiamini kuwa si jambo sahihi kuzungumzia suala la hedhi hadharani kwa sababu tu ya tamaduni kitu ambacho kwa namna moja au nyingine husalia kama kizingiti katika harakati za kuleta uelewa juu ya hedhi salama hasa kwa vijana.

Wasichana wengi walioko shule wanakumbana na changamoto kubwa ambayo inaathiri masomo yao na kufifisha ndoto zao kutokana na kutokuwa katika mazingira mazuri yanayowafanya wawe na hedhi salama.

Inatajwa kuwa nyenzo za msingi ili kufanikisha hedhi salama mashuleni ni; elimu sahihi kuhusiana na hedhi, upatikanaji wa vifaa vya kujihifadhia, maji safi na salama, chumba cha kujistiri,  matundu ya vyoo ya kutosha, walimu na walezi wanaojali na bajeti ya kuwezesha kununua taulo za kike (pedi).

Akizungumzia kuhusu hedhi na hedhi salama, Balozi wa Flowless Sanitary Pads, Dk Romana Malikusema anasema hedhi ni hali au kipindi katika kila mwezi ambapo binti aliyebalehe au mwanamke ambaye hajafikia ukomo ki umri anatokwa na damu kupitia maumbile yake ya kike/ukeni kwa muda wa siku tatu hadi saba katika kila mwezi.

Dk Romana anasema hii ni kwa sababu baada ya kubalehe kila mwezi mwili wa mwanamke unaandaliwa kubeba mimba, hivyo ikitokea hakubeba basi kuta za kizazi chake huporomoka na kuonekana kama damu kila mwezi na hii ndiyo hufahamika kama hedhi.

“Hedhi salama hufanyika pale ambapo binti au mwanamke yuko katika mazingira rafiki ya kupata taulo salama za kike zenye ubora kwa afya yake ya uzazi, uwezo wa binti/ mwanamke kupata maji safi na sabuni kuhakikisha anaoga vizuri na kunawa mikono anapohitaji kubadili taulo, mwongozo wa kiafya katika changamoto anazozipata wakati yuko katika hedhi na uwezo wa kuhifadhi na kuteketeza taulo ambayo amekwishatumia kwa usalama wake na mazingira kwa ujumla,” anasema Dk Romana.

Anasema ili msichana awe na hedhi salama anatakiwa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu hedhi na hedhi salama kwa ujumla, taulo za kike zilizo sahihi na matumizi sahihi ya taulo hizo, upatikanaji wa maji safi na sabuni katika kipindi chote cha hedhi kwa sababu akikosa vitu hivi muhimu anaweza kupata madhara ya kiafya ikiwamo; changamoto katika afya ya uzazi hasa kwa siku za usoni, maambukizi katika mfumo wa mkojo mfano; fangasi au kushindwa kuendelea na shughuli zake hivyo kumrudisha nyuma kielimu au kimaendeleo.

Nafasi ya T-MARC Tanzania katika kuhakikisha suala la hedhi salama katika jamii

T-MARC Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kuboresha afya na kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi. Bidhaa na jitihada zetu za kubadilisha tabia za wanajamii zinalenga kuboresha afya za watu katika kupanga uzazi na afya ya uzazi, afya ya mtoto, maji na mazingira safi, lishe bora na kupambana na magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza kama vile malaria, Ukimwi na saratani ya mlango wa kizazi.

Meneja Programu Mwandamizi wa T-MARC Tanzania, Hamid Al-Alawy anasema suala la hedhi limekuwa changamoto kubwa hususani kwa wasichana walioko shuleni kwani wengi wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa kwenye hedhi kwa sababu wanaogopa aidha kuchekwa na wanafunzi wenzao na hata wakati mwingine kutengwa.

T-MARC Tanzania imekuwa mshirika mzuri wa Serikali na wadau wengine wa maendeleo katika kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa kuhusu hedhi salama.

“Tumefanikiwa kutekeleza miradi ya hedhi salama kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo ilijikita katika utoaji wa elimu kwa jamii kuanzia kwa waratibu wa elimu ngazi ya kata, walimu, wanafunzi, , wenyeviti wa vijiji, viongozi wa shule, Afisa Elimu wilaya/halimashauri hadi mkoa. Elimu hiyo iliambatana na utoaji wa taulo za kike bure kwa wanafunzi,” anasema Al-Alawy.

Anasema miradi hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo wanawake na wasichana wakati wa hedhi, kutoa suluhisho chanya na za kibunifu zinazosaidia kukabiliana na changamoto hizi, kushiriki katika mazungumzo ya sera na kutetea ujumuishaji wa usimamizi wa hedhi salama katika sera na mipango ya kijamii na kitaifa.

Kwa upande wa taulo za kike, mabadiliko ya teknolojia yamesaidia upatikanaji wa taulo   zinazomfanya mwanamke /msichana kuwa huru, kujiamini na kuweza kuendelea na shughuli nyingine pindi anapokuwa kwenye hedhi.

Taulo za kike za Flowless ni chapa inayomilikiwa na kusambazwa na Taasisi ya T-MARC Tanzania, ni bidhaa sahihi ambayo imekuja kuleta mapinduzi katika kusaidia wanawake na wasichana nchini kuwa na hedhi salama.

Akizungumzia kuhusu taulo hizo Meneja Masoko wa T-MARC Tanzania, Alpha Joseph anasema ujio wa Flowless (Taulo ya Kike yenye ubora wa hali ya juu) ni uthibitisho wa nia thabiti ya taasisi hiyo ya kuendelea kuboresha maisha kwa kuhakikisha wanashiriki moja kwa moja katika kukuza uelewa wa jamii kuhusu hedhi salama kwa Watanzania.

“Taulo za kike za Flowless zimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kwa kutumia pamba laini inayosaidia kufyonza unyevu kwa haraka na uhakika zaidi. Taulo hizi ni nyembamba jambo linalomfanya mtumiaji kuwa huru wakati wowote. Ubora wake ni wa hali ya juu na salama,” anasema Joseph.

Anasema, Flowless Sanitary Pads zimetengezwa madhubuti kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwaenzi wasichana na wanawake katika siku zao za hedhi. Pakiti moja ya Flowless inakaa taulo kumi na inapatikana kwenye maduka madogo na makubwa Tanzania nzima kwa bei ya shilingi 3,000 tu.

Joseph anasema suala la hedhi kila mtu analifahamu hivyo watu wote wana wajibu wa kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu hedhi salama.

“Natoa wito kwa Watanzania, wasichana, kinamama na kinababa tuwasitiri vizuri dada zetu, wapenzi wetu wanapokuwa kwenye siku zao za hedhi kwa kutumia taulo za Flowless zenye ubora uliothibitishwa na mamlaka za ubora za kitaifa na kimataifa,” anasema Joseph.


T-MARC Tanzania na maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani

Al-Alawy anasema “Suala la hedhi limekuwa la usiri na lisilojadiliwa kwa uwazi hivyo Umoja wa Mataifa (UN) na Jumuiya za Kimataifa ikiwemo taasisi isiyo ya kiserikali WASH United ya Ujerumani ziliamua Mei 28 ya kila mwaka iwe siku ya hedhi salama ambapo Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi, vyombo vya habari na watu mbalimbali huja pamoja kusherehekea siku hiyo na kutetea umuhimu wa usimamizi mzuri wa hedhi salama pamoja na kutambua changamoto wanazopitia wasichana na wanawake wakati wa hedhi,” anasema Al-Alawy.

Anasema siku hii huadhimishwa ili kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya hedhi na hedhi salama kwa sababu jamii ina uelewa mdogo kuhusu hedhi.

“T-MARC Tanzania tunaiadhimisha siku hii kwa kutoa elimu ya hedhi salama kwa jamii kupitia vyombo vya habari vya redio vya Clouds Fm (vipindi vya Power breakfast na Leo Tena) pamoja na Efm (kipindi cha uhondo), magazeti (Mwananchi na The Citizen) na mitandao ya kijamii,” anasema Joseph.

Anasema katika maadhimisho ya mwaka huu pia T-MARC Tanzania itashirikiana na Chama cha watu wenye sickle cell (Seli Mundu)Tanzania (Sickle cell Disease Patients Community of Tanzania) katika kutoa elimu ya hedhi salama na misaada ya taulo za kike kwa wanawake wenye matatizo ya ugonjwa huo. Hii itafanyika kwenye Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani  na  Wilaya ya Temeke, mkoa wa Dar es Salaam.

Mikakati T-MARC Tanzania

Joseph anasema T-MARC Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu hedhi salama kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kuendelea kushirikiana na vijana katika matukio mbalimbali yanayowakutanisha vijana wa kike, kuboresha upatikanaji wa bidhaa za Flowless, na kuendelea kuboresha ustawi wa wasichana na wanawake wote.

Ujumbe na wito kwa Watanzania

Joseph anasema kwa niaba ya T-MARC Tanzania ninawatakia wanawake wote maadhimisho mema ya siku ya hedhi salama duniani. Tunapoadhimisha siku hii kila mmoja anatakiwa kutambua kwamba ana jukumu la msingi la kuhakikisha jamii inayomzunguka iko salama katika masuala ya hedhi. Kumbuka nguzo mojawapo kuu ya hedhi salama ni matumizi sahii ya taulo za kike zenye ubora; hivyo nawasihi wanawake wote wa Tanzania kuanza kutumia sasa taulo za Flowless kwa afya na usalama sahihi wa hedhi.

Imeandikwa na Jafari Juma, Mwananchi