Mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu Hassan ameshaingia katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa chama hicho siku ya pili.

Rais Samia ameingia katika geti Kuu saa 3.00 asubuhi na moja kwa moja msafara wake ulielekea katika Ofisi za chama makao makuu zilizopo ndani ya majengo ya ukumbi huo.

Leo Alhamisi Desemba 8, 2022 mkutano utapokea na kujadili utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo itawasilishwa na Waziri Mkuu kwa Serikali ya Muungano na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar kwa upande wa pili wa Muungano.