Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Comunications Limited (MCL), Bakari Machumu (kulia) na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Ejat kutoka Kampuni ya Mwananchi wakati wa sherehe za kutoa Tuzo za Umahili wa Uandishi wa Habari kwa mwaka 2015 zilizofanyika Dar es Salaam juzi. Picha na Said Khamis
Photo: 1/7
Mkuu wa Uhusiano wa kampuni ya TBL, Emma Urio akimkabidhi Tuzo ya Mazingira mwandishi wa gazeti la The Citzen, Sauli Gilliard wakati wa utoaji wa Tuzo za Umahili za EJAT. Picha zote na Said Khamis
Photo: 2/7
Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF), Ernest Sungura akimkabidhi mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Nuzulack Dausen Tuzo ya Habari za Uchunguzi.
Photo: 3/7
Mwandishi wa Mwananchi, Shijja Felishian akipokea Tuzo ya Uandishi wa Habari za Mafuta na Gesi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Bg Tanzania G, John Ulanga.
Photo: 4/7
Mwakilishi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Benard Konga akimkabidhi mwandishi mwandamizi wa Gazeti la Mwananchi, Florence Majani, zawadi ya kompyuta mpakato na Tuzo ya Mwandishi Bora wa Habari za Mama na Mtoto.
Photo: 5/7
Mwandishi wa Mwananchi, Mussa Juma akipokea Tuzo ya Habari za Utalii na Uhifadhi kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu.
Photo: 6/7
Mwandishi wa Gazeti la The Citizen, Benard Lugongo akipokea Tuzo ya Habari za Mama na Mtoto kutoka kwa jaji, Kiondo Mshana.