Miti ya Sh421 milioni yateketea kwa miaka mitatu Mashamba ya miti yenye thamani ya Sh421.4 milioni yameteketea kwa moto Wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe kwa mwaka 2020 - 2023.
Sh5.4 bilioni kuboresha barabara mlimani Ludewa Serikali yatenga 5.4 Bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara eneo la mlima Kimelembe kufuatia mtelemko na kona kali zilizopo katika mlima huo.
DC Ludewa ataka kesi zimalizwe kwa usuluhishi Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amewataka wananchi wilayani humo kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ili kuokoa muda wa kufanya shughuli za kimaendeleo.
Wanafunzi watembea kilometa 10 kufuata masomo Ikiwa mkakati moja wapo wa sekta ya elimu ni kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi kujisomea, watoto kutoka Kata ya Ruhuhu Wilayani Ludewa wanalazimika kusafiri umbali wa 10 km kufuata elimu ya...
Binti afariki kwa kupigwa radi Ludewa Binti Calister Haule (15) amefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakati akichunga mbuzi katika Kijiji cha Lifua wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe.
Wafungwa 95 waachiwa huru Gereza la Ludewa Katika maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 1,631 huku wanufaika 95 wa msamaha huo wakitokea Gereza la Wilaya ya Ludewa.
Watoto 96 hubakwa kwa mwaka Ludewa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Andrea Tsere amesema ukatili wa jinsia bado ni tatyizo kubwa wilayani humo, kwani takwimu zimeonyesha wastani wa watoto 96 wamekuwa waakibakwa kwa mwaka.
Atupwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka minne Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe imemuhukumu kifungo cha maisha jela, Simon Msanga (24), mkazi wa kijiji cha Kiwe wilayani Ludewa kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka minne.
Watoto wawili wafariki banda la kuku likishika moto Watoto hao wawili wamefariki baada moto kulipuka katika banda la kuku walimokuwa wakicheza, huku mtoto mwingine akijeruhiwa na moto huo.