Chakula salama, chenye viini lishe bora ni muhimu katika kukuza afya njema


Chakula salama, chenye viini lishe bora ni muhimu katika kukuza afya njema

Chakula kisichokuwa salama ni chanzo cha afya duni, magonjwa na vifo duniani kote. Kinasababisha magonjwa kuanzia kuharisha mpaka saratani. Inakadiriwa watu laki sita – karibu mtu mmoja kati ya watu 10 duniani anaugua baada ya kula chakula kichafu na watu 420 000 hufariki kila mwaka.

Kauli mbiu ya Siku ya Usalama wa Chakula Duniani ni “Usalama wa Chakula, Jukumu la Kila Mmoja” inatutaka tut­ambue kuwa suala la usalama wa chakula ni jukumu la kila mmoja wetu. Upatikanaji wa chakula cha kutosha na chenye virutubisho vyote muhimu ni muhimu kwa maisha na afya njema. Kila mmoja ana haki ya kupata chakula salama, chenye lishe bora na cha kutosha.

Chakula kisichokuwa salama ni chanzo cha afya duni, magonjwa na vifo duniani kote. Kinasababisha magonjwa kuanzia kuharisha mpaka saratani. Inakadiriwa watu laki sita – karibu mtu mmoja kati ya watu 10 duniani anaugua baada ya kula chakula kichafu na watu 420 000 hufariki kila mwaka.

Watoto chini ya miaka mitano ndio wanaoathirika na magonjwa yatokanayo na magonjwa yanayohusiana na chakula kwa asilimia arobaini, huku 125 000 wakifa kila mwaka. Magon­jwa ya kuharisha ndio mengi zaidi kutokana na kula vyakula vilivyochafuka, ikisababisha watu milioni 550 kuugua na 230 000 kufariki kila mwaka.

Usalama wa chakula ni muhimu katika kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na Siku ya Usalama wa Chakula inalilta hili kwa ajili ya kutafakari, ili kusaidia kuzuia, kutambua na kudhibiti hatari zinayosambazwa kutokana na vyakula. Chaku­la salama kinachangia kwenye kunawiri kwa uchumi, kubore­sha kilimo, ufikiwaji wa masoko, utalii na maendeleo endelevu.

Chakula kinaweza kuchafuka katika hatua yoyote ya uzalish­aji na usambazaji, na jukumu la msingi lipo kwa wazalishaji wa chakula. Lakini pia sehemu kubwa ya magonjwa husababishwa na uandaaji wa chakula usio mzuri majumbani, katika maeneo ya huduma ya kuuza vyakula na hata katika masoko. Sio wabe­baji wote wa chakula au walaji wanaojua majukumu wanayo­takiwa kutekeleza, kama vile kuwa na tabia zinazoheshimu usafi kuanzia kwenye manunuzi, uuzaji na uandaaji wa chakula ili kulinda afya zao na zile za jamii pana inayowazunguka. Kila mmoja anaweza kuchangia kufanya chakula kile salama.

Kuhakikisha chakula kipo salama, kila mmoja analo jukumu. Watunga sera wanaweza kujenga na kuweka mifumo ya chaku­la na miundombinu kama vile maabara ili kuitikia na kudhibiti vitisho vyovyote dhidi ya usalama wa chakula katika mnyororo mzima wa chakula ikijumuisha wakati wa dharura.

Wanaweza kuhakmasisha ushiriki wa sekta mtambuka kwa ajili ya mawasiliano mazuri na hatua za pamoja na kujumuisha usalama wa chakula katika mawanda mapana ya sera na pro­gramu za lishe na uhakika wa chakula.

Kwa upande mwingine, wanunuzi na walaji wa chakula wanaweza kukijua chakula wanachotumia (wasome nembo kwenye vifungashio, kufanya maamuzi sahihi, kujua athari zozote zinazoweza kutokea); na kuandaa chakula kwa usalama na kulima matunda na mboga mboga kwa kutumia Mwongozo wa Vigezo Vitano wa WHO kuhusu Kilimo Salama cha Matunda na Mboga Mboga ili kupunguza uwepo wa vijuasumu kwenye chakula. (Tizama mchoro hapo chini).

WHO inalenga kufanikisha kuzuia, kugundua na kukabi­li hatari zozote zinazohusiana na chakula kisicho salama. Kuhakikisha kuwa walaji wanaziamini mamlaka zao, na kuami­ni kwenye mifumo salama ya usambazaji wa chakula, yote haya ni miongoni mwa malengo ambayo WHO inalenga kuyatimiza.

Ili kufanya hivyo, WHO inasaidia nchi wanachama kujenga uwezo wa kuzuia, kutambua na kudhibiti hatari zihusianazo na chakula kwa kutoa tathmini huru za kisayansi kuhusu hatari za vimelea vya magonjwa na kemikali zinazoweka msingi wa viwango vya kimataifa vya chakula, miongozo na mapendekezo zinazojulikana kama Codex Alimentarius kuhakikisha kuwa chakula ni salama popote kinapotokea.

WHO pia inasaidia nchi wanachama katika kutathmini usalama wa teknolojia mpya zinazotumika katika uzalishaji chakula, kama vile uboreshaji wa vinasaba ambazo zinatumika katika kuboresha mifumo ya uzalishaji chakula na sharia, na kuwekwa kwa miundombinu ya kutosha kudhibiti hatari zin­azohusiana na masuala ya usalama wa chakula.

Kutokana na hilo, Mamlaka ya Mtandao wa Usalama wa Chakula (INFOSAN) ilianzishwa na WHO and the UN Food na FAO ili kutoa taarifa kwa haraka wakati wa dharura zinazohu­siana na masuala ya usalama wa chakula.

Mbali na hayo, WHO inasaidia nchi wanachama kuhama­sisha juu ya usalama wa chakula na utunzwaji wake kupitia mfumo wa kuzuia magonjwa na programu za kukuza uelewa, kupitia Miongozo Mitano kwa Ajili ya Chakula Salama na nyaraka nyingine za mafunzo; na kuhamasisha juu ya usalama wa chakula kama sehemu muihimu ya uhakika wa afya njema na kujumuisha suala la chakula salama katika sera za taifa na programu kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Kimataifa za Afya (IHR - 2005).

WHO inafanya kazi kwa karibu na FAO, Shirika la Afya za Wanyama Duniani (OIE) na taasisi nyingine za kimataifa kuhakikisha usalama wa chakula katika mnyororo mzima wa chakula kutoka kwenye uzalishaji hadi ulaji.

Leo, WHO inajiunga na Umoja wa Mataifa na nchi wana­chama katika kukuza uelewa wa Siku ya Dunia ya Usalama wa Chakula chini ya ujumbe wake - “Usalama wa Chakula, Jukumu la Kila Mmoja”. Ujumbe huu unasisitiza juu ya umuhimu wa nguvu za pamoja kwa ajili ya jamii inayojitahidi kuboresha suala la usalama wa chakula.

Umoja wa Mataifa unaamini kuwa kuboresha usalama wa chakula unachangia kwenye Biashara, ajira na utokomezaji wa umaskini.

Makala hii imeandikwa na Mwakilishi wa WHO hapa nchini Tanzania.