Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikakati ya d.light katika kuinua kipato cha Watanzania, kuunga mkono ajenda ya nishati safi

Moja ya vifaa vya kisasa vya sola vinavyoweza kufanya kazi zaidi ya moja ambavyo vinazalishwa na d.light Tanzania Limited. Kifaa hicho kinaweza kutumika kama taa, kuchajia simu na kuwashia redio.

Miongo kadhaa nyuma, mwanga hafifu wa vibatari ndiyo ulikuwa chanzo pekee cha mwanga kwa mamilioni ya kaya vijijini hapa nchini.

Ingawa vilitoa mwanga, gharama madhara yake yalikuwa makubwa ikiwemo kutoa moshi wenye sumu, ajali za mara kwa mara za moto na gharama kubwa za kifedha kwa familia duni nchini.

Leo hii, hali hiyo inabadilika kwa kasi kikubwa. Msingi wa safari hii ya mabadiliko ni d.light Tanzania Limited, kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kijamii ambayo imegeuza nishati ya jua kutoka kuwa bidhaa ya anasa na kuwa nyenzo ya kubadilisha maisha kwa zaidi ya Watanzania milioni 1.5 tangu mwaka 2019.

Mapinduzi ya d.light yanaweza kugawanywa katika hatua tatu kuu; Hatua ya kwanza (2007–2013) ilianza kwa kubuni na kutengeneza taa ndogo za jua ambazo ni za gharama nafuu na imara, huku ikijenga mtandao mpana wa usambazaji Afrika Mashariki, India, na Kusini Mashariki mwa Asia.

Mwaka 2014, kampuni ilifanya mabadiliko makubwa kwa kuanzisha mfumo wa malipo kidogo kidogo (Pay-As-You-Go - PAYG) ili kutoa suluhisho kamili za nishati, na hatua ya mwisho ni kupanua huduma zake kutoka taa za kawaida hadi mifumo kamili ya umeme wa jua wa majumbani (Solar Home Systems - SHS) na vifaa vya kielektroniki.


Ajali ya moto ilivyoanzisha safari ya d.light

Hadithi ya d.light haikuanzia kwenye kumbi za mikutano, bali katika kijiji kidogo huko Benin, Afrika Magharibi. Mwaka 2007, mwanzilishi mwenza, Sam Goldman alishuhudia ajali ya kusikitisha ambapo mtoto wa jirani yake aliungua vibaya baada ya taa ya mafuta ya taa kuanguka.

Wafanyakazi wa d.light Tanzania Limited wakifikisha vifaa vya kampuni hiyo kwenye moja ya vijiji nchini.

Ajali hiyo ilileta mtazamo mpya wa kutokomeza matumizi hatari ya taa za mafuta na badala yake kuleta suluhisho salama, nafuu na endelevu za nishati ya jua. d.light ilianza kama mradi wa ubunifu katika Chuo Kikuu cha Stanford ambapo ilitumia miaka yake ya mwanzo kuboresha taa ndogo na imara kama vile Nova na S250.

Hata hivyo, kampuni hiyo iligundua kuwa teknolojia pekee haitoshi bali kikwazo cha upatikanaji wa nishati safi ni uwezo wa kumudu gharama.

Ugunduzi huu ulipelekea kuanzishwa kwa mfumo wa malipo kidogo kidogo (PAYG) mwaka 2014 ambao ni uvumbuzi wa kiteknolojia wa kifedha ulioruhusu familia zenye kipato cha chini kulipia mifumo ya umeme wa sola kwa awamu kupitia simu za mkononi.


Safari ya d.light ilivyoanza Tanzania

Wakati d.light ikiwa na alama duniani kutokana na kugusa maisha ya zaidi ya watu milioni 210, safari yake nchini Tanzania imekuwa na faida kubwa sana. Tangu kuanza kwa shughuli zake nchini mwaka 2018, kampuni hiyo imepanua wigo katika mikoa 24 na kanda tano.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa d.light Tanzania Limited, Moses Cliff anasisitiza kuwa mafanikio ya kampuni hiyo hayapimwi kwa idadi ya bidhaa zilizouzwa, bali kwa mabadiliko yanayoonekana katika jamii. “Maono yetu ni hadithi ya matokeo chanya,” anasema Cliff.

“Watu wanaposoma kuhusu d.light, nataka waone zaidi ya balbu ya mwanga. Wanapaswa kuona ajira tulizotengeneza, biashara tulizoziunga mkono na maisha tuliyoyabadilisha.

Matokeo chanya ndiyo kigezo chetu kikuu cha mafanikio,” anasema Cliff.

Mafundi wa d.light Tanzania Limited wakifunga paneli za sola kwenye moja nyumba za wateja wa kampuni hiyo.

Cliff anabainisha kuwa, ingawa watu wengi wanahusisha nishati ya jua na maeneo ya vijijini, ushawishi wa kampuni hiyo unaonekana hata mijini.

“Watu wa mijini wanaweza kufikiri hili haliwahusu, lakini d.light inatoa fursa za ajira kila siku kwa watu wa mijini na vijijini. Tunajenga uchumi huku tukitoa suluhisho bora za nishati.”


Kutoka ‘Kibatari’ hadi mifumo ya kisasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani

Mageuzi ya bidhaa za d.light yanaakisi dhamira yake ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya Watanzania.

Meneja Mafunzo wa d.light Tanzania Limited, Ummi Marealle anaeleza kuwa safari ya kampuni hiyo ilianza na kuleta mbadala rahisi wa taa za vibatari zilizozoeleka.

“Tuna bidhaa zilizobadilisha maisha kwa sababu zilibuniwa kuendana na kile ambacho watu tayari walikuwa wanakifahamu, lakini kwa njia safi zaidi,” Ummi anaeleza.

“Tuna bidhaa inayoitwa ‘kibatari’ (S3), ambayo ilikuwa ya kwanza kuanza kuchukua nafasi ya taa hatari mashuleni na majumbani. Hii ndiyo ilikuwa bidhaa halisi kabla ya bidhaa za kughushi zilivyoanza kuvamia soko.” anafafanua Ummi.

Tangu kipindi hicho, d.light imekua na kutoa mifumo kamili ya umeme wa jua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani (SHS). Mifumo hii sasa inaendesha luninga za inchi 32 na 40, feni, na pia kusaidia kuchajia vifaa vingi vya umeme kwa wakati mmoja.

Februari mwaka 2026, kampuni hiyo iliweka viwango vipya sokoni kwa kuanzisha dhamana ya miaka mitano kwa mifumo yake ya umeme wa jua na invata (inverters), ikiwa ni ya kwanza katika sekta ya nishati ya umeme jua nchini.

“Tunataka wateja wetu wafurahie na kuwa na amani ya moyo kila siku,” Ummi anasema

“Dhamana hii inathibitisha kuwa bidhaa zetu si tu za bei nafuu, bali ni imara. Tuko hapa kuwahudumia, tukisaidiwa na mtandao wa mafundi wenye ubora na vituo vya huduma kwa wateja nchi nzima,” anabainisha Ummi.


Uwezeshaji wa kiuchumi na kuwafikia watu

Mojawapo ya mchango mkubwa ya d.light nchini ni mtandao wake mpana wa usambazaji na huduma. Kwa sasa, kampuni hiyo inashirikiana na mawakala zaidi ya 10,000, ikiwa na mtandao wa mawakala 1,000 wanaofanya kazi na zaidi ya timu 200 za utoaji huduma.

Miundombinu hii ya kuwafikia watu wengi inahakikisha kuwa, hata vijiji vya mbali kabisa vinaweza kupata nishati safi na msaada wa kiufundi.

Matokeo ya kiuchumi ni makubwa sana. Mawakala wametumia mapato yao kutoka d.light kujenga nyumba, kununua magari na kuwasomesha watoto wao.

Kwa wamiliki wa biashara ndogo, kama vile mafundi cherehani au wenye maduka katika maeneo yasiyo na umeme, mwanga wa uhakika unaotokana na umeme wa sola unamaanisha kuwa, sasa wanaweza kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi, jambo linaloongeza mapato yao kwa hadi asilimia 83 katika baadhi ya maeneo.

“Tunawawezesha wanawake kwa kuwapa nafasi kama wataalamu wa nishati ya jua na kupunguza mzigo wa kila siku wa kutafuta nishati,” Ummi anabainisha.

Aidha, matumizi ya nishati ya jua yameokoa wastani wa dola 150 (zaidi ya Sh 400,000) kwa kila kaya katika kipindi cha miaka mitano ikilinganishwa na gharama ya mafuta ya taa na betri.


Mustakabali wa matumizi ya nishati safi ya kupikia

d.light inapiga hatua zaidi ya kutoa masuluhisho ya nishati ili kushughulikia masuala mengine muhimu ya kitaifa, haswa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika meneo mbalimbali nchini.

Wakati Tanzania ikitekeleza ajenda ya kitaifa ya nishati safi, d.light inajiandaa kuzindua majiko ya umeme (induction cookers) yanayotumia teknolojia yenye ufanisi mkubwa.

“Tunaingia kwenye sekta ya nishati safi ya kupikia kupitia majiko ya kisasa ya umeme ambayo ni salama, safi, na yanapatikana kupitia mfumo wetu wa PAYG. Hii itaruhusu familia nyingi kuacha kutumia mkaa na kuni, hivyo kulinda afya zao na misitu yetu,” anasema Ummi.

Kwa wakazi wa mijini wanaokabiliana na changamoto za kukatika kwa umeme, kampuni pia hiyo inakuja na mfumo wa akiba wa umeme (smart inverter backup systems). Mfumo huu unatoa umeme bila kukatika wakati wa dharura, ukihakikisha kuwa biashara na shughuli nyingine za kiuchumi zinaendelea kama kawaida pale umeme unapokatika.

“Mkakati wetu ni kuhakikisha tunapanua wigo wa huduma zetu za nishati ili kujumuisha mifumo ya akiba ya umeme na vifaa vinavyofanya kazi kwa kutumia nishati ya jua na umeme wa gridi,” Cliff anabainisha.


Mshirika wa kweli katika maendeleo

Shughuli za d.light zinaendana kwa karibu na Sera ya Taifa ya Nishati na mikakati ya kitaifa ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Kwa kuondoa matumizi ya nishati isiyo safi, bidhaa za kampuni hiyo zimesaidia kupunguza mamilioni ya tani za hewa chafu (CO2) duniani kote na kuchangia katika mkakati wa kulinda na kutunza mazingira.

Jukwaa la “Atlas” la kampuni hiyo, ambalo ni mfumo wa kusimamia akaunti kwa njia ya mtandao, linaonyesh jinsi teknolojia inavyotumika kuziba pengo la ushirikishwaji wa kifedha.