Ulanga. Mama wa watoto watatu wa kike wa kijiji cha Gombe wilayani Ulanga mkoani Morogoro waliokuwa wametelekezwa baada ya wazazi wote wawili kuondoka kila mmoja kuoa na kuolewa amejisalimisha kituo cha Polisi Ulanga huku akiomba kurudi kuwalea watoto wake.

Julai 21 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya alipowatembelea watoto hao aliagiza wazazi wawili, Thomas Ulanda na Adelyda Nakashawa wakamatwe.

Tangu wazazi hao waondoke, Elionida Ulanda (17) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Celina Kombani amekuwa na jukumu la kuwalea wadogo zake.