Zana Bora Limited ni kampuni namba moja ya uuzaji wa zana za kilimo, kulipa kodi

Muktasari:

Rais wa Jamhuri ya Muungunao wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan alipokuwa akilihutubia Bunge la Tanzania kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo, Machi 2021 alitoa ahadi ya kuboresha sekta ya kilimo na kuhakikisha inaongeza tija katika kukuza uchumi.

Rais wa Jamhuri ya Muungunao wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan alipokuwa akilihutubia Bunge la Tanzania kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo, Machi 2021 alitoa ahadi ya kuboresha sekta ya kilimo na kuhakikisha inaongeza tija katika kukuza uchumi.

Kwenye hotuba hiyo Rais Dk Samia aliahidi Serikali ya awamu ya sita itaelekeza nguvu kubwa katika kujenga misingi imara ya sekta ya kilimo kwa lengo la kuongeza tija.

Rais Dk Samia alisema watahakikisha upatikanaji wa mbolea ya kutosha na kwa wakati, kuboresha afya ya udongo, kukuza huduma za utafiti na ugani, kujenga masoko imara kwa kujenga miundombinu na mfumo na kuwezesha uuzaji wa mazao ya kilimo nje ya nchi na upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu.

Ahadi hiyo ya Rais Samia ilipokelewa kwa furaha kubwa na wadau wa sekta ya kilimo, wakulima na wananchi wote kwani sekta hiyo inachangia kiasi kikubwa katika pato la Taifa pamoja na upatikanaji wa chakula.

Tangu kipindi hicho wadau mbalimbali waliopo katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo wamekuwa wakiunga mkono juhudi za Rais Samia na Serikali katika kuhakikisha sekta ya kilimo inazidi kupiga hatua.

Moja ya wadau hao ni Zana Bora Limited ambayo inajishughulisha na uuzaji na usambazaji wa zana za kilimo ambazo ndiyo msingi wa kufikia mafanikio ya sekta ya kilimo pamoja na utekelezaji wa sera ya kilimo kwanza.

Kampuni hiyo ina uzoefu wa muda mrefu wa kuuza zana za kilimo mbalimbali ambazo zinapatikana kwa bei nafuu ukilinganisha na sehemu nyingine.

Ukinunua zana za kilimo kutoka Zana Bora Limited utakuwa umejihakikishia usalama na upatikanaji wa vipuri wa uhakika pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi ya zana hizo.

Teknolojia ya kilimo Tanzania (kwa ripoti ya mwaka 2009) ilionyesha kuwa kati ya jumla ya nguvu kazi iliyopo katika sekta ya kilimo nchini ni takriban asilimia 10 tu ilikuwa inatumia kilimo cha trekta, asilimia 20 wanyama wa kukokotwa na wanaotumia njia za asili ikiwa ni asilimia 70.

Hii inaonyesha kuwa kilimo kinategemea zana za mkono na hivyo kukwamisha ongezeko la eneo linalolimwa kila mwaka pamoja na tija katika mazao ya kilimo na hivyo wakulima kupata kipato kidogo.

Mkurugenzi wa Zana Bora Limited, Vijay Jobanputra anasema kwa kuzingatia pengo lililopo katika matumizi ya teknolojia kwenye sekta ya kilimo kwa wakulima wadogo na wa kati nchini, Zana Bora Limited ambayo imeanzishwa na kusajiliwa rasmi mwaka 2010 chini ya Sheria ya Sheria ya Makampuni (Sura ya 212) imejizatiti kuhakikisha inawasaidia wakulima kufanya kilimo cha kisasa kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

“Jina "Zana Bora" linaonyesha vifaa/mashine bora na hivyo ubora wa bidhaa zetu ni kipaumbele cha kwanza kisha gharama hufuata,” anasema Vijay.

Anasema Zana Bora Limited inaamini katika uhusiano thabiti na wa muda mrefu na wateja wake lakini pia uhusiano na ushirikiano wa kufanya kazi na washirika wake chini ya maadili ya msingi ya kampuni hiyo.

Bidhaa za Zana Bora Limited

Kampuni hiyo imekuwa ikiongoza katika uuzaji na usambazaji wa zana bora za kilimo nchini jambo lililosaidia wakulima wa Watanzania kuwa na uhakika wa upatikanaji wa zana hizo kwa urahisi na bei nafuu. Zana Bora Limited inasambaza na kuuza vifaa vifuatavyo;

Kubota Power Tiller RT140

Kubota RT140 ni injini ya dizeli inayopozwa na maji yenye mizunguko minne yenye usawa. Kwa uwezo wa 14HP kwa 2400RPM, Kubota RT140 inajulikana na kuaminika kutokana na uimara wake inayoiwezesha kudumu muda mrefu.

Miongoni mwa faida za kutumia Kubota ni; ina nguvu na imara, inatumia mafuta kidogo, vipuri vyake hupatikana kwa urahisi, ni rahisi kuendesha na ina uwezo wa kulima ekari tano mpaka sita kwa siku.

Bidhaa nyingine ni; mashine za kisasa za kuvunia na kuchakatia mahindi, mashine za ugwagiliaji wa dawa shambani, mashine za kupandia mahindi, mashine za kulimia na kusafishia shambani, mashine za umwagjiliaji wa maji na mashine za kukobolea mpunga.

Hizi zote ni bidhaa ambazo zimezalishwa na kampuni zinazoaminika duniani katika uzalishaji wa zana za kilimo ikiwemo Vidhata ambayo ni mshirika mkuu wa kampuni ya Zana Bora Limited.

Bidhaa hizi zimekuwa mkom-bozi kwa kuwasaidia maelfu ya wakulima Tanzania nzima katika kuboresha shughuli zao za kilimo.

Zana Bora Limited yang’ara tuzo za TRA mwaka 2022

Mafanikio ya Zana Bora limited hayaishii katika utoaji wa zana bora na imara za kilimo pekee bali hata kulipa kodi na kusaidia maendeleo ya Taifa.

Kutokana na ulipaji kodi bora kampuni hiyo imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika tuzo za walipaji kodi bora wa mwaka zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Novemba mwaka huu.

Kampuni hiyo ilishinda tuzo hiyo katika kipengele cha kampuni ndogo bora katika ulipaji wa kodi kwa Wilaya ya Kikodi ya Buguruni jambo ambalo limetokana na juhudi kubwa zinazofanywa na uongozi wa kampuni hiyo chini ya Mkurugenzi wake Vijay Jobanputra.

Tuzo hiyo haikuja hivi hivi bali ni kutokana na nguvu kubwa na jitihada za kampuni hiyo katika kulipa kodi jambo ambalo linawafanya kuwa wadau muhimu wa maendeleo ya Taifa.