TCC yasherehekea miaka 60 ya fahari

Meneja Usambazaji na Usafirishaji wa TCC Plc Abaswege Mwakipiti (kushoto) akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo (wa pili kushoto), wakati alipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirika wa kampuni hiyo Patricia Mhondo na Mwenyekiti wa bodi ya TCC Plc, Paul Makanza.

Muktasari:

Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc) ilizinduliwa kama 'East African Tobac­co na Mwalimu Julius Nyerere Decemba 4, 1961 siku tano tu kabla ya Tanganyika kupata uhuru kutoka kwa Uingereza. Pamoja na mwanzo wao wa pamoja katika kipindi hiki muhimu, fahari ya kam­puni na taifa hili imesalia katika muungano katika kipindi chote cha miaka 60 iliyopita.

Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc) ilizinduliwa kama 'East African Tobac­co na Mwalimu Julius Nyerere Decemba 4, 1961 siku tano tu kabla ya Tanganyika kupata uhuru kutoka kwa Uingereza. Pamoja na mwanzo wao wa pamoja katika kipindi hiki muhimu, fahari ya kam­puni na taifa hili imesalia katika muungano katika kipindi chote cha miaka 60 iliyopita.

Katika kipindi hicho chote, safari ya mafani­kio makubwa na hatua nyingi muhimu zilizotim­izwa imeweza kuonekana. Kwani haikua kazi rahisi kuanzisha kitu kipya katika kipindi cha mwanzoni mwa Uhuru wa Tanzania, hivyo safari ya TCC inaleta utofauti wa kiwango cha kip­ekee cha umakini na mata­rajio ambayo yalihakikisha mafanikio yake hata katika nyakati ngumu zaidi.

Baada ya Azimio la Aru­sha lililofanyika mwaka 1967, serikali ilipata asilim­ia 60 ya kampuni. Mwaka 1975, serikali ilipata asil­imia 40 iliyobaki ya hisa na hapo ndipo Kampuni ya Sigara Tanzania ilizaliwa rasmi kama taasisi inayo­milikiwa na serikali kika­milifu. Mwaka 1995, kama sehemu ya sera ya serikali ya kujitenga na biashara TCC, pamoja na makam­puni mengine mengi, ilibi­nafsishwa.

Mwaka 1999, Japan Tobacco International (JTI) ilinunua hisa asilimia 51 kutoka TCC na mwaka 2000 TCC iliorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es salaam huku JTI ikiongeza hisa zake hadi kufikia asil­imia 75.

Tangu wakati huo, thamani ya hisa za TCC imeendelea kukua na kuwa ya juu zaidi katika soko la hisa la Dar es salaam. Ni wazi kuwa TCC imekuwa moja ya hadithi za mafani­kio ya ubinafsishaji nchini.

Historia ya TCC ni muunganisho wa zamani na wa sasa unaowiana na historia adhimu ya taifa kwakua na jicho la matu­maini juu ya siku zijazo.

Kwa maono madhubuti, TCC iliweka jiwe la msingi kwa siku zijazo na baada ya muda mfupi ikawa kiongozi wa soko baada ya kuweka msingi imara katika sekta.

Kwa miaka mingi, TCC imewekeza kwa kiasi kikubwa kwa watu wake na teknolojia, na kufikia uwezo wa uzalishaji wa sigara bilioni 10. Mwaka huu TCC inatarajia kufikia mauzo katika soko la ndani la sigara zaidi ya bilioni 5 na sigara za karibu bilioni 3 katika masoko yake ya nje katika nchi za Kati na Kusini mwa Afrika.

Pamoja na uwekezaji huo wote, mchango wa TCC kwenye mapato ya serikali ume­ongezeka kwa kiasi kikub­wa na kuifanya TCC kuwa miongoni mwa walipakodi wakubwa nchini Tanzania.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, TCC ilireko­di matokeo bora ya utend­aji mzuri na mauzo ya juu zaidi kuwahi kutokea. Kiasi cha mauzo ya ndani kilikua kwa asilimia 16.5 wakati mauzo ya nje yalikua kwa asilimia 3.7; na kiasi cha jumla kiliongezeka kwa asilimia 12.5. Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, na pia TCC imeongeza sehe­mu yake ya soko hadi zaidi ya asilimia 90.

TCC imefanikiwa kuji­patia shangwe na sifa tele katika tasnia na sekta hiyo na ndiyo washindi wa kujivunia wa tuzo nyingi. Hii ni pamoja kua muajiri bora wa Tanzania na Afri­ka kwa miaka 4 mfululizo, Tuzo ya Mwekezaji katika People Gold, OSHA, NBAA, DSE na pia tuzo ya Waziri katika Msaada wa Mipan­go ya Kukuza Ajira kwa Vijana kupitia utekelezaji wa kitaifa wa programu ya mafunzo.

TCC pia imekuwa na mchango mkubwa katika kurudisha kwa jamii kwa kutoa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu, kutoa sapoti ya kiuchumi kwa ajili ya kupunguza umaskini kwa vikundi vya wanawake wajasiriamali pamoja na kutafuta suluhu endelevu kwa jamii na tas­nia kwa ujumla.

Kwa ujumla, miaka 60 iliyopita inaonyesha safari ya kuustaajabisha, had­ithi ya mafanikio, maono yasiyoisha, ya uvumilivu na ukamilifu, ya kujitolea na kufanya kazi kwa bidii, ya uongozi katika biashara na huduma ya jamii bila masharti, yote haya kwa pamoja yamesaidia kui­marisha msingi. wa TCC.

Miaka 60 adhimu ya fahari na urithi, inayorudi­sha kumbukumbu zisizo­kadirika za jana, kushere­hekea leo na ahadi ya kesho iliyo bora zaidi.