Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TotalEnergies kukidhi kiu ya Watanzania katika matumizi ya nishati safi ya kupikia

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Dar es Salaam. Wakati dunia ikipata msu¬kumo mkubwa wa kuhamia katika matumizi ya nishati safi, kampuni ya TotalEnergies ilishachanga karata zake vyema.

Ikiwa na uelewa na uongozi wa soko, uzoefu na bidhaa bora za nishati, kampuni hiyo ilishatambua mahitaji yanayoongezeka ya kila siku ya nishati safi ikiwamo zile za kupikia.

Akifanya mazungumzo na gazeti hili, Mku¬rugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TotalEn¬ergies Marketing Tanzania Limited Getrude Mpangile amesema mwaka 2021 wakati wanabadilisha jina kutoka ‘Total’ na kuwa ‘TotalEnergies’ hatua hiyo ililenga kubadili mtazamo wao kutoka kwenye biashara ya nishati ya mafuta pekee na kwenda katika nishati safi na salama.

"Mwaka 2021, wakati bodi inaazimia na kupitisha uamuzi wa kubadili jina kutoka Total kwenda TotalEnergies haikuwa tu kwa sababu ya jina bali kubadili mtazamo wetu kwenda kwenye nishati safi na salama," amesema Getrude.

Katika kutekeleza ajenda hiyo kwa vitendo, amedokeza kuwa kampuni hiyo imezindua mitungi ya gesi ya kupikia ya TotalEnergies Gas ili kuwawezesha Watanzania kutumia nishati safi za kupikia zenye faida lukuki ikilinganishwa na nishati za jadi.

"Pengine mtauliza kwanini tumezindua sasa na si wakati mwingine wowote, jibu ni kuendana na kasi ya mahitaji ya nishati safi duniani.

Lakini pili, wakati tunajiandaa na mkakati wetu wa kampuni wa mabadiliko kwenda kwenye nishati safi tumekuta Serikali nayo inazindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, hivyo imekuwa kama bahati kwetu."

Akizungumzia ubora na utofauti wa mitun¬gi hiyo, Getrude amesema wameleta bidhaa hiyo sokoni kuwapatia Watanzania uzoefu mpya kupitia mitungi hiyo iliyobuniwa kisasa kwa rangi zenye mvuto, ujazo unaostahili, usalama na gharama nafuu.

"Hata ukiangalia muonekano wake ni wa kuvutia na wa kipekee, lakini kwa juu ya eneo la kufungulia limezingatia usalama wa mtumiaji.

Mitungi hii kama kampuni tunapambana ifikie mikoa yote licha kwa sasa imeshafikia mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku gharama yake ikiwa ni ile anayoweza kumudu kila Mtanzania."

Getrude amesema kampuni hiyo imejid¬hatiti kuwekeza takribani Sh16 bilioni (Dola za Marekani milioni 7) kwa mwaka katika nishati safi ya kupikia, kiasi ambacho kitatu¬mika katika utafiti, utoaji elimu, na kuweka miundombinu ya usambazaji wa nishati safi ya kupikia.

Kupitia mpango huo wa uwekezaji, ame¬sema wanaamini Watanzania wengi zaidi watahamasika kutumia nishati safi ya kupikia katika biashara zao na kuachana na nishati zisizo safi zenye athari nyingi kwa ustawi wao.

"Nishati safi zina faida nyingi. Zinatunza mazingira, zina ufanisi mkubwa na kuokoa muda, yaani muda ambao ungetumika na kwenda kukata kuni badala yake utatumika kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali."

Amebainisha kuwa pia nishati hizo zina faida za kiafya ambapo kundi kubwa la akina mama watajikinga dhidi ya mata¬tizo ya mfumo wa upumuaji, kifua na macho yasababishwayo na hewa ukaa wanayoivuta wakati wa mapishi.

Alipoulizwa kuhusu changamoto zinazo¬chelewesha ajenda ya nishati safi za kupikia nchini kufikia matarajio yake, amesema bado idadi ya Watanzania wanaoutumia nishati zisizo safi ni wengi licha ya jitihada zinazofanywa lakini anaamini mabadiliko yanawezekana na muda si mrefu tutafikia malengo yaliyowekwa.


Wito

Getrude amewaomba Watanzania kuacha¬na na matumizi ya nishati zisizo safi kwani hivi sasa bidhaa za gesi safi za kupikia zimesambaa nchini kote.

Pia, amewahimiza kutumia gesi ya kupikia ya TotalEnergies ambayo ina faida lukuki ikiwamo usalama, ufanisi na unafuu.

"Kwa sasa mitungi ya gesi inapatikana katika vituo vya TotalEnergies na mawakala walioidhinishwa Dar Es Salaam na Pwani lakini lengo ni kusambaza nchi nzima lakini tunahitaji mtandao wa mawakala wakubwa kufanikisha hili na hapa nitoe rai kwa wafan¬yabiashara kuchangamkia fursa hii ya kusam¬baza mitungi hii kwa wateja wa mikoani."

Amesema pamoja na mambo mengine mawakala watakaokuwa tayari kufanya biashara nao watafaidika kwa kupatiwa elimu ya uendeshaji biashara kwa weledi.

Akihitimisha mazungumzo hayo, ame¬waomba pia wamiliki wa vyombo ya moto kufika katika vituo vya mafuta vya TotalEn¬ergies ambavyo ni jumuishi na vinawezesha wateja kupata huduma mseto wawapo vitu¬oni hapo ikiwamo huduma za matengenezo, ubadilishaji oili, uoshaji chombo na huduma za miamala ya fedha migahawa,ma kupata mahitaji ya nyumbani kwenye maduka ya Bonjour.