UJENZI WA BARABARA: Mafundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Hanil-Jiangsu Joint Venture LTD, wakiendelea na kazi ya kujenga daraja katika Mto Nduruma, Arusha jana. Ujenzi huo ni sehemu ya upanuzi wa Barabara ya Sakina hadi Tengeru yenye urefu wa kilometa 14.1. Picha na Filbert Rweyemamu
Photo: 1/8
NANI FUNDI HAPA: Mpigapicha kutoka Uingereza, Harry Whitetead akimpiga picha mmoja wa wapigapicha za ‘pasipoti’ anayefanya shughuli zake Mtaa wa Makongoro, Morogoro jana. Picha na Juma Mtanda
Photo: 2/8
MAJI: Mkazi wa Nyamahuna, wilayani Geita , Yohana Lazaro akionyesha kisima cha maji kilichokuwa kikitumiwa na wakazi wa eneo hilo ambacho kimekauka na kusababisha adha kwao. Wakazi hao wamedai kisima hicho kimekauka baada ya mwekezaji kuchimba dhahabu karibu yake.
Photo: 3/8
MACHINGA: Wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwa wakifanya biashara zao nje ya Soko la Machinga Complex lililoko Ilala Dar es Salaam, wakiondoa mabaki ya mali zao baada ya mabanda kuvunjwa asubuhi jana. Picha na Elicky Boniphace
Photo: 4/8
KILIMO: Wakazi wa Jiji la Mwanza wakisililiza maelezo namna kilimo cha mbogamboga kwenye makopo kinavyofanyika kutoka kwa mkulima Victoria Buzale (kushoto) walipotembelea maonyesho ya kilimo yanayofanyika eneo la Capri point. Picha na Ngollo John
Photo: 5/8
BIASHARA: Wakazi wa Mwanza wakianda udongo wa ‘pemba’ eneo la Chakechake, jijini Mwanza. Udongo huo ambao hutumiwa zaidi na wajawazito unauzwa kilo moja kwa sh1,000 hadi 1,500. Picha na Johari Shani
Photo: 6/8
MACHINJIO: Wafanyakazi wa Machinjio ya Kibirizi Kata ya Gungu, Manispaa ya Kigoma-Ujiji, mkoani Kigoma wakiendelea na kazi kabla ya Mamlaka Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kutangaza kuwa machinjio hayo hayana sifa na kuyafunga jana. Picha na Anthony Kayanda
Photo: 7/8
SIASA: Wagombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kupitia vyama vya upinzani, Twaha Taslima (kushoto) na Lawrence Masha wakibadilishana mawazo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi