Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai hakuwezi kuleta mpasuko ndani ya chama hicho kwa kuwa kimeshawahi kupitia mitikisiko mingi lakini kikabaki imara.