Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jetour kufungua fursa mpya za ajira nchini, Waziri Kapinga aeleza

Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga (Mb), amesema ujio wa magari ya chapa ya kimataifa ya Jetour nchini Tanzania unatarajiwa kufungua ukurasa mpya wa fursa za kiuchumi, hususan katika ujenzi wa ajira kwa vijana katika sekta za mauzo, huduma za kiufundi na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Akizungumza Juni 8, 2026 katika uzinduzi rasmi wa chapa hiyo uliofanyika Super Dome, jijini Dar es Salaam, Kapinga alisema ushirikiano huo hauishii katika kuongeza chaguo la bidhaa sokoni pekee, bali pia unaleta faida kubwa ya uhamishaji wa teknolojia na ujuzi kwa Watanzania.

Amesema kupitia mifumo ya kisasa ya huduma na matengenezo ya magari, mafundi na wataalamu wazawa watapatiwa mafunzo yatakayowaongezea uwezo na kuinua viwango vya ushindani katika sekta ya magari ndani na nje ya nchi.

Aidha, Waziri Kapinga alibainisha kuwa uwekezaji huo unatarajiwa kuchochea mzunguko wa fedha katika sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji, matangazo na huduma za kifedha, hatua inayoonesha mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa taifa.

Uzinduzi huo uliofanyika kupitia ushirikiano kati ya Jetour Global na Africarriers Group, umeelezwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha biashara, kuongeza ushindani sokoni na kusaidia ajenda ya Serikali ya kujenga uchumi wa kisasa unaoongozwa na sekta binafsi.

Kapinga alisema uzinduzi huo ni uthibitisho wa mazingira rafiki ya uwekezaji yaliyoimarishwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia maboresho ya sera na sheria za biashara.

Ameongeza kuwa uwekezaji huo pia unaendana na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano, unaolenga kujenga uchumi jumuishi na imara.

Hata hivyo, Waziri Kapinga aliipongeza kampuni hiyo kwa kuchagua Tanzania kuwa kitovu cha kimkakati cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki, akisisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha wananchi wananufaika na matokeo ya uwekezaji huo.