Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Henry Mkunda amesema wafanyakazi wanakumbuka kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Mei Mosi ya kupandisha mishahara hivyo wanaamini atatekeleza ahadi hiyo leo.

Mkunda amesema hayo leo hayo leo Jumapili Mei Mosi 2022 katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zinazofanyika katika uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma.