ZBS inaendelea kuweka viwango bora na kusimamia ubora wa bidhaa na huduma


ZBS inaendelea kuweka viwango bora na kusimamia ubora wa bidhaa na huduma

Taasisi ya viwango ina jukumu la kuandaa na kuvisimamia viwango na kusimamia ubora wa bidhaa zote zikiwemo za vyakula, taasisi ina­hakikisha kuwa vyakula vyote viki­wemo vinavyotengenezwa viwan­dani kama vile unga, maziwa na bidhaa zake, mafuta ya kula, mafuta yatokanayo na mimea, pia bidhaa za kilimo kama vile matunda na mboga mboga, bidhaa za oganiki, nafaka, viungo, pia vyakula vya wanyama huwekewa viwango na bidhaa hizi lazima zikaguliwe kati­ka maabara ili kuhakikisha ubora wake ndipo ziruhusiwe kwa matu­mizi ya binadamu.

Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) ni taasisi ya Umma ambayo imeanzishwa mwaka 2012 kupitia sheria ya viwanda namba 1 ya Zan­zibar ya mwaka 2011.

Majukumu makuu ya taasisi hii ni kuweka viwango, kuvisimamia na kusimamia ubora wa bidhaa na huduma hapa nchini.

Kabla ya kuanzishwa kwa ZBS, Zanzibar hakukuwa na taasisi ambayo inasimamia masuala ya viwango vya bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini na zile zinazotoka nje.

Taasisi ya viwango ina jukumu la kuandaa na kuvisimamia viwango na kusimamia ubora wa bidhaa zote zikiwemo za vyakula, taasisi ina­hakikisha kuwa vyakula vyote viki­wemo vinavyotengenezwa viwan­dani kama vile unga, maziwa na bidhaa zake, mafuta ya kula, mafuta yatokanayo na mimea, pia bidhaa za kilimo kama vile matunda na mboga mboga, bidhaa za oganiki, nafaka, viungo, pia vyakula vya wanyama huwekewa viwango na bidhaa hizi lazima zikaguliwe kati­ka maabara ili kuhakikisha ubora wake ndipo ziruhusiwe kwa matu­mizi ya binadamu.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS), Khatib Mwadini anaeleza jinsi taasisi hiyo inavyoadhimisha siku ya chakula duniani mwaka huu.

Tueleze kuhusu siku ya chakula duniani na namna (ZBS) ilivyoji­panga kuiadhimisha kama Taasisi inayosimamia Ubora na Viwango vya bidhaa?

Siku ya chakula duniani inaad­himishwa kila mwaka ifikapo tarehe 16/10. Kwa upande wa Zan­zibar maadhimisho hayo kitaifa hufanyika katika eneo la Cha­manangwe liliopo Mkoa wa Kaska­zini Pemba.

ZBS ikiwa ni Mdau mkubwa kati­ka kuhakikisha usalama na Ubora wa bidhaa katika soko la Zanzi­bar itaendelea kushirikiki kamilifu katika maadhimisho hayo.

Maadhimisho hayo yanajumui­sha Maonyesho ya chakula kila mwaka ambapo ZBS itaendelea kutoa taaluma kwa wazalishaji na watumiaji juu ya umuhimu wa Viwango na Ubora wa bidhaa.

Viwango na Ubora wa bidhaa za chakula vina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa Uchumi na kulinda afya za walaji. Kwa namna gani ZBS mmefanikiwa katika kusimamia ubora wa bidhaa za chakula Zan­zibar?

ZBS imefanikiwa kuandaa viwango tofauti vya bidhaa za chakula na kilimo, pia kuanza kut­hibitisha baadhi ya bidhaa zinazo­zalishwa ndani na nje ya Zanzibar na kudhibiti bidhaa zote katika soko la Zanzibar. Bidhaa zilizot­hibitishwa na kutumia Alama ya Ubora ya ZBS hujiimarisha katika soko na hivyo kuongeza uzalishaji na kupelekea bidhaa hizo kupata imani kwa watumiaji.

Kwa muelekeo huo bidhaa zilizo­zalishwa hapa nchini na zile zinaz­otoka nje ya nchi hupata ushindani mzuri na hatimaye kuongeza tija pamoja na mapato ya Serikali.

Moja ya jukumu kubwa la ZBS ni kuhakikisha kwamba bidhaa zote zinazozalishwa au zinazotoka nje ya Zanzibar zinakuwa na viwango na ubora. Kwa namna gani mme­fanikiwa katika utekelezaji wa jukumu hili kwa upande wa bidhaa za chakula?

Ili kuhakikisha kwamba bidhaa za chakula zinakuwa na viwango pamoja na ubora, ZBS imeweza kuandaa Viwango 101 vya bidhaa za chakula na pia imeweza kuthibi­tisha bidhaa 19 za vyakula zinazo­zalishwa Zanzibar na nyingine nje ya Zanzibar.

Aidha ZBS imeweka mifumo miwili ya ukaguzi wa ubora wa bid­haa zinazoingizwa hapa Zanzibar. Mfumo wa kwanza ni ule unao­husisha ukaguzi wa bidhaa kwa kutumia mawakala waliopo nje ya nchi ambapo bidhaa hukaguliwa na kuthibitishwa ubora wake (PVOC). Mfumo wa pili unahusisha ukaguzi wa ubora wa bidhaa baada ya bid­haa kuingizwa hapa nchini kabla ya kusambazwa katika soko (DI).

Mafunzo na ushauri ni moja ya huduma zinazotolewa na Taasisi hii. Je, huduma hii imesaidia vipi kubadilisha mitazamo ya wafan­yabiashara na wakazi wa Zanzibar kuhusu ubora na viwango vya bid­haa?

Kwa kupitia mafunzo na ush­auri unaotolewa na ZBS, wazal­ishaji pamoja na wafanyabiashara kwa kiwango kikubwa wameweza kubadilisha mitazamo yao katika viwango na ubora wa bidhaa.

Ushahidi unaonekana kwa waza­lishaji wengi kuwasilisha maombi ya kutaka kuthibitishiwa ubora wa bidhaa zao ili waweze kutumia alama ya ubora ya ZBS.

Aidha waagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi wanaonyesha kuwa na muamko mkubwa na kuendelea kufanya ukaguzi wa ubora wa bid­haa kabla ya kusafirishwa na kuin­gizwa Zanzibar.

Je, ZBS inashirikiana vipi na wafan­yabiashara wa ndani na nje ya Zan­zibar katika kuhakikisha kwamba Wazanzibari wanakuwa salama kutokana na matumizi ya bidhaa za chakula?

ZBS inashirikiana na wafanyabi­ashara wa ndani na nje ya Zanzibar kwa kuwapa mafunzo na ushauri juu ya uzalishaji wa bidhaa zenye ubora pamoja na kuhakikisha waa­gizaji wa bidhaa wanaelewa juu ya umuhimu wa viwango na ubora wa bidhaa pamoja na kufahamu mad­hara kwa watumiaji na mazingira yanayotokana na bidhaa hafifu.

Dira ya ZBS ni kuwa Taasisi kubwa ya kusimamia viwango na ubora duniani. Mpaka sasa mmefikia wapi katika kufikia malengo ya dira hii?

Katika kufikia malengo ya Dira ya ZBS, ZBS kwa sasa imeshaandaa Viwango 101 na kuthibitisha bidhaa 19. Aidha ZBS imo katika maadalizi ya kuwa na Maabara itakayoweza kukidhi matakwa ya kitaifa, kikan­da na kimataifa katika kuthibitisha ubora wa bidhaa kabla ya kuwafikia watumiaji.

Ni mafanikio gani ambayo ZBS mnajivunia mpaka sasa katika kudhibiti ubora na viwango vya bidhaa za chakula Zanzibar?

ZBS inajivunia mafanikio ya kuandaa Viwango 101vinavyohusu bidhaa za chakula, kuthibitisha bid­haa 19 na kupewa leseni ya matu­mizi ya Alama ya Ubora ya ZBS.

Aidha ZBS imeweza kukagua Shehena 3514 za bidhaa ikiwemo bidhaa za chakula. Kuimarisha uwezo wa kiutendaji kwa wafan­yakazi wa ukaguzi na maabara za chakula pamoja na hatua za upa­tikanaji wa vifaa vya maabara ya chakula kwa ajili ya upimaji wa bid­haa hizo.

Lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya nchi kuwa ya Uchumi wa Viwanda. Kwa namna gani ZBS mnashiriki katika kuhakikisha azma hii inafanikiwa hususan kati­ka nyanja yenu ya kusimamia ubora na viwango vya bidhaa?

ZBS inahakikisha kwamba bidhaa ambazo hazina viwango zinaandaliwa ili kuenda sambam­ba na mahitaji ya wawekezaji wa viwanda wanaozalisha bidhaa za aina tofauti.

Kuendelea kudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini kuto­ka nje ili kuhakikisha bidhaa zin­azozalishwa hapa nchini zinapata ushindani halali.

ZBS ina mikakati gani kwa sasa katika kuhakikisha afya za Wazan­zibari zinakuwa salama?

ZBS inatoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kuifahamu bidhaa yenye ubora na hafifu kimatumizi. Aidha ZBS inaendelea na juhudi za kuimarisha miundombinu ya kimaabara pamoja na huduma za ukaguzi wa sokoni na bandarini ili kuhakikisha bidhaa zinazotumiwa ziko salama kwa mtumiaji na maz­ingira pamoja na kuimarisha uchu­mi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Mnatoa wito gani kwa wafanya­biashara na Wazanzibari katika maadhimisho haya ya siku ya usal­ama wa chakula duniani?

ZBS inaendelea kuwanasihi wafanyabiashara wanaoagiza bid­haa kutoka nje kuhakikisha bid­haa hizo zinakuwa na viwango na ubora unaotakiwa. Kufanya hivyo kutaendelea kuimarisha biashara pamoja na kumlinda mtumiaji.

Aidha ZBS inatoa wito kwa Wazanzibari wote kutambua umuhimu wa kutumia bidhaa zenye viwango na ubora ili kulinda usalama wa afya zao na mazingira ya nchi. Wazanzibari wanaombwa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake.