VICHOCHEZI VYA UWEZO WA UZALISHAJI KWA AJILI YA UKUAJI WA VIWANDA NA BIASHARA NCHINI

Na Donald Mmari na Ahmed Ndyeshobola

VIASHIRIA VYA UKUAJI UCHUMI KWA TANZANIA

Tangu kuanza kwa milenia ya pili, uchumi wa Tanzania umekua kwa zaidi ya asilimia 6 na pato la mtu mmoja mmoja kwa zaidi ya asilimia 3.5 licha ya ongezeko la kasi ya idadi ya watu. Kwa hakika, katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita mwenendo wa ukuaji wake umekuwa juu ya wastani wa Afrika huku kukiwa na muendelezo.

Ukifanya tathmini hata kwa viwango vya dunia, bado mwenendo wake umekuwa mzuri. Kwa kuangalia Kielelezo 1.A, katika kipindi cha 2014-19, wastani wa ukuaji wa pato halisi kwa Tanzania kwa mwaka ulikuwa takriban asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 5.2 kwa nchi zinazoendelea za kipato cha kati, asilimia 4.4 kwa nchi za kipato cha chini (LDCs), asilimia 4.3 kwa nchi zinazoendelea, asilimia 3 kwa dunia, na asilimia 2.8 kwa Afrika.

Matarajio yenye changamoto na athari za UVIKO-19 katika vichochezi vya uwezo wa uzalishaji mali. Kulingana na Kielelezo 1.B, janga la UVIKO-19 limeweka vikwazo katika matarajio ya muda mfupi ya baadaye ya tija na ukuaji wa uchumi. Uwekezaji na biashara hafifu, kupungua kwa nguvu kazi, ucheleweshaji wa mabadiliko ya kiugawaji wa majukumu, mzigo mkubwa wa deni la Serikali na sekta binafsi, na kuongezeka kwa kutokuwa na usawa kiuchuni bado kunaendelea kushusha ukuaji wa uzalishaji. Matarajio ya ushirikiano zaidi wa kibiashara na upanuzi wa minyororo ya thamani ya kimataifa yamezidi kufifia.

Kushuka ghafla kwa biashara na uwekezaji, katika kipindi cha janga la UVIKO-19, kungeweza pengine kuwa na athari mbaya zaidi ya hizi. Licha ya Tanzania kuwa na rekodi nzuri ya ukuaji, hali hii itazifanya nchi nyingi kushuka kwa shughuli za uzalishaji, kupoteza uimara na kusababisha shinikizo na misikumo mipya kwa Serikali husika. Licha ya hayo yote, upande wa pili wa shilingi, janga hilo linaweza bado kutengeneza fursa za ukuzaji tija ikiwamo mabadiliko ya muda mrefu ya kitaasisi na kiteknolojia kwa ajili ya elimu na biashara, kubadilisha minyororo ya thamani ya dunia kuelekea mageuzi makubwa zaidi, na hata kubadilika kwa kanuni na miiko ya kijamii.


VYANZO NA MIENENDO YA UKUWAJI WA UZALISHAJI MALI

Ukuaji wa uzalishaji - yaani ufanisi ambao jamii huchanganya watu wake, rasilimali, na zana zao - na ndiyo kichocheo kikuu cha mchakato wa maendeleo ya viwanda na upanuzi wa biashara, unaosababisha upatikanaji wa mali na kupunguza umaskini. Maboresho ya muda mrefu ya kuimarika kwa kipato katika sekta za viwanda na/au kilimo ndiyo chanzo cha ajira na maisha kwa watu wengi katika nchi zinazoendelea - mafanikio haya yanaweza kupatikana hususan kwa kukuza na kuboresha tija ya uzalishaji mali kwa wafanyakazi wa viwandani na wakulima. ]


Kulingana na Kielelezo cha 2, faida za uzalishaji kwenye kila sekta ya shughuli za kiuchumi ni matokeo ya awali ya kuongezeka kwa msukumo wa kiuzalishaji kwenye kila kitengo cha uzalishaji mali. Ugawaji upya wa rasilimali kutoka katika kampuni zenye uwezo duni kwenda kwenye zile zenye tija zaidi katika uzalishaji huchangia ukuaji wa uzalishaji kwenye sekta ya viwanda kwenye uchumi wowote wa soko - hususan katika nchi za uchumi wa kipato cha chini ambazo kimsingi huwa na mvurugiko wa chumi zake kutokana na kukosa mfumo wa masoko kamilifu, mkwamo na changamoto za kiuratibu, pamoja na uhaba wa kiteknolojia.

Teknolojia mpya hupunguza gharama na kuboresha ufanisi wa utoaji huduma katika nyanja zote za kijamii. Nusu ya ukuaji wa uzalishaji unaorejelewa unatokana na maboresho ndani ya kampuni hupatikana kwa kubuni, kutumia teknolojia mpya, na kutekeleza mbinu bora za usimamizi.

VICHOCHEZI VYA NDANI NA NJE VYA UKUAJI WA UZALISHAJI MALI

Vichochezi vya ndani vya ukuaji wa uzalishaji mali ni pamoja na vipengele vya kitaasisi vinavyoboresha tija na shughuli ambazo huchagiza uwezo wa kampuni. Vichochezi hivi ni kama ifuatavyo:-


Ukuaji wa uzalishaji mali wa ndani wa muda mrefu unachagizwa na ubunifu, uwekezaji katika mtaji halisi, na mtaji wa rasilimali watu ulioimarishwa. Hili linahitaji mazingira rafiki ya ukuaji, yenye taasisi zinazounga mkono jitihada hizo, na uimara wa uchumi mkuu.


Vichochezi vya nje. Misukumo kutoka nje huathiri upatikanaji wa uzalishaji wa kampuni. Sababu hizi za nje zinatoa nafasi kwa kila kampuni kuboresha ufanisi wake (athari ya “ndani”) na kuchochea kampuni yenye ufanisi zaidi kukua kwa kasi kuliko nyingine (athari ya “kati ya”). Hizi ni pamoja na zifuatazo:HITIMISHO NA MAPENDEKEZO YA KISERA

Kuimarishwa kwa uwezo wa uzalishaji mali wa nchi kunajumuisha uwezekano wa uzalishaji, ukuaji wa uchumi, upanuzi wa viwanda na biashara. Rasilimali za uzalishaji, uwezo wa ujasiriamali na muunganiko wa minyororo ya uzalishaji - hutengenezwa na kupitia mabadiliko kila baada ya muda. Wakati jambo hili hutokea kwa uendelevu, uwezekano wa kuwa na pato la uchumi huongezeka na hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi, upanuzi wa viwanda na biashara kwa kadri iwezekanavyo na kwa uendelevu.

Inapendekezwa kuwa mfumo huu wa uchambuzi utumike ili kuwafahamisha wachambuzi wa sera, watendaji wa sekta binafsi, na watoa maamuzi katika taasisi za umma zinazohusika na kukuza uchumi, maendeleo ya viwanda, uwekezaji, upanuzi wa biashara na maendeleo ya sekta binafsi. Jambo hili lipo ndani ya uwezo wa wadau hao kushughulikia changamoto mbalimbali za ukuaji wa uzalishaji mali ambazo Tanzania inaweza kuendeleza kasi yake ya ukuaji, kufikia uwezo wake wa maendeleo, na kupunguza umaskini kwa kiasi kikubwa.