Urafiki wa Wajapani kwa kila mtu unatengeneza mazingira mazuri kwa Watanzania kujifunza

Elias Balimponya anayesoma masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Hokkaido, Japan.

Muktasari:

Kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao huamua kusoma elimu ya juu Japani.

Kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao huamua kusoma elimu ya juu Japani.

Vikijulikana kwa utoaji elimu yenye ubora wa hali ya juu, vyuo vikuu vya Japani kwa sasa hutoa programu takribani 1000 zinazofundishwa kwa lugha ya Kiingereza (program takribani 150 ni katika ngazi ya shahada ya kwanza na takribani 850 katika ngazi ya shahada za juu).

Fursa ya kusoma na kutunukiwa shahada bila kuwa na uwezo wa lugha ya Kijapani imefanya nchi ya Japan kuwa kitovu maarufu cha elimu kwa wanafunzi na pia kutokana na kuwa na utamaduni mchang-anyiko, usalama na ajabu zaidi gharama nafuu za maisha.

Tumekuandalia ushuhuda wa Watanzania, Elias G. Balimponya na Neema Y. Yohana, ambao ni wanafunzi wa Shahada za Uzamivu (PhD) kwe-nye Chuo Kikuu cha Hokkaido moja ya vyuo vikuu vya Serikali nchini Japan.

Elias alipata ufadhili wa Serikali ya Japani uitwao MEXT (*) (The Ministry of Education, Culture, Sports, Science and Technology-Japan) ambao maombi yake hufunguliwa Aprili kwa Watanzania na husimamiwa na ubalozi wa Japan ulioko Dar es Salaam Tanzania.

Miaka miwili baada ya kuwasili Japan, kwa masomo yake katika Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Kilimo, mke wake Neema ambaye alikuwa akitafuta nafasi ya kujiendeleza kimasomo aliomba kujiunga na vyuo vya Japan na akabahatika kujiunga na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Mifumo ya Ikolojia ya Kilimo.

Simulizi yao hapa chini itakufanya utambue namna Mtanzania anavyoweza kupanua upeo wake kwa kusoma Japani.

Ujumbe kutoka kwa Elias (E) na Neema (N)

Sababu ya kuichagua Japan kwa masomo yangu

(E) Kwanza ni teknolojia ya juu na ya kisasa katika utafiti, nilitaka kujifunza na kufanya tafiti mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya juu nchini Japan.

Pili ni jamii rafiki ya kijapani, moja wa marafiki zangu aliyesoma hapa alikuwa akinisimulia kwamba wajapani ni watu wenye urafiki wa kweli na hivyo nikaiona Japan kama sehemu nzuri ya kuishi takribani miaka minne ya shahada yangu ya uzamivu.

Neema Yohana akifurahia maisha kwenye mazingira mapya nchini Japan.

Tatu ni uzalishaji wa mpunga. Japan imejitosheleza kwa zaidi ya asilimia 100 katika uzalishaji wa mpunga na kwa vile nyanja niliyokuwa navutiwa nayo ni utafiti katika mpunga, niliamini ningepata ujuzi zaidi katika nyanja hiyo kutoka katika Taifa ambalo uzalishaji wake wa mpunga umezidi kiwango cha utoshelevu.

Namna nilivyotafuta na kupata chuo kikuu cha Japani moja ya yanayovutia. Kwanza nilienda “Google” nikatafuta maabara bora yenye shughuli za biolojia ya mpunga na nikapata maabara kwenye Chuo Kikuu cha Hokkaido, kisha nikaenda katika tovuti ya maabara hiyo na nikatuma barua pepe kwa maprofesa kuomba wawe wasimamizi wangu lakini bahati mbaya sikujibiwa.

Nikarudi tena kwenye tovuti ya maabara na kuona orodha ya wanafunzi na kisha nikawatafuta kama wako “Facebook” na kwa bahati nikawapata baadhi wakiwa na account kwenye mtandao huo.

Nikamtumia ujumbe mmoja wapo nikijitambulisha kwake na kumuuliza kama alifaha-miana na maprofesa ndani ya maabara ile. Alinijibu anamfahamu na akafikisha ujumbe wangu kwa profesa yule na kupitia kwake ndiyo nikaanza mawasiliano na profesa wangu.

Kumpata profesa aliyebobea katika kila unachotamani kukisoma kabla hata hujaomba chuo ni jam-bo muhimu sana kwa yeyote anayetamani kusoma shahada ya juu nchini Japan. Unatakiwa kuwa na hali ya kuendelea kutafuta profesa na kutokata tamaa.

Je, kutokujua Kijapani yaweza kuwa kikwazo?

(N) Vyuo vikuu vilivyo vingi nchini Japan hutoa kozi za lugha ya Kijapani bure kwa wanafunzi wao. Nilikuwa na hamu ya kujua Kijapani kwa ajili ya Mawasiliano. Mara nilipowasili na kusajiliwa Chuo Kikuu cha Hokkaido niliamua kujifunza kijapani ndani ya kampasi na ilinisaidia kuwasil-iana na wajapani ndani na nje ya mazingira ya chuo changu. Kwa wenzangu wanaotegemea kuja Japan, kabla ya kuja unaweza kusoma Kijapani ili kupata uelewa tu wa mambo madogo madogo kama salamu. Kozi hizi hutolewa na baadhi ya taasisi na vyuo vikuu vya Tanzania. Unaweza pia kujifunza kupitia kozi za mitandaoni ambazo hutolewa bure.

* Mapendekezo mbalim-bali ya kozi za kujifunza Kijapani hupatikana hapa kwenye tovuti ya. www.studyinjapan-africa.com/learn-japanese

(E) Lugha ya Kijapani inahi-tajika kwa wingi nje ya mazingira ya chuo na hivyo kui-shi vizuri kwenye nchi hiyo kunahitaji angalau uelewa wa mambo ya msingi. Ndani ya chuo, lugha ya Kijapani huwa na umuhimu mdogo kwa saba-bu kozi nyingi za shahada za juu hutolewa kwa Kiingereza.

Hata hivyo kupuuza kujifunza Kijapani si jambo jema.Moja ya kumbukumbu mbaya nisizoweza kusahau ni kukosa Yeni za kijapani 200,000 ambayo ni takribani milioni 4 za kitanzania. Hii ilikuwa ni ruzuku kwa watoto wangu wawili iliyotolewa na Serikali ya Japan kwa familia zenye watoto ili kupunguza makali ya maisha yanayoweza kuwa yalitokana na Janga la UVIKO-19.

Elias Balimponya (katikati) na Neema Yohana (kushoto) wakitoa maelezo kuhusu faida za kusoma Japan.

Lakini ili kupata fedha hizi ililazimika kujaza fomu ya maombi na kila familia yenye watoto ilitumiwa hiyo fomu. Sasa mimi nilipoiona kwenye box langu la barua nikaipuuza na kuendelea na mambo yangu ya shule. Nikapoteza fursa ya kupata milioni 4. Ni bora sana kutopuuza lugha ya Kijapani.

Fursa za kazi wakati unasoma Japani

(N) Ninafanya kazi ya muda katika moja ya viwanda vya kutengeneza chakula. Wanafunzi walio wengi hufanya kazi za muda (part-time jobs) wakati wakiendelea na masomo yao ya vyuo vikuu.

Na hivyo inawezekana kabisa kujilipa ada na kupata hela za kujikimu wakati ukiendelea na maso-mo. Inahitajika tu kuhakikisha kuwa lengo ambalo ni masomo linapewa kipaumbele na kazi za muda ni kama nyongeza.

(E) Ninafanya kazi katika kampuni ya usafirishaji nikipangilia mizigo inayokwenda maeneo mbalimbali, lakini pia nimewahi kufanya kazi katika kampuni inayoandaa na kusambaza vyakula katika moja ya maduka maarufu hapa Japan (7-eleven). Na wakati mwingine nimefanya kazi kama mwalimu wa Kiingereza wakati wa mwisho wa juma katika moja ya shule za sekondari.

Kitu kikubwa ni kuwa kazi za muda hazi-takiwi kabisa kuingiliana na masomo na hivyo nililazimika kutafuta kazi zinazofanywa siku za mwisho wa juma.

Kwangu mimi mazingira ya kazi za muda ni fursa nzuri sana ya kujifunza Kijapani maana hukutana na wajapani wachache sana wanaoweza kuongea Kiingereza na hivyo wewe mwenyewe hulazimika kuongea Kijapani ili kuwasili-ana.

Yapi mazuri ndani ya Japan

(E) Nilikuwa nikiwaza kwamba kuishi na familia wakati huo nikiwa mwanafunzi ingekuwa vigumu Japan. Lakini kwa bahati njema, Japan ina mfumo wa shule za awali ambako watoto wote kuanzia mtoto wa siku 48 hupelekwa asubuhi na kulelewa na kisha huchukuliwa jioni na wazazi wao.

Japan pia ina mfumo wa kutoa kiasi cha fedha kila mwezi (Sh 200,000 kwa kila mtoto) kwa watoto wote ili kumudu gharama za maisha maana watoto hawafanyi kazi.

Haya hufanyika kwa kila raia anayeishi Japan bila kujali kama ni Mjapani au mgeni. Kwa hiyo katika mwaka wangu wa pili nikiwa Japan niliamua kuileta familia yangu na kuishi nao.

(N) Kabla ya kuja Japan-nilidhani Wajapani wanaweza wasiwe watu wa kutoa ush-irikiano kwa wageni au wanafunzi toka mataifa ya nje. Baada ya kuja niligundua Wajapani ni watu wema na wenye usaidizi hata kwa wageni.

Mimi na familia yangu tunakaa umbali wa kilometa karibia 10 kutoka chuoni katikati ya jamii ya Kijapani haswa. Lakini hatujawahi kuhisi upweke na tunapata ushirikiano wa kila hali.

Wito wa Watanzania

(N) Ningependa kuwatia moyo Watanzania wenzangu wanaotamani kusoma masomo ya elimu ya juu kuicha-gua Japan. Hii ni kwa sababu mazingira ya taaluma ni mazuri, rafiki na uwepo wa vifaa vya kisasa na bora katika maabara kwa ajili ya utafiti.

Lakini pia kuchagua kusoma Japan hukuhakikishia kumaliza masomo ndani ya muda pangwa. Tuna mifano hai ya marafiki zetu ambao wamehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Hokkaido.

Kuna fursa za kupata ufadhili ama kabla ya kujiunga na chuo au baada ya kujiunga na chuo kupitia ubalozi wa Japan nchini Tanzania, vyuo vikuu, Serikali ya Japan na kupitia wahisani binafsi ndani ya Japan.

Kubwa zaidi ni urafiki wa Wajapani kwa kila mmoja wakiwemo wageni, hii itamfanya mwanafunzi kuwa na mazingira bora ya kujifunza.

(E) Niko mwaka wa pili wa Shahada ya Uzamivu lakini nahisi kama nina kitu cha kuto-sha kufanya jambo ndani ya jamii yangu. Niwatie moyo Watanzania kuchangamkia fursa ya kusoma Japan. Ni nchi ambayo hutoa elimu lakini pia fursa za kufanya kile ulichokisoma au kutafiti kwa vitendo. Kwa wale wenye umri chini ya miaka 35, kuna fursa nyingi za ufadhili ikiwemo MEXT, JICA (Japan International Cooperation Agency) na kupi-tia mashirikiano kati ya vyuo vikuu vya Tanzania na vile vya Japan.

Kwa wale wenye umri zaidi ya miaka 35, kuna nafasi za ufadhili za kutosha zinazotolewa na vyuo vikuu, mashirika na taasisi mbalimbali ndani ya Japan. Changamoto kubwa kwa watu wa umri wa zaidi ya miaka 35 inayohitaji kutatu-liwa ni kupata udahiri tu chuo cha Japan, kupata nauli ya kuja Japan na kuwa na malipo angalau muhula mmoja.

Baada ya hapo ni rahisi kupata ufadhili wa Masomo kwa kipindi kingine chote kilichobaki. Ni muhimu kuwasiliana na profesa anayetarajiwa kukusimamia ndani ya Japan ili akue-lekeze uwezekano wa ufadhili uliopo baada ya wewe kujiunga na chuo kikuu.

Hivi karibuni tulizindua umoja wa wanafunzi wa kitanzania wanaosoma Japan (The Association of Tanzanian Students in Japan, TSJ).

Nichukue nafasi hii kuwaalika kutembelea mitandao yetu ya kijamii na hasa facebook; (ttps://www.facebook.com/TzStudentsinJapan) na muu-lize maswali mengi kwa kadri mtakavyoweza. Tutakuwepo kusaidia kwa kila hali. Juu ya yote, kusoma nchini Japan ni bora zaidi!

Taarifa za ufadhili wa Serikali ya Japan kupitia MEXT

Kupitia ubalozi wa Japan nchini Tanzania, Watanzania wanaweza kupata fursa ya kuomba ufadhili wa masomo toka Serikali ya Japan. Dirisha la maombi hufunguliwa mara moja kila mwaka mwishoni mwa mwezi Aprili. Tembelea tovuti ya Ubalozi wa Japan nchini Tanzania (https://www.tz.emb-japan.go.jp/) ili kuangalia vigezo na masharti yanayohitajika.

Nyakati za kutuma maombi

Mwishoni mwa mwezi Mei: Mwisho wa kutuma maombi. Mwanzoni mwa mwezi Juni: Orodha ya waliopita usaili wa awali hutolewa Katikati ya mwezi Juni: Mitihani inayohusisha kuandika pamoja na mahojiano.

Namna ya kutafuta vyuo vya Japan

Kwa msaada juu ya kut-ambua nafasi mbalimbali za masomo nchini Japani, “MEXT” ilikabidhi jukumu hilo kwa “Study in Japan Global Network Project Regional Office in Sub-Saharan Africa” ili kutoa taarifa muhimu na haswa juu ya vyuo vipi vya kuomba.

Ofisi hii ina kanzidata ambayo huruhusu watumia kutafuta program wanazopendelea kulingana na kitivo pamoja na shahada ambayo mtu angependa kusoma. Tafadhali tembelea; studyinjapanafrica-portal.com     

Kongamano la kusoma Japan litakalofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia Jumamosi 26/2/2022

Ofisi ya “Study in Japan Global Network Project Regional Office” kusini mwa jangwa la Sahara inapenda kutangza kuwa kongamano la “Soma Japan, Fursa za Masomo ya Juu Nchini Japan kwa Waafrika Februari 2022” liko mbioni kufanyika.

Kama una mpango wa kusoma masomo ya juu nje ya nchi, tafadhali jisajili ili uweze kukutana na watumishi wa vyuo vikuu vya Japan kwa njia ya mtandao siku ya kongamano. Tunafanya kila tuwezalo kufanya siku hiyo ya Jumamosi kuwa ya kum-bukumbu katika maisha yako yajayo.