TFNC: Ni muhimu kuikumbusha jamii kuhusu lishe na chakula bora


 TFNC: Ni muhimu kuikumbusha jamii kuhusu lishe na chakula bora

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) ni mojawapo ya Taasisi ya umma inayotekeleza maju­kumu yake kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Lengo kuu la taasisi ni kud­hibiti na kutokomeza kabi­sa matatizo ya utapiamlo hapa nchini, kuhakikisha jamii inakula chakula sahihi na salama na jamii inaz­ingatia ulaji unaofaa. Taa­sisi ina majukumu ya msingi mbalimbali, miongoni mwa majukumu na wajibu wake katika jamii ni pamoja na

Chakula ni mojawapo ya mahitaji muhimu ya binad­amu ya kila siku kwa ajili ya maendeleo yake kimwili, kiafya, kiuchumi na jamii kwa ujumla.

Hata hivyo chakula kisi­poandaliwa kwa kuzinga­tia kanuni za usalama wa chakula wakati wa uzal­ishaji, uvunaji, usafirishaji, uhifadhi,uandaaji na utumi­aji, chakula kinaweza kuwa ni chanzo cha maambukizi ya magonjwa mbalimbali kwa mlaji ikiwemo magon­jwa ya kuhara kama vile; kip­indupindu, kuhara damu na homa ya matumbo.

Hivyo usalama wa chaku­la ni muhimu kuzingatiwa katika hatua zote muhimu za maandalizi na matumizi ya chakula kwa ajili ya kud­hibiti na kulinda madhara kwa mlaji na jamii.

Kila Juni 7, ulimwengu huadhimisha Siku ya Usal­ama wa Chakula ambapo kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inasema “Usalama wa Chakula ni wajibu wa kila mtu” (Food Safety, everyone’s busi­ness).

Kuelekea maadhimisho hayo, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) ambayo ndiyo wasimamizi wakuu wa masuala ya lishe na chakula hapa nchini wameandaa makala maalum yenye lengo la kutoa elimu kwa umma wa Watanzania kuhusiana na mitindo bora ya lishe na chakula.

Umuhimu wa usalama wa chakula

Hii ni kutokana na kuon­gezeka kwa vihatarishi kati­ka chakula. Vihatarishi ni kitu chochote kinachoweza kudhuru afya ya mlaji. Viha­tarishi hivyo ni pamoja na vile vya kibailojia ambavyo ni vimelea vya magonjwa (bakteria, virusi, minyoo na fangasi). Mfano ongezeko la vijidudu vya maradhi vina­vyosababisha magonjwa ya mlipuko yatokanayo na kula chakula kisichokidhi usalama mfano kipindupin­du, homa ya matumbo na kuhara damu.

Aidha kuwepo kwa sumu kuvu (aflatoxin) aina ya fangasi ambayo imeongeze­ka sana kwenye mazao mbalimbali mfano; mahin­di, karanga n.k ambayo inatishia maisha ya walaji pamoja na wanyama.

Sumu kuvu inapoku­wepo mwilini kwa kiwango kikubwa inaweza kusababi­sha magonjwa kama vile Saratani na hatimaye kifo. Pia baadhi ya tafiti zina­onesha kuwa sumu kuvu inapunguza kinga mwili na ukuaji wa watoto wadogo ambapo inachangia kwenye udumavu.

Pia kuwepo kwa sumu ya asili kwenye mazao mfano sianidi (cyanide) inayopati­kana kwenye mihogo hasa ile mihogo michungu. Mtu akitumia sumu ya aina hii huweza kumsababishia udu­mavu ujulikanao kama kon­zo (cyanide paralysis)

Aina nyingine ya vihatari­shi kwenye chakula ni kemi­kali ambazo ni pamoja na mabaki ya madawa ya kuua wadudu kwenye mazao ya chakula ( pesticides resi­dues)) dawa za kuhifadhi mazao ya chakula, madawa ya mifugo (Veterinary drug residues) dawa hizi kama hazikutumika kwa usahihi zinaweza kuingia kwenye mazao ya chakula, nyama, maziwa na kuleta madhara kwa watumiaji.

Kemikali nyingine zinato­kana na vitu vinavyoongez­wa kwenye chakula mfano rangi za chakula na vitu vya kuongeza ladha na harufu kwenye chakula. Kemikali hizi kama hazikutumika kwa usahihi zinaweza kusababi­sha madhara kwa mtumiaji hasa saratani.

Majukumu ya Taasisi katika kuhakikisha jamii ya Tan­zania inazingatia swala la usalama wa chakula

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) ni mojawapo ya Taasisi ya umma inayotekeleza maju­kumu yake kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Lengo kuu la taasisi ni kud­hibiti na kutokomeza kabi­sa matatizo ya utapiamlo hapa nchini, kuhakikisha jamii inakula chakula sahihi na salama na jamii inaz­ingatia ulaji unaofaa. Taa­sisi ina majukumu ya msingi mbalimbali, miongoni mwa majukumu na wajibu wake katika jamii ni pamoja na

• Kushirikiana na waza­lishaji, watengenezaji/ wasindikaji na wasam­bazaji wa chakula ili kuhakikisha kwamba chakula kinachouzwa nchini na kusafirishwa nje ya nchi ni bora na salama.

• Kuandaa miongozo ya Kitaifa inayoelezea swala zima la usala­ma wa chakula. Hii ni pamoja na Mwongozo wa kitaifa wa ulish­aji watoto wachanga na wadogo, likiwepo swala la usalama wa chakula.

• Kutoa elimu ya lishe inayolenga kuondoa tatizo la njaa kupitia vyombo vya habari na kuzingatia usalama wa chakula.

• Kuelimisha jamii kuhu­su njia bora ya kuandaa na kuhifadhi vyakula ili visipoteze virutubisho  muhimu, umuhimu wa jamii kutumia vyakula vilivyoongezwa viru­tubishi na kujihusisha na kilimo cha mazao lishe ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa vitamini na madini miongoni mwa jamii.

• Kufanya Tafiti mbalim­bali zinazohusiana na swala zima la ubora na usalama wa chakula.

• Kubuni na kusambaza teknolojia mbalimbali zinazolenga kuongeza ubora na usalama wa chakula.

Taasisi ya chakula na lishe inalo jukumu la kuhakikisha jamii inakula chakula bora na usalama wa chakula na lishe. Taasisi hii pia inahusi­ka pia katika utengenezaji wa sera na mikakati mbalim­bali inayohusiana na ubora na usalama wa chakula.

Uchunguzi mbalimbali wa sampuli za vyakula umeku­wa ukifanyika ili kuangalia ubora na usalama wa chaku­la. Sampuli mbalimbali kama vile sampuli za mahindi, mihogo zimekuwa zikifany­iwa uchunguzi wa kuangalia kiwango cha sumu kilichopo na kupendekeza njia sahihi za usindikaji ili kupunguza sumu hizo kufikikia kiwan­go kinachokubalika pasipo kusababisha madhara kwa mlaji.

Vile vile taasisi imekuwa ikitoa mafunzo na ushauri kwa jamii na wajasiriamali kuhusu njia bora za uanda­aji na usindikaji na uandaaji wa vyakula ili kupunguza matumizi ya vyakula vyenye masalia ya sumu. Mfano kwenye upande wa zao la mhogo Taasisi inatoa inae­neza teknolojia za usindikaji unga bora wa muhogo na hivi karibuni imetoa mafun­zo kwenye vikundi 65 (kila kikundi kina wanachama kati ya 15 - 20) vya wazal­ishaji wasindikaji wadogow­adogo, wajasilimali wadogo (SMEs) 25 katika wa mikoa ya ya Mtwara, Mara, Mwan­za, Pwani na Kagera, mikoa hii ambao ni wazalishaji wakubwa wa zao la muhogo.

Sambamba na hilo Taa­sisi imeshatoa mafunzo kwa maafisa ugani 100 kutoka katika halmashauri za mikoa hiyo. Mafunzo hayo yamesaidia wakulima na vikundi vya usindikaji kutumia teknolojia rahisi ya usindikaji na kulion­gezea thamani zao la muho­go ikiwa ni pamoja na na kupunguza kiasi cha sumu ya asili ya sianidi (cyanide) iliyopo kwenye mhogo ili ifikie kiwango kinachokuba­lika kwa mlaji. Pia vikundi vimepatiwa vitendea kazi na ushauri wa kitaalam ili kuliongezea zao hili tha­mani lilishe na kupata soko ndani na nje ya nchi.

Taasisi pia imeweza kujenga makaushio manne (4) ya kisasa yanayotumia teknologia ya jua (solar house dryers) katika wilaya ya Mtwara vijini (1), Newala (1), Kibiti (1) na Sengerema (1). Kaushio moja la kutumia umeme (flash dryers) lime­jengwa wilaya ya Ilemela na lina uwezo wa kuzalisha unga bora wa muhogo tani nne kwa siku. Pia kupitia maabara, taasisi imepewa jukumu la kufanya uchun­guzi wa vyakula kuangalia kama chakula kinafaa kwa matumizi ya binadamu hii ikiwa ni pamoja na kuanga­lia kama vyakula vimesham­buliwa na bakteria, virusi, minyoo au fangasi wanao­haribu vyakula na kuten­geneza sumu yenye kuleta madhara au magonjwa kwa binadamu.

Taasisi inatandaa mach­apisho mbalimbali yanahu­siana na swala la ubora na usalama wa chakula.

Sera ya chakula na lishe

Sera ya chakula na lishe iliundwa mwaka 1992, lengo la sera ni kuboresha ubora na usalama wa chakula na kuimarisha hali ya lishe kwa mtu mmoja mmoja, ngazi ya kaya na jamii kwa ujumla. Kauli ya sera ni kuhakikisha uratibu wa sekta zote katika mnyororo wa chakula ili kuboresha ubora na usalama wa chakula wenye matokeo chanya ya lishe, kuhakikisha ubora na usalama wa vyaku­la vya nyongeza kwa watoto wadogo na kukuza uelewa juu ya ubora na usalama wa chakula ili kuzuia magonjwa ya kuambukizwa yatokan­ayo na chakula katika hatua mbalimbali za mnyororo wa chakula.

Umuhimu wa siku ya usala­ma wa chakula duniani kwa Taasisi

Siku ya usalama wa chakula dunia ina umuhimu mkubwa kwa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) kwa kuwa inasaidia taa­sisi kuikumbusha jamiii mambo muhimu ya kuz­ingatia kuhakikisha chakula kinakuwa bora na salama ili kujikinga na mlipuko wa magonjwa yanayotokana na chakula kisicho salama.

Taasisi pia huadhimisha siku ya usalama wa chaku­la duniani kwa kuonesha teknolojia rahisi za maan­dalizi ya vyakula mbalimba­li mfano jinsi ya kusindika unga bora wa muhogo uto­kanao na muhogo mchungu, maandalizi ya vyakula vya nyongeza kwa watoto wa miezi 6-59, namna ya uon­gezaji viwango sahihi vya madini joto kwenye chumvi, vitamin A kwenye mafuta ya kula, virutubishi vya madini chuma, foliki ya aside, zinki na vitamini ya kundi la B12 ambavyo huongezwa kwe­nye unga wa ngano na unga wa mahindi. Siku hiyo pia hutumika kuelimisha jamiii jinsi ya kuzuia sumu kuvu katika vyakula mbalimbali hasa nafaka na jamii ya mikunde ili kuihakikishia jamii lishe bora na salama.

Namna wananchi wanavyo­shirikishwa katika Sera ya usalama wa chakula

Wananchi wanashirikish­wa kuhusu sera ya chakula na lishe kupitia mafunzo na elimu mbalimbali pamoja na maonyesho juu ya maan­dalizi salama ya vyakula mbalimbali.yanayohusiana na maswala ya chakula na lishe.

Mfano jamii imekuwa ikipewa elimu juu ya usin­dikaji bora wa vyakula, iki­wa ni pamoja na namna ya kupata unga bora wa muho­go ambao una viwango vina­vyokubalika kwa matumizi ya binadamu, ukaushaji bora na salama wa mboga za majani na matunda na kueneza teknolojia mbalim­bali za usindikaji. Elimu hii imekuwa ikitolewa kupitia nija mbalimbali kama vyom­bo ya habari, mafunzo kwa vikundi na wataalamu wa ugani, warsha na makonga­mano.

Jinsi Serikali ya Tanzania inavyotimiza majukumu yake ya kuhakikisha usala­ma wa chakula na lishe

Serikali ina jukumu la kuratibu masuala yote ya kitaifa ya lishe, ubora na usalama wa chakula kupi­tia taasisi zake. Serikali ina jukumu la kuhakikisha uwepo wa sera na mikakati bora ya usalama wa chakula na lishe. Pia, Serikali ina jukumu kujenga mazin­gira wezeshi ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli za usalama wa chakula na lishe bora ikiwemo uwezeshaji kifedha na rasilimali watu.

Ushirikiano baina ya TFNC na wakala wa Serikali kwe­nye usalama wa chakula

TFNC imekuwa ikishiriki­ana na wakala mbalimbali wa Serikali katika kuhakiki­sha ubora na usalama wa chakula. Taasisi inashiriki­ana na Wakala wa Chaku­la na Dawa (TFDA) katika kutengeneza miongozo ili kuhakikisha chakula kina­chosindikwa na kusamba­zwa ni bora na salama.

Taasisi pia inashirikiana na Shirika la Viwango Tan­zania (TBS) katika kuandaa viwango vinavyotumika wakati wa utengenezaji na usindikaji na usambazaji kuhakikisha chakula kina­choifikia jamii kina viwango bora na salama.

Taasisi inashirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika uandaaji wa miongozo inayolenga uza­lishaji bora na salama wa mazao ya chakula, mifugo na samaki.

Taasisi vile vile inashiriki­ana na Wizara ya Madini na Wizara ya Viwanda ili kuhakikisha kwamba kiwan­go cha madini joto kina­choongezwa kwenye chum­vi na virutubishi vingine vinavyoongezwa kwenye mafuta ya kula na unga wa ngano na mahindi ni sahihi na vina viwango vywa ubora na ni salama kwa afya ya mlaji.

Wakati wa kutengeneza Sera, kanuni na Miongozo mbalimbali Taasisi (TFNC) imekuwa ikishirikiana hasa na Wizara zifuatazo: Wiz­ara ya maji na umwagiliaji, Mifugo na Uvuvi, Madini, Kilimo, Viwanda na Biasha­ra, Elimu na TAMISEMI. Pia imekuwa ikishirikiana na vyuo mbalimbali vya uta­fiti kama vile SUA, UDSM, MUHAS, Chuo kikuu cha Mandela, Vyuo vya utafiti wa Kilimo (ARIs) na vyuo vinginevyo vya ndani na nje ya nchi.

Ushirikiano na taasisi za kimataifa

Katika kutekeleza majuku­mu yake kwa kufikia ufanisi na kufanikisha malengo yake, Taasisi imekuwa inashirikiana na Taasisi na Asasi mbalimbali za kima­taifa nkama vile UNICEF, WFP, FAO, WHO, NI, GAIN n.k. Taasisi hizo zimekuwa zikitoa msaada wa kifedha na kitaalam.