Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukosefu chombo cha usuluhishi wachochea migogoro kazini

Muktasari:

  • Utafiti uliofanywa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) umebainisha sekta ya umma hakuna chombo cha majadiliano kinachosaidia kuleta uhusiano mwema kati ya wafanyakazi na mwajiri

Unguja. Wakati Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (Suza) kikisaini mkataba kuanza ujenzi wa majengo mawili ya maabara na shule ya kilimo kupitia Mradi wa Elimu ya Juu ya Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), uongozi wa chuo hicho umesema umepitia safari ndefu na changamoto nyingi mpaka kufikia hatua hiyo.

Katika mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, Suza ilipata Dola20 milioni Marekani  (Sh53.8 bilioni) ambazo zimegawanywa katika programu ndogondogo na asilimia kubwa zaidi ya kiwango hicho imewekezwa katika ujenzi ili kuweka mazingira mazuri ya miundombinu kwa taasisi.

Mradi huo unajumuisha ujenzi wa miundombinu, ukarabati, ununuzi wa vifaa vya Tehama, kujengea uwezo wafanyakazi kwenye mafunzo ya muda mrefu na mfupi, uanzishaji wa programu mpya na kuzifanyia mapitio mitalaa ya programu za zamani kuendana na mahitaji ya sasa ya soko la ajira.

Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba ujenzi wa majengo hayo na Kampuni ya Mohammed Builders ya Dar es Salaam leo Novemba 5, 2024,  Makamu Mkuu wa Suza, Profesa Moh’d Makame Haji amewataka wahusika kuweka uzalendo na masilahi ya vijana kupata elimu bora.

“Tumepitia pagumu lakini leo tumeweka mkataba wa ujenzi licha ya katikati kumetokea changamoto kidogo, lakini tumekwamuka na leo tupo katika hatua hii,” amesema Profesa Makame.

Amesema ujenzi huo si tu unakwenda kunufaisha Suza kama taasisi bali kwa vijana ambao wapo nje wanatafuta eneo la kupata taaluma bora kwa kujenga maisha yao na kujenga uwezo wa kuchangia maendeleo ya Taifa. 

“Haitapendeza kutokea bahati mbaya,  jambo litakalosababisha kutotekeleza kama mikataba inavyosema, iwe katika muda, iwe katika viwango, katika malipo usimamizi au maeneo yote yaliyotajwa, haitakuwa vyema kama tutaweza kusimamia na kumaliza kama inavyotakiwa,” amesema. 

Amesema Serikali ilifanya utafiti na kubaini upungufu uliopo kwa wahitimu kutoka tasisi za elimu ya juu na ndio badaye ukapatikana mkopo uliokuja kuwezesha taasisi za elimu ya juu ili kuwaandaa vijana watakaokuwa na uwezo wa kusaidia jamii.

Kiongozi wa Kampuni ya Ukandarasi, Nizar Lakhani amesema kwa imani yao watapata ushirikiano na watahakikisha wanafanya kazi usiku na mchana kuumaliza mradi huo kwa wakati na ikiwezekana kabla ya wakati. 

“Kwa uzoefu tulio nao, kuna umuhimu wa mradi wenyewe kila kitu kikienda sawa tunatarajia kufanya kazi usiku na mchana ikiwezekana hata tumalize kabla ya muda ambao upo kwenye mkataba,” amesema. 

Kwa upande wa msanifu majengo kutoka Kampuni ya Arqes Afrika, Lazaro Peter amemtaka mkandarasi kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia misingi ya mkataba.

“Lazima tuwe makini ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati lakini iwe na viwango kwa mujibu wa mkataba,” amesema Peter.