Snura alalamikia gharama vipimo vya DNA

Thursday January 26 2017

By Elizabeth Edward, Mwananchi [email protected]

Baada ya ukimya wa muda mrefu, mwanamuziki Snura Mushi ameibuka na kuiomba Serikali iangalie uwezekano wa kupunguza gharama za kipimo cha vinasaba (DNA) ili watu wa hali ya chini waweze kumudu.

Snura alisema kipimo hicho kikipatikana kwa urahisi, kitasaidia kupunguza kesi za wanaume kutelekeza watoto na kukataa mimba. Nyota huyo ambaye ni mama wa watoto wawili alisema DNA ikiwa bei nafuu hata watu wasiokuwa na uwezo watamudu kupima tofauti na ilivyo sasa ambako wachache ndiyo hupima