Tanzania yasherehekea kukamilika kwa mradi wa reli ya SGR na Yapi Merkezi
Sponsored by Tanzania Railways Corporation
Tanzania inayo furaha kutangaza kukamilika kwa mafanikio kwa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Dodoma, mafanikio makubwa yaliyochangiwa na Yapi Merkezi.
Hatua hii muhimu katika maendeleo ya miundombinu ya Taifa inaashiria ukurasa mpya wa uunganishaji, ukuaji wa uchumi na maendeleo ya teknolojia kwa Tanzania.
Ushuhuda wa ubora na ubunifu
Yapi Merkezi, kampuni maarufu duniani ya ujenzi na uhandisi, imekamilisha mradi huu wa kimapinduzi uliotekelezwa kwa utaalamu wa kipekee, usahihi na kujitoa. Kujitoa kusikotetereka kwa kampuni hiyo pamoja na ubora na ubunifu kumekuwa sehemu muhimu katika kutimiza maono ya upatikanaji wa mfumo wa reli wa kisasa.
Reli mpya ya SGR itaimarisha ufanisi katika masuala ya uchukuzi, kupunguza muda wa kusafiri na kuwezesha usafirishaji wa mizigo na abiria kwa urahisi.
Mradi wa SGR, uliotekelezwa na Yapi Merkezi Insaat ve Sanayi Anonim Sirketi, ulijumuisha usanifu na ujenzi wa sehemu ya reli kutoka Dar es Salaam hadi Isaka, zenye jumla ya kilomita 1,000. Mradi umewekeza zaidi ya asilimia 70 ya fedha katika uchumi wa Tanzania kupitia wasambazaji bidhaa wa ndani, wakandarasi wadogo na wafanyakazi, hii ni kuonyesha dhamira ya Yapi Merkezi katika kusaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Pongezi za Rais Samia Suluhu Hassan
Katika hotuba yake, Rais Samia Suluhu Hassan aliipongeza Yapi Merkezi kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Tanzania.
“Mradi huu unasimama kama ushuhuda wa uwezo na taaluma ya Yapi Merkezi. Juhudi zao zisizo na kikomo na kufuata viwango vya juu zaidi vimefungua njia kwa mustakabali mzuri wa Taifa letu. Reli ya SGR bila shaka itakuwa na umuhimu mkubwa katika safari yetu kuelekea ustawi wa kiuchumi na ushirikiano wa kikanda.” Alisema Rais Samia.
Shukrani kutoka kwa Masanja Kadogosa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa pia alitoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Yapi Merkezi.
“Kukamilika kwa mafanikio kwa reli ya SGR ni hatua muhimu inayoakisi nguvu ya ushirikiano wetu na Yapi Merkezi. Utaalamu na kujitoa kwao katika utekelezaji kwa wakati umekuwa wa kupigiwa mfano. Reli hii sio tu ishara ya maendeleo, lakini pia ni kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania.”
Neno la shukrani kutoka Yapi Merkezi
Dk. Erdem Arioglu, Makamu wa Rais wa Yapi Merkezi, alitoa shukrani zake kwa uongozi wa Tanzania na TRC. “Tunajivunia sana kuwa sehemu ya mradi huu wa kihistoria. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Shirika la Reli Tanzania kwa uaminifu na msaada wao usioyumba.
“Ushirikiano huu wenye mafanikio unasimama kama ushuhuda wa nguvu ya ushirikiano na maono ya pamoja. Tunatazamia kuona matokeo chanya ya reli hii katika mustakabali wa ukuaji wa Tanzania.”
Urithi wa ubora
Kujitoa kwa Yapi Merkezi katika utekelezaji wa mradi huu kumeweka kigezo kipya katika ujenzi wa reli na uhandisi. Mipango yao, mbinu za kibunifu za ujenzi na kuzingatia uendelevu vimehakikisha uwepo wa mfumo wa reli wa kiwango cha kimataifa.
Mradi wa SGR ni mfano wa ushirikiano wenye mafanikio kati ya Tanzania na Yapi Merkezi unaoonyesha nguvu ya ushirikiano katika kufikia malengo makubwa kwa pamoja.
Mikakati ya mbele
Tunaposherehekea mafanikio haya muhimu, tunatazamia kuendelea kushuhudia matokeo chanya ya reli ya SGR katika maendeleo ya Tanzania. Mradi huu ni msingi katika mazingira ya miundombinu ya Taifa letu na unaangazia mustakabali wa kuimarishwa kwa uungannishaji, ukuaji wa uchumi na ushirikiano wa kikanda.
Kuhusu Yapi Merkezi
Yapi Merkezi ni kampuni ya kimataifa inayoongoza katika ujenzi na uhandisi yenye historia ndefu ya kutekeleza miradi mbalimnbali ya miundombinu ulimwenguni kote. Yapi Merkezi inayojulikana kwa mbinu zao za ubunifu na kujitoa kwa ubora, huweka viwango vipya katika sekta hiyo kila mara.