Waziri Mkuu kuongoza mkutano tathmini sekta ya mkonge Tanga Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Tathmini ya Maendeleo ya Zao la Mkonge 2020–2023 Machi 6, mwaka huu jijini Tanga.
Wakazi wa Tanga waomba huduma za kibingwa kufika hospitali za wilaya, kata Wakazi wa Tanga wameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kutoa huduma za madaktari bingwa katika Hospitali za mikoa na wilaya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo.
Watatu wafariki malori yakigongana Tanga Watu watatu wamefariki usiku wa kuamkia leo Ijumaa baada ya lori lililokuwa limebeba gesi kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso.
Moto wateketeza ghala Tanga Ghala lililokuwa limehifadhia shehena za bidhaa za magendo ambazo zimeshindwa kulipiwa ushuru na wafanyabiashara limeteketea kwa moto katika Bandari ya Tanga huku chanzo kikiwa bado hakijajulikana.
Kigogo polisi adaiwa kutorosha walionaswa na mali za Sh2.2 bilioni Ofisa upelelezi wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuwaachia huru watuhumiwa wa uhujumu uchumi.
Mashirika binafsi yaanzisha ugawaji chakula shuleni Mpango huo wa chakula shuleni unatarajia kuwafuisha wanafunzi 28,000 kutatua tatizo la utoro Wilaya za Handeni na Mkinga.
Warioba amkumbuka Mrema kwa kuachia uwaziri Warioba amesema Mrema aliamua kuacha nafasi ya Waziri baada ya kutofatiana na wenzake jambo alilosema siyo dogo katika siasa.
Serikali mbioni kukifungua kiwanda cha Mponde Wakati Serikali ikianza mikakati ya kukifungua kiwanda cha chai cha Mponde, baadhi ya wakulima waeleza changamoto ya bei ndogo ya majani ghafi.
Rais aagiza Uhamiaji kudhibiti urasimu kwa wageni Rais Samia amemwagiza Kamishna wa Uhamiaji nchini kudhibiti urasimu katika utoaji wa vibali vya kuishi kwa wageni wachukuliwe hatua kali.
Rais Samia kuanza ziara Tanga Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku mbili Mkoa wa Tanga kuanzia kesho Jumapili, Agosti 14, 2022.