Tanzania imepiga hatua katika kuendeleza hifadhi na maeneo tengefu ya bahari


Tanzania imepiga hatua katika kuendeleza hifadhi na maeneo tengefu ya bahari

Mara nyingi watu wanaposikia neno hifadhi mawazo yao moja kwa moja hukimbilia kwenye hifadhi za taifa zilizopo nchi kavu kama vile Mbuga za Wanyama za Serengeti, Ngorongoro, Mikumi na nyinginezo, lakini ni nadra mno kusikia watu wakitaja hifadhi zinazopatikana katika bahari.

Wakati hali ikionyesha hifadhi za bahari kutokuwepo akilini na midomoni mwa watu wengi, Tanzania inajulikana kuwa miongoni mwa mataifa duniani ambayo yamejizolea sifa kubwa katika kusimamia vizuri hifadhi za bahari.
Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu ni nini?

Kwa mujibu wa Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dkt. Adilian Chande, kitengo hicho kilikuwa chini ya Idara ya Uvuvi, kwa mujibu wa sheria ya Maeneo Tengefu ya Bahari Na. 29 ya mwaka 1994.

Kutokana na kwamba kwa sasa Sekta ya Uvuvi imegawanyika katika idara mbili; Ufugaji wa Samaki na Maendeleo ya Uvuvi, kitengo sasa kipo chini ya Idara ya Maendeleo ya Uvuvi.

"Hivyo sheria iliyounda kitengo kwa sasa ipo redundant (imepitwa na wakati), kwani idara ya Maendeleo ya Uvuvi haijatajwa kwenye sheria ya wakati huo na sasa tupo katika mchakato wa kurekebisha sheria," alisema Dkt. Chande.
Akizungumza mwaka jana wakati wa kupokea ujumbe wa watendaji wa Mradi wa Kuhifadhi Mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP) uliokuwa kwenye ziara ya kujifunza kutoka kwenye miradi inayotekelezwa kuhifadhi mazingira ya Ukanda wa Pwani na hasa Mradi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingira ya Ukanda wa Pwani (TCMP) unaofadhiliwa na USAID, Dkt. Chande alisema kitengo kilianzishwa baada ya idara kugundua kuwa kulikuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira hasa katika maeneo yenye bayoanuai kubwa na viumbe ambao ni adimu baharini kama vile nguva, pomboo, kasa, papa na wengine ikiwa ni pamoja na uoto wa asili ambapo mikoko ilikatwa ovyo na matumbawe kuharibiwa kwa kupigwa mabomu.
"Matumbawe yalivunjwa ovyo ovyo kwa kutumia mabomu, shida kubwa ni mabomu ambayo yanaangamiza matumbawe ambayo ndiyo uhai wa bahari, hakuna bahari bila matumbawe, hakuna uhai kabisa," alisema Dkt. Chande.
Ndipo idara ikaona kuna haja ya kuanzisha kitengo kuweza kubainisha maeneo husika ili yaweze kuhifadhiwa kwa njia mbili, Hifadhi za Bahari au Maeneo Tengefu.
Kwa kutofautisha, Hifadhi ya Bahari ni eneo kubwa ambalo hata watu wanaishi ndani yake. Shughuli za eneo hilo husimamiwa na Mpango wa Usimamiaji ujulikanao kama General Management Plan, ambao kwa mujibu wa Dkt. Chande, maandalizi yake yanashirikisha wadau wote.
Mpango unashirikisha wanajamii ambao wanaishi ndani ya hifadhi, Halmashauri husika ambazo ziko ndani ya hifadhi, na wadau wengine ikiwa ni pamoja na wanasayansi kwa kushirikiana na uongozi wa kitengo kukubaliana kuwa baadhi ya maeneo yatengwe kabisa ambapo hakuna uvuvi wowote utakaoruhusiwa, kutenga maeneo ya matumizi ya jumla ambapo uvuvi unaruhusiwa kwa wavuvi wa ndani na nje ya hifadhi na maeneo ya matumizi maalum ambayo pamoja na kwamba wavuvi wa ndani ya hifadhi wanaruhusiwa kuvua kwa kutumia zana maalum zinazoruhusiwa kisheria, wavuvi wa nje hawaruhusiwi kabisa kuvua katika maeneo hayo.
Kwa upande mwingine, maeneo tengefu ni maeneo madogo madogo ya visiwa ambayo yanazungukwa na matumbawe. Katika maeneo haya watu hawaruhusiwi kuishi wala matumizi ya rasilimali hayaruhusiwi. Shughuli zinazoruhusiwa katika maeneo hayo ni zile zinazohusiana na utalii tu. Kwa mujibu wa Dkt. Chande, maeneo hayo ni pamoja na visiwa vya Bongoyo na Mbudya mjini Dar es Salaam ambapo ndani yake kitengo kimetengeneza njia vinjari (nature trails) kwa ajili ya watalii kupita.
Je, Unazijua Hifadhi za Bahari Tanzania?
Kwa mujibu wa Dkt. Chande, ni mpango wa dunia nzima kuwa asilimia 10 ya maji ya bahari na maziwa yanakuwa chini ya hifadhi, na Tanzania ina asilimia 4.5 tu ya hifadhi. Alisema kama kitengo chake kitaingia katika kuanzisha hifadhi kwenye maji ya ziwa, anatarajia asilimia hiyo itaongezeka hadi 7 na hivyo nchi kupiga hatua kubwa.
Asilimia hiyo 4.5 inahusisha hifadhi za bahari 3 na maeneo tengefu 15. "Tuna Hifadhi za Bahari 3 nchini Tanzania," alisema Dkt. Chande.
Akizitaja kwa majina, alisema hifadhi ya kwanza ni ile ya kisiwa cha Mafia katika Mkoa wa Pwani ambayo ilianzishwa kati ya mwaka 1995/96. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilomita za mraba 822.
"Katika hifadhi hii huwezi kusikia bomu linalia kwani tumeshadhibiti hali na wananchi wengi wameshakuwa na uelewa na hivyo kusaidia katika kazi za uhifadhi," alisema na kuongeza kuwa pia wananchi wanafaidika kutokana na kuongezeka kwa utalii katika eneo hilo.
"Kuna geti la kuingilia kwenye hifadhi na kiingilio ni dola 20. Kila mwaka wanakijiji wanapata asilimia 20 na halmashauri asilimia 10 ya mapato yatokanayo na utalii," alibainisha na kuongeza kuwa kila mwaka wanakijiji wanaandaa mpango wao wa shughuli za maendeleo ambao unapitishwa na halmashauri husika. Mpango huo unabainisha vijiji vya kufaidika na fedha za hifadhi mwaka hadi mwaka na unaweza kuhusisha shughuli za uchimbaji visima, kujenga zahanati, madarasa na shughuli nyingine.
Pia, kitengo hicho kinasomesha baadhi ya watoto wa wanajamii katika hifadhi katika kiwango cha elimu ya sekondari ili kuhamasisha jamii hizo kupenda kupeleka watoto wao shule.
"Kwa hiyo wameona faida ya hifadhi, ila hapo kabla walikuwa hawajaelewa," alisema Dkt. Chande. "Wameona umuhimu wa kutunza hizi rasilimali. Hakuna mwananchi wa Mafia ndani ya hifadhi ambaye sasa anapenda kusikia bomu."
Hata hivyo, kwa mujibu wa Dkt. Chande, kuna aina ya uvuvi wa kutumia nyavu za mitando ambazo haziruhusiwi kutokana na kuwa na macho madogo. Uvuvi huu bado unatumika katika vijiji viwili kwenye hifadhi ya Mafia. Lakini, alisema kitengo chake kinafanya jitihada za kudhibiti uvuvi huo. Hifadhi ya pili ni ya Mnazi Bay ambayo imeanzishwa mwaka 2000. Hifadhi hii inahusisha eneo lenye gesi la Mnazi Bay na ina ukubwa wa kilomita za mraba 650. Hapa uvuvi haramu ni mkubwa kutokana na kuwepo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika mkoa wa Mtwara.
"Doria imekuwa ngumu kutokana na kuwa wavuvi haramu wanapofukuzwa upande mmoja wa nchi wanakimbilia upande mwingine," alisema Dkt. Chande, akiongeza kuwa hata hivyo hali imeweza kudhibitiwa baada ya kuongeza nguvu ya doria katika hifadhi hiyo.
"Kwa sasa hali imekuwa nzuri, ilibidi usimamiaji wa sheria uwe mkali zaidi ili kupunguza upigaji wa baruti na wavuvi haramu wamepungua kwa kiasi kikubwa," kwa mujibu wa Dkt. Chande.
Alisema, “Hata hivyo, bado kuna vijiji viwili ambavyo vinasumbua katika kuendesha uvuvi haramu kwenye hifadhi hiyo.Lakini wamekuja wenyewe na kujisalimisha kwa Mkuu wa Wilaya na kula kiapo mbele ya mwanasheria mkuu wa Serikali wakiahidi kuwa hawatarudia tena vitendo vyao vya uvuvi haramu, pia tumewaanzishia vikundi vyao vya doria ili wao wenyewe washiriki katika kusimamia hifadhi."
Akifafanua zaidi juu ya hifadhi hiyo, Dkt. Chande alisema ina rasilimali nyingi na vivutio viko vingi ikiwa ni pamoja na msitu mkubwa wa mikoko ambao usingekuwa katika maji hata wanyama wakubwa wangeweza kuishi humo. Pia kuna maingilio ya Mto Ruvuma ambayo yana viboko wengi na kuanzia mwezi wa nane kuna mapitio ya nyangumi. Watu wanavutiwa kuangalia nyangumi wakipita. Na ili kukuza utalii wa kuangalia nyangumi, ofisi ya hifadhi sasa imejengwa katika mapitio ya nyangumi. Ni kivutio kikubwa.
Pia kuna viota vya kasa ambavyo vinavutia watalii wengi wakati wa kuanguliwa kwa kasa na kuna vivutio vya matumbawe.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Dkt. Chande utalii wa eneo hilo unakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa miundombinu.

"Vivutio viko vingi, lakini utalii bado haujakua kutokana na kukosekana kwa miundombinu. Barabara yetu ya Kibiti hadi Lindi haijaisha, hata usafiri wa kutoka (Mtwara) mjini kwenda eneo tulilojenga ofisi kilomita 45 ni barabara mbaya ambayo inahitaji uwekezaji," alielezea Dkt. Chande.
Hata hivyo, kuna watalii ambao wanapita vikwazo hivyo vyote kutokana na kupenda kufikia vivutio adimu vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.
Hifadhi ya tatu ni ile ya Tanga Coelacanth ambayo ilianzishwa mwaka 2009 ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 552. Ilianzishwa kwa shinikizo la Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na umuhimu wake wa kuwepo kwa samaki adimu duniani aina ya silikanti (Coelacanth). Pia ni kutokana na wananchi wenyewe wa Tanga ambao tayari wamehamasika kutunza mazingira na hivyo kuwasukuma kufika kwenye kitengo kuomba kuanzishwa kwa hifadhi.
Mbali na samaki aina ya silikanti, vivutio vingine vinavyopatikana katika hifadhi ya Tanga ni pamoja na matumbawe, kasa na ni eneo lenye samaki wengi.
"Kuanzia mwaka 2009 mpaka sasa hivi wananchi wenyewe wameanza kushuhudia kuwa samaki wameongezeka kwa kiasi kikubwa," alisema Dkt. Chande.

Maeneo tengefu
Kuna maeneo tengefu 15 nchini Tanzania huku Dar es Salaam pekee ikiwa na maeneo tengefu 7 ambayo yanapatikana upande wa Kaskazini na Kusini. Kwa upande wa Kaskazini kuna kisiwa cha Bongoyo, Mbudya na eneo tengefu la fungu la mchanga lijulikanalo kama Fungu Yasin na Pangamin.

Maeneo haya tengefu yalianzishwa kabla ya kitengo hakijaanza mwaka 1975 wakati Idara ya Uvuvi ilipokuwa inaanza. Maeneo hayo yalipitishwa kwa kutumia sheria ya Idara ya Uvuvi. Visiwa vya Kusini ni pamoja na kisiwa cha Finda, Kenda na Makatobe ambavyo vimeanzishwa na Kitengo cha Hifadhi za Bahari.

Ukiacha Hifadhi ya Bahari, Mafia pia ina maeneo tengefu katika visiwa vya Shungimbili, Nyororo na Mbarakuni.

Kwa upande wa Tanga, kuna kisiwa cha Maziwe katika Wilaya ya Pangani. Hiki kilipitishwa mwaka 1975 kuwa eneo tengefu ambapo wakati huo kilikuwa ni kisiwa. Lakini sasa kutokana na uharibifu wa mazingira, kimegeuka na kuwa fungu la mchanga. Kisiwa hiki kina mazalia makubwa ya kasa ambapo kuna utalii mkubwa unaoendelea wa kushuhudia jinsi kasa wanavyoanguliwa katika fukwe za Ushongo na Kikokwe.
Maeneo mengine tengefu yanaanzia Tanga mjini kwenda mpakani mwa Kenya. Maeneo hayo ni pamoja na Mwewe, Kilui, Ulenge na Kwale. Kisiwa cha Kilui kiko mpakani kabisa mwa Kenya. Hali hii imesababisha kitengo kuona haja ya kuanzisha usimamiaji wa pamoja wa maeneo tengefu na nchi za jirani. Hii itasaidia kudhibiti uvuvi haramu na kuhifadhi viumbe wanaohama kama vile kasa.
Tofauti ya Hifadhi za Bahari na Hifadhi za Taifa
Kuna tofauti kati ya Hifadhi za Bahari na Hifadhi za Taifa zilizopo chini ya Mamlaka ya Kusimamia Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Wakati hifadhi zinazosimamiwa na TANAPA haziruhusu wanajamii kuishi katika hifadhi za taifa, kitengo cha kusimamia hifadhi za bahari kinaruhusu wanajamii kuishi ndani ya hifadhi.
Kwa mujibu wa Dkt. Chande, mpangilio huu unafanya kazi ya kuwashirikisha wanajamii katika uhifadhi kuwa rahisi zaidi.

Mafanikio ya hifadhi na maeneo tengefu ya bahari
Moja ya mafanikio ni kuongezeka kwa akiba ya samaki baharini na kuhifadhiwa kwa rasilimali na viumbe bahari walio katika hatari ya kutoweka kama vile mikoko, matumbawe, kasa, nguva, silikanti n.k.
“Pia kuna ongezeko la utalii katika maeneo ya hifadhi, tunajaribu kuhamasisha utalii," alisema Dkt. Chande.

Eneo la bahari, ambalo kimsingi linaaminika lingetowa mchango mkubwa katika uimarishaji wa uchumi wa Taifa, limebaki na matumizi duni, hususan yale ya uvuvi wa kiwango cha chini yanayohusisha uvuvi wa vyombo, vifaa na teknolojia dhaifu, hivyo kushindwa kuleta tija yenye kukidhi haja.

Aidha, mbali na kuwepo mpango wa uanzishaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa Bandari kubwa ya kisasa katika eneo la Mpigaduri, kwa kipindi kirefu Zanzibar imebaki na bandari ndogo isiyoendana na wakati uliopo.

Kwa hakika hali hiyo inasabisha bandari hiyo kushindwa kukidhi mahitaji yaliyopo sambamba na kuhimili ushindani na bandari nyingine za Ukanda wa Afrika Mashariki.

Kuwepo kwa bandari za Mombasa na Dar es Salaam zinazohodhi eneo kubwa pamoja na vifaa mbalimbali vya kisasa, kumezifanya kuwa njia kuu ya kibiashara kati yake na mataifa ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika.

Lakini ‘penye ni pana njia’, juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Uongozi wa Rais, Dkt. Ali Mohamed Shein ni biashara njema inayoonyesha muelekeo wa kuimarika kwa uchumi wa Zanzibar baada ya ujenzi wa Bandari hiyo kukamilika.

Pamoja na shughuli za kibiashara za uingizaji na utoaji wa bidhaa kutoka mataifa mbalimbali duniani, Zanzibar bado inabaki kuwa na fursa pana ya mafanikio katika matumizi ya bandari hiyo.

Shirika Ia International Maritime Organization (IMO) limebainisha kuwa asilimia 90 ya mizigo mizito duniani, husafirishwa kwa kutumia usafiri wa baharini, yaani njia ya meli.

Hivyo ni dhahiri kuwa bandari hiyo itakuwa kimbilio la makampuni na mataifa mbalimbali duniani katika usafirishaji wa mizigo yake.

Fursa nyingine inayoonekana kuimurikia Zanzibar, ni ile ya vijana wake kupata nafasi za ajira katika meli mbalimbali zitakazokuwa zikitumia bandari hiyo.

Kwa mantiki hiyo juhudi za makusudi zinahitajika kuchukuliwa na Serikali za kuharakisha ujenzi wa bandari ya Mpigaduri, sambamba na kufanikisha azma ya ujenzi wa Chuo cha Mabaharia hapa Zanzibar.

"Pamoja na kuwa lengo letu la msingi ni kuhifadhi mazingira, lakini baada ya kuhifadhi, mahitaji ya uwekezaji katika utalii yanazidi kuongezeka."
Changamoto za kuendeleza Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu
Changamoto kubwa ya kusimamia Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu ni ulipuaji wa mabomu kutokana na kuongezeka kwa samaki katika maeneo hayo.
"Tunapata shida sana na uvuvi haramu katika maeneo hayo, baada ya kuyatunza samaki wamekuwa wengi wengi sana, kwa hiyo wahalifu wakilipua bomu na samaki kuelea wanachota samaki wengi. Kazi kubwa ni kusukuma utekelezaji wa sheria kwa kufanya doria za mara kwa mara ambazo ni za gharama kubwa. Hii kwa kiasi kikubwa imepunguza uvuvi haramu," alisema Dkt. Chande.

Jinsi Serikali zinavyoimalisha uchumi wa bahari

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuimarisha sekta ya bahari ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali zilizopo nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Dkt. Makame Ali Ussi akizungumza katika mafunzo ya siku tatu kwa wafugaji wa samaki na watendaji wa sekta za mazao ya bahari juu ya ufugaji wa mazao ya baharini katika ukumbi wa kituo cha kuzalishia vifaranga vya mazao ya bahari Bet al ras Bububu Wilaya ya Magharib A Unguja alisema Serikali inatambua umuhimu wa rasilimali za bahari ambazo zinachangia kutengeza mapato ya nchi pamoja na kuwawezesha wananchi kujikwamua na umaskini.

Alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea na jitihada mbalimbali katika kutatua matatizo yanayowakabili wavuvi na wafugaji wa mazao ya bahari ikiwemo Majongoo, Samaki na Kaa.

Dkt.Makame alisema wakati umefika kwa sekta ya bahari kuendelea kuwa mhimili mkuu utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na kuwawezesha wananchi kuwa na uhakika wa chakula.

Alisema takwimu za uzalishaji wa mazao ya baharini zinaonyesha kuwa takribani asilimia 40 inawawezesha wananchi kunufaika na ajira ambapo asilimia 70 ya wananchi wanategemea sekta hiyo katika kujikwamua na umaskini jambo linalochangia ukuaji wa maendeleo nchini.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mifugo na Uvuvi, Dkt.Islam Seif alisema ili kuhakikisha wavuvi na wafugaji wanafikia malengo waliyoyakusudia Wizara itaendelea kushirikiana na wataalamu katika kutatua matatizo yanayojitokeza katika sekta hiyo.

Alisema mpaka sasa muitikio kwa wafugaji umekuwa mkubwa ambapo hadi kufikia wavuvi 49 elfu kutoka 35 elfu jambo ambalo linachangia maendeleo ya uchumi nchini.

Alitowa wito kwa wavuvi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wa maendeleo katika kuleta maendeleo pamoja na kuwa na matumizi mazuri rasilimali za bahari ili ziweze kuwanufaisha wananchi.

Mratibu wa kituo cha kuzalisha vifaranga vya Samaki Bet al ras, Buriani Mussa alisema ni vyema kwa wananchi hususan vijana kuchangamkia fursa zilizopo za kujikita na ufugaji wa mazao ya baharini ili waweze kujingizia kipato cha uhakika.

Alisema si vyema kwa vijana kushindwa kushiriki katika miradi inayoanzishwa badala yake watafute njia mbadala za kuweza kujiajiri na kuachana na mawazo ya kusubiri ajira kutoka serikalini.

Washiriki wa mafunzo hayo, Naima Ibrahim na Semen Muhammed wenyewe waliomba kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kuzalisha mazao ya bahari yanayoendana na mahitaji ndani na nje ya nchi.

Walisema mbali na mafunzo pia ni vyema kwa wasimamizi wa kituo cha kuzalisha vifaranga vya mazao ya bahari kufanya kazi kwa uhakika ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia ikiwemo kuondoa tatizo la upatikanaji wa vifaranga kwa wafugaji.

Mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku tatu kwa lengo la kuwafunza wafugaji na wasimamizi wa mazao ya baharini namna bora ya kuimarisha ufugaji wa mazao hayo yaliwakutanisha pamoja wafugaji,  wataalamu wa masuala ya bahari na watendaji wa Wizara ya Kilimo chini ya ufadhili wa FAO na KOICA pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Taarifa sahihi za viwango vya samaki tulionao zinaweza kuchochea ujenzi wa viwanda

Meli ya kisasa ya utafiti wa samaki na mazingira bahari ya Dkt. Fridtjof Nansen imekamilisha uchunguzi wake wa rasilimali na mazingira bahari katika maji ya Bahari ya Hindi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni meli ya tatu kubeba jina hili katika miaka 40 ya ushirikiano wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na nchi ya Norway. Ikiwa na maabara saba tofauti zenye vifaa vya kisasa kabisa, meli hii ya Dkt. Fridtjof Nansen ni chombo pekee cha majini chenye kupeperusha bendera ya Umoja wa Mataifa.  

Chombo hiki kinaendesha tafiti kwenye nchi mbalimbali lengo likiwa kukusanya taarifa kuhusu mtawanyiko na uwingi wa samaki, bionuwai, hali za mazingira, na shughuli nyingine nyingi kwa kutumia teknolojia na vifaa vya kisasa kabisa kusaidia nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kukusanya taarifa za kisayansi muhimu kwa ajili ya uvuvi endelevu na kujua namna mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri bahari zao. 

Chini ya Mpango wa Programu ya EAF-Nansen inayofadhiliwa na Norway na kutekelezwa na FAO kwa kushirkiana na Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Bahari ya Norway (IMR) meli hii inaendesha utafiti wake wa rasilimali bahari na mazingira baharini katika Ukanda wa Kusini Mashariki mwa Afrika na Bahari ya Hindi. Chini ya Programu hii, nchi thelathini (30) za Kiafrika ikiwemo Tanzania zitapata msaada wa kitaalam na kisayansi wa namna ya udhibiti wa rasilimali zao za samaki na viumbe bahari wengine kutumia na kutekeleza mpango endelevu wa utunzaji wa mazingira.

Akizungumza katika hafla fupi ya kilele cha utafiti huo katika pwani ya Tanzania iliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam ndani ya meli ya Dkt. Fridtjof Nansen, Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Mhandisi John William Kijazi alisema utafiti huo umekuja kwa wakati muafaka kwani ilikuwa inaenda kuongeza kasi ya uanzishwaji wa viwanda hapa nchini hususan katika sekta ya uvuvi. Alikuwa anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika hafla hiyo.

“Hii ni hatua kubwa sana kwa Tanzania ambayo itafaidika na huduma za utafiti wa kisasa wa meli hii kupitia ushirikiano wa wadau hapa nikizungumzia FAO na Serikali ya Norway, kuweza kujua kwa uhakika aina na kiwango cha samaki na rasilimali bahari nyingine tulizonazo katika maji yetu,” alisema na kuongeza: “Taarifa kuhusu rasilimali bahari zetu zitakuwa muhimu sana katika kufanya maamuzi na kupata fursa za ndani na kimataifa za uwekezaji katika sekta ya uvuvi huku tukitilia maanani mambo muhimu ya utunzaji wa mazingira. Kwa kutumia taarifa sahihi tunaweza kuwavutia wawekezaji waje na kujenga viwanda vya kusindika samaki na vingine vinavyohusiana na sekta hii ya uvuvi na hivyo kuongeza kasi kwenye mpango wetu wa kujenga Tanzania ya viwanda.”

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh.Luhaga Joelson Mpina alisema kuwa ni matumaini ya Serikali kwamba takwimu zitakazotokana na utafiti huo zitaisaidia Tanzania kujua kwa uhakika juu ya aina na kiwango cha samaki na rasilimali bahari nyingine katika eneo letu la Bahari ya Hindi.

“Hii itatuwezesha kupata wawekezaji katika eneo hili ambao watajenga viwanda vya kuchakata na kusindika mazao ya samaki ambapo mbali ya kutoa fursa za ajira kwa watu wetu hususan vijana katika mnyororo wa thamani, lakini pia utakuza mapato ya serikali,” alisema.  

Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania, Fred Kafeero alisema kuwa ushirikiano na Serikali ya Norway katika kutekeleza Programu ya Nansen ni wa umuhimu wa kipekee kwa FAO.

“Mbali ya taarifa ambazo zitawezesha udhibiti bora wa rasilimali kwa matumizi endelevu, utafiti huu utapelekea uelewa mzuri wa athari za mabadiliko ya tabia nchi na athari nyingine za nje, kama vile uchafuzi wa mazingira na mifumo ya uhai baharini,” alisema.

Kwa upande wake, Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad, alisema: “Ni matumaini yetu kuwa meli ya Nansen itachangia siyo tu katika kuhakikisha kuwa takwimu za uhakiki za kisayansi zinapatikana, lakini pia kuimarisha uwezo katika matumizi ya takwimu hizo ili kujenga mikakati bora ya udhibiti na matumizi ya rasilimali bahari.

Bahari zina utajiri mkubwa kuanzia ufugaji wa samaki, uvuvi na pia uchakataji na usindikaji wa mazao ya samaki. Sera zenye kutilia maanani taarifa hizi ni muhimu katika kujenga msingi kwa ajili ya viwanda vipya kama vile uchimbaji wa madini katika sakafu ya bahari na kilimo pamoja na uvunaji wa mwani na viumbe vingine, na hivyo kuchangia katika juhudi za maendeleo kwa Tanzania.”

Hafla hii iliandaliwa kwa pamoja kati ya FAO kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway hapa nchini na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na ilihudhuriwa na Mawaziri kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, Mabalozi na wakuu wa Mashirika na Taasisi za Kimataifa na Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.

Chimbuko

Programu ya Udhibiti na Matumizi Endelevu ya Rasilimali Samaki (EAF) – imekuwa ni moja ya marejeo makuu ya FAO katika kusaidia nchi katika juhudi zao za kudhibiti na kutekeleza kanuni za maendeleo endelevu.

Kanuni za FAO za Uvuvi Sahihi na pia sheria nyingi za kimataifa zinaangazia faida ambazo zinaweza kupatikana kupitia programu ya EAF. EAF ni njia ya kutekeleza Kanuni Sahihi za Uvuvi kwa kutoa muongozo wa namna ya kufikia malengo, sera ya kiuchumi, kijamii na ikolojia kupitia malengo, viashiria na njia za tathmini.

EAF inanuia kuweka uwiano kati ya mambo mawili muhimi: utunzaji wa mazingira na mifumo ya ikolojia kwa upande mmoja  na kuweza kutatua mahitaji ya binadamu ya chakula na faida za kiuchumi upande mwingine.

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi na FAO wamesaini mkataba wa programu ya ushirikiano kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya EAF-Nansen huku Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Bahari ya Norway (IMR) ikitoa huduma ya kisayansi.

Programu mpya ya EAF-Nansen imeongeza eneo jipya la kushughulikia ambalo linaangalia athari za tofauti na mabadiliko ya tabia na uchafuzi wa mazingira yanavyoathiri uzalishaji wa mazingira bahari na afya.

Serikali: rasilimali za bahari zitumike kwa maslahi ya Watanzania

Serikali imesema kuwa itahakikisha rasilimali za bahari zinatumika kwa ajili ya Watanzania wote.

Hayo aliyasema Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Ahmad Rashid alipofanya ziara ya ukaguzi wa meli ya uvuvi katika bandari ya Zanzibar.

Rashid alisema kuwa rasilimali za baharini zikitumika ipasavyo zinaweza kuleta maendeleo na kuhakikisha uvuvi unaofanyika katika bahari unafuata taratibu kwa maslahi ya taifa.

Katika ukaguzi  huo wa meli hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Ahmad Rashid pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo, Abdallah Ulega walitembelea ofisi za utoaji leseni wa meli za uvuvi  ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Alisema sheria iko wazi kwa hivyo lazima rasilimali za Tanzania ikiwemo na bahari iwanufaishe Watanzania wote bila kujali vyama vyao.

Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema Serikali zote mbili zitahakikisha rasilimali za bahari zinatumiwa na Watanzania na siyo kwa wageni tu.

Alisema watasimamia sheria za uvuvi katika kulinda rasilimali za bahari ili ziweze kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Zanzibar, Hosea Mbilinyi alisema mamlaka imepiga hatua katika kuhakisha rasilimali za bahari zinanufaisha Tanzania.

Mazingira Endelevu kwa rasilimali bahari

Mazingira ni nini? Mazingira  ni  vitu  vyote  vyenye  uhai  na  visivyoishi ambavyo  vinatuzunguka  vitu  vya  maumbile  na vilivyofanywa na binadamu. 

Mazingira yanajumuisha vitu vyote visivyoishi kama vile hewa tunayovuta maji tunayokunywa, barabara  na  nyumba, bahari  na fukwe, hata  jua, mwezi  na  vyota.  Mazingira pia  ni pamoja na  vitu  vyenye  uhai  kama  mimea:  misitu  na  mashamba makubwa,  mibuyu,  vichaka  na  nyasi,  mikoko, mwani,  nyasi  bahari, miamba  ya  matumbawe  na  mazao,  na  wanyama  wakiwemo  wanyama  pori,  samaki, vipepeo,  ndege,  nyuki, wanyama wanaofugwa  na watu.  

Kila kitu kilichopo karibu yako ambacho unaweza kukiona, kukigusa, kukihisi, kukinusa au kukisikia ni sehemu ya mazingira. Mazingira yanatupatia nini? Chakula  na  maji. Katika  Zanzibar  maji  yetu  safi  yote  yanapatikana  kutoka  maji  ya  mvua  ambayo huzama ndani ya ardhi.  Hujichuja kupitia mawe ya chokaa, nasi huchimba visima ili tupate maji ya kunywa, kupikia na kuoshea.   

Samaki  wote  tunaokula  ni  viumbe  wanaokamatwa  baharini,  na  mifugo  yetu  pia inategemea chakula na maji ya kunywa, mazao kama mpunga, matunda na mbogamboga yanahitaji udongo mzuri wenye rutuba, mvua nyingi na nyuki, ndege na popo ili kurutubisha. 

Bila ya mazingira wangelikula na kunywa nini? Afya  njema  –  Mimea  hupunguza  kasi  ya  umwagikaji  wa  maji  yanayotiririka  juu  ya  ardhi  kwa  hiyo yanazama  ardhini ambako yanachujwa  na  mawe, na  hiyo  hufanya  maji yawe salama  zaidi kunywa.  

Hewa safi (oxijini) iliyomo kwenye  hewa tunayovuta ambayo inatupa  uhai inatolewa na mimea  nayo  huchukua  na kutumia  hewa chafu kutoka kwenye  hewa.   Pia, sisi tunatumia mimea mingi inayoota Zanzibar katika kutibu magonjwa, kuanzia malaria hadi mafua: inasaidia kutuweka katika afya njema.

Mahali pa kuishi

Ukiangalia baharini kwenye ufukwe wa mashariki ya Zanzibar unaweza kuona wapi mwamba ulipo, kwa sababu ya mawimbi makubwa yanayoonekana wakati yanagonga mwamba huo. Lakini ikiwa mwamba huu hautakuwepo na kupiga kwenye ufukwe inaweza kusababisha mmomonyoko.

Miamba ya matumbawe, nyasi bahari na mikoko yote hulinda ufukwe dhidi ya mmomonyoko. Ardhini, miti na nyasi (majani) inafanya hivyo hivyo, inazuia udongo usiondolewe na kupelekwa baharini inaponyesha mvua. Bila ya vitu hivyo ardhi iliyopo chini ya nyumba zetu ingeondolewa na nyumba zetu zingeharibiwa hata kupelekwa baharini. Miti hutupatia kivuli na kuzilinda nyumba zetu dhidi ya upepo mkali. Nyumba zetu zimeezekwa kwa makuti ya minazi, mawe mchanga, saruji na miti ya mikoko: vifaa hivi vyote vinatokana na mazingira.

Maisha na ustawi wa kiuchumi

Kazi nyingi katika Zanzibar zinategemea mazingira. Asilimia 39 ya watu wameajiriwa katika sekta ya huduma (sana kwenye utalii), na asilimia 37 katika kilimo, Misitu na Uvuvi. Uchumi wote wa Zanzibar unategemea mazingira mazuri.

Maliasili Mazingira yanatupatia kila kitu tunachotaka kwa maisha. Vitu tunavyotumia tunaviita ‘rasilimali’. Rasilimali zinaweza kuwa vitu halisi, kama hewa safi au maji au rasilimali za nishati kama mwangaza wa jua au upepo.

Vitu vyote vinavyofanywa na binadamu vinafanywa kwa kutumia rasilimali ambazo hatimaye vinatokana na mazingira ya kimaumbile yanayojulikana kama ‘mali asili’. Kwa mfano saruji inafanywa kwa kuchoma chokaa, plastiki hufanywa kutokana na mafuta, na vioo vinafanywa kutokana na mchanga. Lakini mali asili zinatoka wapi? Mara nyingi, watu hufanya mambo kama vile rasilimali zote zitadumu milele, lakini kama idadi ya watu inavyoongezeka, baadhi ya rasilimali zinaadimika sana. Kwa hivyo tunapaswa tufikiri tunapotumia vitu: vimefanywa kutokana na nini? Vitu asili vimetoka wapi? Kiasi gani cha vitu hivyo watu wanatumia? Inaweza kumalizika?

Uendelevu

Nini maana ya kuwa endelevu? Kuwa endelevu maana yake ni uwezo wa kuendelea kuwepo. Tunategemea mali asili, kwa hiyo tunazihitaji ziwepo (siku za usoni) kwa ajili ya watoto wetu. Katika muktadha wa maliasili kuweza kuwa endelevu maana yake ni kutumia rasilimali siyo kwa haraka kuliko inavyoweza kupatikana tena. Tunahitaji kutumia rasilimali kwa uangalifu sasa, au hazitakuwepo tena baadae.

Rasilimali zenye kurudishwa upya na zisizoweza kurudishwa upya, Aina  mbali mbali  za  rasilimali  hufanywa  kwa  mchakato  wa  kimaumbile katika  kasi  ya  mwendo  tofauti  na  kwa  viwango  tofauti.    Kwa  mfano, mwanga  wa  jua  hufanywa  mchana  wa  kutwa,  kila  siku, lakini  mibuyu mikubwa  huchukua  mamia  ya  miaka  mpaka  ikawa  mikubwa  kiasi  hicho. 

Tunapotumia  rasilimali,  tunahitaji  kuzingatia  muda ambao  rasilimali  hizo zitachukua  kujirudi  kuwa  kama  hali  ya  mwanzo.    Iwapo tutatumia kwa haraka   rasilimali   kuliko   ambavyo   zinaweza   kurejea, basi   zinaweza kumalizika.  Huku siyo kuwa endelevu.  Ili kuhakikisha tunazo rasilimali hizo tunazohitaji  siku  za  usoni,  ni  lazima  sote  tuishi  kwa  kuzitumia  kwa  njia endelevu, tusitumie rasilimali kwa haraka kuliko zinavyoweza kurejeshwa.

Tunazingatia  kiwango  cha  kurejesha  rasilimali  katika  muda  wa  maisha ya  mwanadamu.    Iwapo  maumbile  yanarejesha  vitu  katika  muda  wa maisha  ya  mwanadamu  tunaviita  vitu  hivyo vinarejesheka.   

Maana yake ni kuwa maumbile yanaweza kuweka   tena rasilimali tunazotumia. Rasilimali  hizi  ni  pamoja  na  maji  safi,  ambayo  yanarejeshwa na mvua inaponyesha, kuni, zinarejeshwa miti mipya inapoota, samaki wanarejeshwa  na  samaki  wapya  wachanga,  na  nishati  ya jua au upepo. Lakini vitu ambavyo huchukua muda mrefu zaidi kuliko uhai wa mwanadamu huitwa visivyorejesheka.

Rasilimali zinaporejesheka 

Baadhi  ya  rasilimali  hazina  kikomo  – hutengenezwa  kwa  wingi  kiasi  ambacho  zipo  zaidi  ya tunazotumia,  kwa mfano hata tukitumia kiasi gani cha nishati ya mwangaza wa jua au upepo leo (kwa mfano kwa kuchemsha maji kwenye jua au kuendeshea jahazi au mashua)  hazitozima  jua  kung’ara  (kutoka  mwangaza)  au  upepo  usivume kesho. 

Hii ina maana tunaweza kutumia kiasi tunachopenda cha rasilimali hizi, na bado zitakuwa zinaendelea na kupatikana! Rasilimali nyingine huchukua muda mrefu zaidi kurejeshwa kimaumbile (wenyewe), zinachukua miezi, miaka,     au hata miongo kabla hazijarejeshwa kimaumbile.    Kundi  hili  ni  pamoja  na  rasilimali  hai  nyingi kama samaki  na kuni na  maji safi, ambayo yanarejeshwa katika  msimu wa  mvua.   

Tunapokata  miti  kuitumia  kwa  kuni  au  mbao  lazima  tupande mingine mipya. Tunapokwenda   kuvua samaki, lazima tuwabakishe wengine ili wazae samaki wengine. Lakini  iwapo  tutakata  miti yote  na kuwauwa samaki wote au kuyavuta  maji yote kutoka  ardhini,  hakutakuwa na kilichobaki kwa siku za usoni.

Rasilimali zisizorejesheka, Rasilimali nyingine tunazotumia zilichukua maelfu  au   mamilioni  ya   miaka  kufanyika, mara nyingi  katika   hali  ya mazingira  tofauti  na  hizi  ya  sasa. Kwa  hiyo  kwa  mtazamo wa  kibinadamu  rasilimali  hizi hazirejesheki.Tukishatumia kile kilichopo sasa  hakitakuwapo tena. 

Rasilimali  zisizorejesheka  ni pamoja  na kisukuku cha fueli,  makaa ya mawe,  mafuta, gesi,  na  vitu  vinavyotengenezwa  kutokana  navyo,  pamoja  na  plastiki. Nyingine  ni  rasilimali  za  madini mawe  na  mawe  ya thamani. Uchimbaji  wa  rasilimali  hizi  na  gharama nyingine  za kimazingira tunahitaji kutafuta rasilimali  mbadala,  zenye kusarifika  na kuendelea ili tusizitumie sana.

Kwa nini kuwa endelevu ni muhimu?

Tunategemea  mazingira  kwa  namna  nyingi  mno  kwa  ajili  ya  kujipatia  riziki,  lakini  iwapo  haturuhusu rasilimali kuongezeka kutokana  na kutumiwa sana, basi samaki tunaokula watatoweka, hatutakuwa na kuni za kupikia, wala  maji ya kunywa. 

Kama vile tunavyotegemea mazingira nayo yanatutegemea pia kwa sisi kuyaangalia na kuyatumia kwa busara. Lakini hatutumii rasilimali kiuendelevu.  Misitu  katika  Zanzibar  inapungua  kwa  kasi,  idadi  ya  samaki inapungua.  Kiwango cha maji yaliyopo ardhini kinashuka na visima vya pwani vinakuwa na maji chumvi na yasiyonyweka. 

Rasilimali zinaondoka, na iwapo hatutachukua hatua sote kuanzia sasa tutakuwa katika shida kubwa baadae. Huu ndiyo mustakbali ambao vijana wa Zanzibar wataurithi. Kwa hivyo tunaweza kufanya nini? Tuko  katika  kipindi  cha  historia  ambacho  bado  zipo  rasilimali, tunaelewa  athari  tunayopata,  na  bado  tunao  muda  wa kuchukua  hatua.

Ni juu yetu kubadili namna tunavyotumia rasilimali na tuzitumie ili zidumu, kuanzia sasa.   Ni vizuri kuvua samaki lakini siyo wengi kiasi ambacho hawabaki kwa siku za usoni. Samaki  wanahitaji  muda  kukua,  kupata  mwenza  wa  kuzaa  kama watu na wanyama wa kufugwa wanavyofanya.  Miti pia inahitaji muda kukua – tusikate miti kwa haraka sana kuliko inavyoweza kuota na kurejea.

Bioanuwai

Bioanuwai ni nini? Bio  maana  yake  ni  maisha,  na anuwai  ni  aina,  kwa  hiyo, bioanuwai  ina  maana  ya  aina  ya  maisha.  Inajumuisha  vitu  vyote  vinavyoishi  duniani  na  katika  bahari,  kuanzia  nyangumi  wakubwa  kabisa  mpaka bakteria wadogo kabisa. 

Mahali ambapo aina nyingi tofauti, au ‘spishi’, au  vitu  vyenye  uhai hukua pamoja, kama vile mwamba wa matumbawe au msitu, panasemekana kuwa na bioanuwai nyingi, na mahali ambapo pana spishi chache, kama shamba lililolimwa, au maeneo ya mjini, pana bioanuwai wachache.

Spishi  adimu,  kuwa  na spishi  nyingi sio jambo la  pekee muhimu lakini ni muhimu pia (kujua) kama spishi  hizo  zinapatikana mahali pote. Spishi adimu ni maalum sana. Kwenye visiwa, kwa sababu makundi ya  mimea  na  wanyama wametengwa  na  bahari na makundi  mengine  ya mimea  na  wanyama,  pole  pole wanabadilika kuweza  kujirekebisha  kwa  hali  za  hapo.

Baada  ya  muda,  mimea  na  wanyama  hao  huwa tofauti sana  na jamaa  zao kiasi cha kuwa spishi mpya.  Sehemu  za  visiwa kwa hivyo, ni muhimu sana kwa viumbe anuawai kwa sababu kunaelekea kuwa na spishi adimu zaidi kuliko maeneo ya bara yenye ukubwa kama huo.

Bioanuwai katika Zanzibar: makazi na spishi Makazi ya baharini, Kuna aina nyingi tofauti za makazi ya baharini katika Zanzibar kuanzia ufukweni mpaka kwenye bahari iliyo wazi.  Kila makazi yanamudu mamia ya spishi, na bioanuwai katika Zanzibar ni maarufu duniani kote. 

Spishi nyingi  huishi sehemu ya maisha yao katika  makazi moja  na waliobaki  huishi mahali pengine, kwa hiyo makazi ya bioanuwai ni muhimu sana.

Makazi ya chini ya maji ni vigumu kuyagundua, lakini kuna mengi ya kugundua kwa kutembea tu ufukweni na  sehemu  za  baharini  wakati  wa  maji  kupwa. 

Kwa mara ya kwanza, fukwe zenye mchanga zimeweza kuonekana hazina viumbe isipokuwa minazi. 

Lakini viumbe wamejificha hapa – lazima ujue pa kutazama. Chimba  chini  kidogo  tu  na  unaweza  kuona  chaza;  kaa pepo  wanaishi  katika  mashimo  na  hutembea  kwa haraka  sana,  kwenye fukwe  na  unaweza  kuwaona  kwa  shida;  kaa  watawa  wamejificha  vile  vile katika makome ya  viumbe wengine. 

Fukwe  zenye  mchanga  ni muhimu kwa makazi ya matagio ya kasa, ambao huja ufukweni  usiku  na kutaga mayai yao chini ya mchanga.  Zanzibar inao spishi za kasa bahari, maarufu wao ni kasa wa kijani (green turtle) na kasa wa kawaida (hawksbill). 

Fukwe  zenye  mchanga  hutumika pia kwa ndege  malapulapu ambao wanakula samaki  na kombe: korongo, bua bua,  ndoero, na wengine wengi.  Fukwe  za  maweni  ni  mahali  muhimu  kwa  kuangalia  bioanuwai  wa  baharini.   

Vidimbwi vyenye mawe vinaweka anemone, kaa, mwanamizi na samaki wachanga, na wanyama kama kombe wa baharini.  Aina ya konokono bahari (littorina)  na  ‘barnacles’ ambao wanaambatana  na  miamba  na kuganda chini ya  vyombo.  Sehemu  hizi asilia  za kujionea samaki  na  viumbe wengine ‘aquarium’  vinakufanya  uone aina  nyingi tofauti za viumbe wa kushangaza bila ya kuwasumbua.  Ukibahatika sana unaweza kuona hata pweza.  Wanyama wengi unaoweza kuwaona ni wa ajabu kuliko unavyoweza kufikiria! 

Maji yanapokupwa mfumo mwingine wa ekolojia unaonekana, vitalu vya nyasi bahari vinaota katika mchanga na matope.  Nyasi bahari zinasaidia viumbe wengi wa kuvutia sana majongoo bahari, mwanamizi na aina nyingi za kombe / chaza.   Kwenye vitalu vya nyasi vya maji mengi, kasa wanakula majani pia.

Kati  ya  mifumo  yetu  ya  ekolojia  ya  baharini  inavutia  sana  ni miamba ya  matumbawe. Chini ya  mawimbi yamejificha  mamia ya spishi ya  matumbawe  yenye  rangi  za  kung’ara,  sponji,  kaa, kamba wakubwa, samaki  wa miamba, papa,   taa na mara nyingine  hata  wanyama  wakubwa  duniani nyangumi  (whale shark).

Mbali na miamba katika bahari  kuna  viumbe  wa ajabu sio haba wanyama wa hapa petu tu ni spishi 8  za pomboo, 3 za nyangumi na aina moja ya nguva (dugong).  Mfano wa aina za pomboo ni pomboo kikomo, pomboo madoto, pomboo mweusi pia nyangumi mwenye nundu, wote wanapatikana katika Ghuba ya Menai. Msitu  pori  –  Miti  huipa  misitu  muundo  ambao  hutoa  sehemu nyingi  kwa spishi kupata  makazi.   

Kila spishi za miti zinavyoota msituni ndivyo inavyosaidia bioanuwai wengi zaidi.   Misitu  ya pwani  ya  Afrika  ya  Mashariki  inafanya  mojawapo  ya  maeneo  ya misitu 25 muhimu ya bioanuwai duniani. Kuna aina tatu kuu za misitu pori katika Zanzibar. Msitu mnyevunyevu hustawi   na ni kijani sana.

Miti   hukua   haraka, mikubwa na mirefu, na majani yao yanapoanguka, huoza na kufanya udongo mnene wenye rutba.  Sehemu kubwa ya msitu mnyevunyevu ya Zanzibar ipo Pemba, lakini upo msitu mnyevunyevu Unguja Kaskazini na Jozani.

Msitu  unaoota  pembezoni  mwa fukwe  kwenye  mawe mawe  huota  katika  maeneo  yenye  mvua kidogo,  na  miti  yake  inaweza  kuhimili  ukame.    Huota  katika  Ukanda  wa  matumbawe  chokaa  ambayo inapitisha maji kwa urahisi, kwa hiyo maji ya mvua hupotea haraka. 

Maeneo makubwa kabisa ya msitu wa aina hii inayokuwa juu ya mawe katika Zanzibar yapo Kusini Mashariki ya Unguja.  Mikoko huota Ukanda wa pwani na inavumilia chumvi.  Mikoko ni muhimu kwa sababu inazaa sana (miti yake huota haraka) na ukuaji huu hutoa chakula kingi kwa wanyama pori.  Visiwa vyote viwili vikuu vinahimili mikoko mikubwa na muhimu ambayo  inafanya  kazi  ya  sehemu  za  malezi  kwa  samaki  wengi  wanaoishi  baadae  katika miamba  ya matumbawe. Zanzibar ni   nyumba   ya   zaidi   ya spishi 50   za wanyama wakiwemo wanyama wa hali ya juu kama nyani, kima punju adimu kima bluu Sykes’ na spishi tatu za komba. 

Tunazo spishi mbili za paa,  akiwemo  paa  nunga  (Ader’s  duiker)  ambaye  yupo hatarini kutoweka:  wamebaki  chini  ya  500  duniani  karibu  wote  wakiwa Zanzibar.    Pia  tuna spishi 23  za  popo  pamoja  na  popowa  wa Pemba  anayeruka  (flying  fox).   

Popo wadogo hula wadudu, na wakubwa hula matunda. Mojawapo  ya  kivutio  kisichoaminika  au kinachoshangaza  cha  Zanzibar  ni  uhamiaji  wa  popo  wanaokula matunda   wakati   wa   kutua   jua   wanapotoka   visiwa vilivyoko baharini,  ambako  hulala  mchana  na  kuelekea  msituni ambako hula wakati wa usiku.

Zipo spishi 177  za  ndege,  pamoja  na  chozi  ambaye  ana  rangi inayong’ara,  tai  adimu  na  chiriku  ambao  ni  shida  kuwaona  lakini sauti   zao nzuri ni rahisi kuzisikia, hususan kabla ya jua kuchomoza.

Pemba ni maarufu kwa ndege wake adimu: kinengenenge  wa  Pemba,  njiwa  manga  wa  kijani  wa Pemba, chozi wa Pemba na bundi wa Pemba. Zipo spishi kadha za nyoka na mijusi, maarufu   sana ni kinyonga, anayeweza kubadili rangi yake   ioane na mazingira!  Wapo baadhi ya wanyama   wadogo wadogo maalum pia, wakiwemo  kaa  mnazi  mkubwa  adimu  (coconut  crab),  na maelfu ya wadudu:  vipepeo  vizuri, kerengende wanaocheza, vimetameta na ‘mwindaji’ anayevamia kwa kushambulia, na vunja jungu.

Ardhi  ya  binadamu

Sehemu  kubwa  ya  ardhi  ya  Zanzibar  imebadilishwa  na  wanadamu kuwa ardhi  ya kilimo, vijiji na miji. Lakini wapo bioanuwai hapa.  Ardhi ya kilimo  ni muhimu kwa ndege,  nyuki,  na vipepeo na kutoa nafasi ambayo wanyama pori,  wanaweza  kuitumia  katika  kwenda katika  maeneo ya misitu ya kimaumbile.

Hata vijijini kuna wanyama pori, kwa vile spishi nyingi za msituni zinaweza kuishi  miongoni mwa binadamu, mradi tunawachia miti na vichaka baina ya nyumba zetu.

Kwa nini bioanuwai ni muhimu?

Bioanuwai  ni  muhimu kwa  sababu  viumbe  hai  wanategemeana  kwa  chakula  na  mahali  pa  kuishi  na kuzaa.

Viumbe  hai  kama  sisi  wenyewe  ni  sehemu  ya  mtandao  wa  maisha,  na  sisi  pia  tunategemea  vitu mbalimbali vinavyoishi kwa chakula chetu, kwa hewa tunayovuta na kwa njia  zetu za kujipatia riziki.  Iwapo tutauvuruga uwiano wa maumbile kwa kusababisha spishi kufa, mfumo unakuwa siyo sawa na mfumo mzima wa ekolojia unaweza kuharibika.  Mara nyingine hali hii huyafanya maeneo yasikalike kwa watu kwa mfano yanaweza kugeuzwa jangwa: iwapo miti yote itakatwa, udongo hupeperushwa na mimea kidogo tu inaweza kuota.

Mimea  inatoa  oxijini  (hewa  safi)  tunayoihitaji  ili  tuishi. Mimea  inayoota  hufyonza  gesi  hatari,  na kupunguza  athari  ya  mabadiliko  ya  hali  ya  hewa. Dunia  ya  kimaumbile  ni  nzuri;  watu  wanaoishi  au wanaotumia  muda  katika  maeneo  ya  kimaumbile  wana  afya  zaidi  kuliko  wale  wanaoishi  katika  maeneo ambayo  hewa  imechafuliwa.

Maelfu  ya  mimea  hutumika  katika  dawa  za  asili  za  Zanzibar. Ni muhimu kuhifadhi aina mbalimbali za viumbe wa msituni ili kuilinda mimea hii, na mingine pia, kwa vile wanasayansi wanatafuta tiba mpya na bora.

Maji – Misitu husababisha mvua kwa kupunguza mwendo wa mawingu yanapopita juu kwenye ardhi: miti na mimea huyachuja maji na kuyafanya maji ya chini ya ardhi salama kwetu kuyanywa. 

Maeneo yaliyo  na miti  na  mimea  mingi  hupunguza  mwendo  wa  maji  yaliyopo  juu  ya  ardhi,  kwa  hiyo  maji  huzama  ndani  ya ardhi badala ya kutiririka na kuupeleka udongo baharini. Chakula bioanuwai  hutupatia  mamia ya samaki tunaokula  na miti au  mbao tunazohitaji kutengenezea mitego  na  kujenga  mashua  za  kuvulia,  na  moto  wa  kupikia. Wadudu, popo na ndege wote wanasaidia kuchavusha mazao tunayolima. 

Viumbe waliomo katika  udongo  vile  vile ingawa  ni wadogo sana, kiasi cha kutoweza  kuonekana,  huyavunja  majani  ya  miti  iliyokufa  na  kuyageuza  yawe  udongo  wenye  rutuba  kwa kupanda mazao, ndege, nyoka na wadudu wanaokula wengine wanakula wadudu wanaoharibu mazao.

Malazi, miti  hupunguza  athari  ya  upepo  katika  dhoruba  na  hutoa  kivuli  kutokana  na  jua  kwa  ajili  ya familia zetu, nyumba, mifugo na mazao.

Malighafi tunayotumia kujengea nyumba zetu – aina mbalimblai za mbao, miti, mapaa, na chokaa vyote vinatokana na vitu vya maumbile. Njia  za  kujipatia maisha  (riziki) Utajiri  wa  wanyama  pori  wa  Zanzibar  unavutia  maelfu  ya  watalii  kila mwaka kutembelea  msitu wa Jozani, kuogelea  na pomboo, kuzamia  ndani ya  maji  na kupiga mbizi chini ya maji. 

Wafanyakazi wote katika kazi ya uvuvi, kilimo au utalii wanategemea aina nyingi za wanyama na mimea mikubwa na midogo kwa kupata riziki zao.

Kwa nini wanyamapori wa Zanzibar wamo hatarini?

Inapokuwa  idadi  ya spishi iko  chini  au  inapungua, spishi hiyo  imo  katika  hatari  ya  kutoweka  kabisa,  au ‘imo hatarini’. 

Hii inaweza kuwa kwa sababu ya tishio kwa mmea au mnyama mwenyewe, au kwa sababu makazi yake mahali anapoishi panaharibiwa au panatoweka.

Binadamu  wanashindana  na  mimea  na wanyama  katika  Zanzibar  kwa  rasilimali  na  nafasi  ya  kuishi,  na  baadhi  ya spishi tayari  wameshapotea bioanuwai inapungua Zanzibar. Kuuliwa moja kwa moja Spishi nyengine zinauliwa makusudi.

Tunavua idadi kubwa ya samaki kila siku kwa ajili ya chakula, na watu wengine pia huwinda paa.  Tunakata miti kwa ajili ya kuni, mkaa, mbao za kujengea  nyumba, mashua na ngalawa, na   samani. Spishi nyingine  wanavuliwa  kwa  sababu   ya kibiashara baragume ‘tritoni’, kombe, chaza na magamba ya kasa yanauzwa kama mapambo, na   mapezi ya papa yanasafirishwa nje ya nchi.

Tunawauwa baadhi ya wanyama kama nyoka kwa sababu tunawaogopa. Mara nyingine kuwauwa moja   kwa moja sio makusudi;  pomboo  na  nyangumi  wa  baharini  na  kasa  hukwama katika nyavu.  Uuwaji wa moja kwa moja usio dhibitiwa una athari kubwa  sana  katika  idadi  yao na  wengi  wa spishi hizo  wamo hatarini wakiwemo  papa,  kasa,  pomboo,  na  baragumu. Kuna spishi moja,  ambayo  ilikuwa  ya  aina  yake  kwa  Zanzibar  lakini tumeshachelewa. 

Chui wa Zanzibar aliwindwa mpaka akatoweka kabisa katika miaka ya 1990. Upoteaji  wa  makazi  kutokana  na  udhalishaji  na  uharibifu Tunaharibu miamba  ya  matumbawe baharini  na  vitalu  vya  nyasi  bahari  kwa  kutumia  vifaa  vya  uvuvi  kama  nyavu  ya  kukokota  na baruti. 

Maendeleo ya pwani na mmomonyoko wa ardhi inasababisha kasa wasiweze tena kupata mchanga mkavu ufukweni  kwa  ajili ya  kutaga  mayai  yao  na  kulalia  wakati  wa usiku.    Kasa  wachanga  huchanganyikiwa kutokana  na  mwanga  mkali  unaotoka  hotelini,  kwa  hiyo,  hupotea  na  hawawezi  kuijua  njia  ya  kwenda baharini!  

Uchimbaji wa  mchanga  na  mawe  ya  chokaa  ni  tatizo  kubwa  sana  katika fukwe  na  hata  ndani kwenye ardhi.  Misitu inakatwa Zanzibar, lakini hususan katika ukanda wa pwani ili kupisha kilimo, barabara, nyumba  na  hoteli: kilimo cha kuhama  hama kukata au kuchoma eneo la msitu kwa ajili ya kupanda  mazao, halafu   kwenda   katika   eneo   jingine baada ya miaka michache bado inaendelea, lakini namna kinavyofanywa  sasa  siyo  endelevu.   

Kimila  mashamba  ya  zamani  yaliachwa  ili  misitu  iote  tena,  lakini  sasa watu wengi sana wanahitaji ardhi ya kulima kiasi cha kuwa msitu hauachwi uote tena. Spishi haribifu Mara  nyingine,  watu  wanapokwenda  duniani  huchukua wanyama  na  mimea  kutoka mahali  pamoja  na  kuwaanzisha  mahali  pengine,  ambapo  si  pao.

Kwa  kawaida  hawaishi, lakini iwapo hawana  wanyama  wanaokula  wenzao katika hapo mahali papya, wanaweza  kuzaa  kwa haraka sana na kuangamiza  idadi  kubwa ya  mimea  au  wanyama  wa  hapo,  na  kuchafua  usawa  wa  kimaumbile  wa  mfumo wa  ekolojia.

Meli  hupeleka  panya  visiwani  ambapo  kwa  haraka  sana  huwamaliza  ndege  wanaojenga ardhini. Spishi haribifu  mbaya  kabisa  wa  Zanzibar  ni  kunguru  wa  nyumbani aliyeingizwa  kutoka India. 

Kunguru wapo kila mahali, wanakula  uchafu wa chakula  na mboga na  ndege wa kienyeji  na  mayai yao, mijusi,  vyura  na  wanyama  wengine  wadogo.    Idadi  ya spishi za  kienyeji  zinapungua  Zanzibar  pote,  lakini hasa  Pemba  ambako  wawili  kati  ya spishi nne  za  ndege  adimu  wanahofiwa  wametoweka  sasa.

Paka wa kufugwa wanaweza kusababisha matatizo iwapo wataingia porini, wanazaa kwa haraka, hawana wanyama wanaowala, na wanakula vinyama vidogo, ndege na mijusi. Uchafuzi  wa  hewa Usimamiaji  wa  takataka  katika  Zanzibar hautoshelezi,  na  plastiki,  kemikali,  maji machafu  na  vitu vingine vingi  vinasababisha  matatizo  makubwa  kwa bioanuwai.

Kemikali  hususan  dawa za kuulia wadudu, sumu ya wanyama pori, vipande vya plastiki vinapenya kuingia kwenye mazingira ambako wanyama  wengi  wanaufananisha  na  chakula,  kwa  hiyo  matumbo  yao  hujaa  na  kwa  hiyo  hufa  kwa  njaa. 

Uchafuzi  wa  hewa  unachangia  katika  ongezeko  la  idadi  ya  kunguru  wa  majumbani  kwa  njia  isiyo  dhahiri, kwa kusababisha athari ya kupungua kwa wanyama pori. Ilikuwa tayari ni nadra ulipochapishwa huu mhuhuri mnamo 1984, Chui wa Zanzibar tayari ameshatoweka.