Breaking News

Tancoal yatekeleza ajenda ya uchumi wa viwanda kwa vitendo


Tancoal yatekeleza ajenda ya uchumi wa viwanda kwa vitendo

Kampuni ya Tancoal ilisajiliwa na Msajili wa Makampuni mnamo mwaka 2008. Tancoal iliingia ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kitengo chake cha uwekezaji, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambalo linamiliki asilimia 30 ya hisa na Kampuni ya Intra Energy (Tan­zania) Limited (IETL) ambayo inamiliki asilimia 70 ya hisa. IETL ni kampuni tan­zu ya Intra Energy Corporation Limited, kampuni ambayo imeorodheshwa kati­ka Soko la Hisa la Australia (ASX:IEC).

Kampuni ya Tancoal ilisajiliwa na Msajili wa Makampuni mnamo mwaka 2008. Tancoal iliingia ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kitengo chake cha uwekezaji, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambalo linamiliki asilimia 30 ya hisa na Kampuni ya Intra Energy (Tan­zania) Limited (IETL) ambayo inamiliki asilimia 70 ya hisa. IETL ni kampuni tan­zu ya Intra Energy Corporation Limited, kampuni ambayo imeorodheshwa kati­ka Soko la Hisa la Australia (ASX:IEC).

Tancoal ni kampuni ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe ikifanya shu­ghuli hizo kwa sasa kwa kutumia leseni yake ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe iliyopo eneo la Mbalawala, Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma.

Makaa ya Mawe ni nini?

Makaa ya mawe si madini maarufu sana kwa watu wengi na ni bado bidhaa mpya kwa Watanzania wengi. Makaa ya mawe ni madini ya nishati na pia ni malighafi kwa wakati mwingine.

Makaa ya mawe ni mwamba wenye mchanganyiko wa baina ya aidha rangi nyeusi na kahawia au nyeusi na nyekun­du iliyoiva, huundwa kama mkanda wa mwamba unaojulikana kama coal seams. Sehemu kubwa ya makaa ya mawe ni kaboni ikiwa sambamba na viambata mbalimbali vya elementi zingine kama vile haidrojeni ambayo imechukua sehemu kubwa pia, sulphur, oksijeni, na naitrojeni. Makaa ya mawe hutengenezwa pale ambapo mmea ulio­kufa unapooza na kutengeneza mada ijulikanayo mboji (peat) na baada ya kupita kwa kipindi cha zaidi ya miaka milioni ya kupigwa na jua na mgandam­izo, mada hiyo ya mboji hubadilishwa na kuwa makaa ya mawe.

Makaa ya mawe kutoka katika mgodi wa Tancoal yana ubora wa hali ya juu sawa na yale ya yanayouzwa kule Afrika ya Kusini na wakati mwingine huzidi ubora makaa hayo ikilinganishwa na makaa ya mawe ya Afrika ya Kusini. Makaa ya mawe yanafaa kwa ajili ya matumizi ya viwanda na vituo vya uza­lishaji wa umeme vinavyotumia makaa ya mawe.

Uchimbaji wa makaa ya mawe

Tancoal ilikabidhiwa rasmi leseni ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe namba 439 Mwezi Agosti 18, 2011 na Waziri wa wakati huo aliyekuwa na dha­mana ya Nishati na Madini. Leseni hiyo ilitolewa kwaajili ya eneo la Mbalawala, Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma. Tancoal ilianza shughuli za uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe rasmi mwaka 2011.

Mgodi wa Makaa ya mawe wa Tan­coal unapatikana Ngaka, katika eneo linaloitwa Mbalawala upande wa Kusini na Mbuyura ikiwa upande wa Kaska­zini, eneo hilo likiwa na tani 216 na 207 za mtaji mkubwa wa rasilimali na hii kwa ujumla inafanya kuwe na jumla ya tani 423 za rasilimali hizo za Makaa ya mawe. Tancoal ni kampuni kubwa ya uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Uwezo wa uzalishaji wa makaa ya mawe

Tancoal ina uwezo wa kuzalisha tani takriban 90, 000 za makaa ya mawe kwa mwezi huku mahitaji ya sasa ya soko yanaanzia tani 55,000 mpaka 65,000. Uwezo wa Tancoal wa kuzalisha makaa ya mawe unaakisi mahitaji ya soko kati­ka namna ya kwamba kampuni inaweza kuongeza au kupunguza uwezo wake wa uzalishaji kwa ajili ya mahitaji ya soko lolote.

Tofauti na bidhaa nyingine ambazo zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mre­fu, makaa ya mawe kwa kawaida huwa katika hatari ya kuungua moto (muwa­ko) na hivyo ni lazima yahifadhiwe na kuwekwa chini ya uangalizi wakati wote na hayawezi kukusanywa mengi kwa muda mrefu sana.

Soko la ndani la makaa ya mawe

Soko la ndani la makaa ya mawe tan­gu mwanzo lilikabiliana na ushindani mkali kutoka kwenye makaa ya mawe yaliyokuwa yanaagizwa kutoka Afrika ya Kusini. Makaa ya mawe ya Afrika Kusini yalinunuliwa kutoka bandari ya Richards Bay na kuingia Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kiwango cha bei nafuu ikilinganishwa na makaa ya mawe ya ndani. Sababu kuu ya makaa hayo kuuzwa kwa bei za chini ilikuwa ni ukosefu wa ushuru wa makaa ya mawe yaliyoagizwa kutoka Afrika ya Kusini, lakini pia changamoto za kusafirisha makaa ya mawe kutoka kwa mgodi hadi kwa wateja. Gharama za usafirishaji zilifanya makaa ya mawe yanayozalishwa ndani kuwa na ghara­ma kubwa ikilinganishwa na makaa ya mawe yaliyokuwa yakisafirishwa kwa kutumia njia ya reli kwenda bandarini Afrika ya Kusini.

Hali hii ilibadilishwa wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliyechukua hatua ya kupiga marufuku uingizaji wa makaa ya mawe nchini. Kuanzia hapo, Tancoal ilishuhudia ukuaji wa soko kutoka kwenye viwanda vya ndani. Makampuni mengine yalihama kutoka kutumia malighafi ya mkaa wa kuni na kuni za miti kuanza kutumia makaa ya mawe ya Tancoal – ambayo yanafanya kazi kubwa katika kuokoa misitu. Kwa nyongeza, uamuzi huo wa Rais Magufuli pia ulisaidia kuanzishwa makampuni mengine ya makaa ya mawe nchini Tan­zania, makampuni madogo na ya kati.

Asilimia kubwa ya Makaa ya mawe kutoka Tancoal huuzwa nchini kwe­nye viwanda ambako hutumiwa katika matanuri hususan wakati wa mchakato wao wa uzalishaji wa bidhaa. Tancoal inauza asilimia 75 ya makaa ya mawe yaliyozalishwa katika soko la ndani. Wateja wakuu wa Tancoal ni viwan­da vya saruji, viwanda vya jasi (gyp­sum), viwanda vya vyombo vya udongo (ceramics) na viwanda vingine vya bid­haa. Viwanda hivyo vya saruji ni pamoja na Tanga Cement, Lake Cement, Mbeya Cement na Dangote Cement. Wateja wengine wa ndani (ambao si saruji) ni pamoja na; Keda Tanzania Limited, Knauf Tanzania Limited, Sayona Lim­ited na 21st Century Textile lim­ited, (kwa uchache tu).

Tancoal pia inaangalia kuin­giza kampuni kubwa ya saruji katika orodha ya wateja wake ambayo ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Mteja huyu anatazamiwa kuinufaisha kam­puni ya Tancoal akitazamiwa kuwa na wastani ya matumizi ya tani 1.2 Milioni kwa mwaka.

Soko la nje la Tancoal

Tancoal inauza nje asilimia 25 ya uzalishaji wa makaa ya mawe ya kila mwezi, kwa wateja wa nchi za Afrika Mashariki, zikiwa­mo nchi za Uganda, Rwanda na Kenya. Tena zaidi, mauzo haya ni kwa viwanda vya saruji na viwanda vya vyombo vya udon­go (ceramics).

Soko la nje bado ni dogo kuto­kana na ushindani kutoka kwe­nye makaa ya mawe kutoka Rich­ards Bay, Afrika Kusini, hasa kwa wateja wa Ukanda wa Pwani.

Hata hivyo, ni ukweli kwamba mahitaji ya makaa ya mawe ya Tancoal ni makubwa, na tayari kumekuwa na maulizio kutoka kwa wateja wengi kutoka Ethio­pia, Madagascar na Uturuki.

Ushindani wa kuuza nje makaa ya mawe ya Tancoal unakabiliana na changamoto ya gharama kubwa za usafirishaji kuharakisha kutoa makaa hayo ya mawe kutoka mgodini kwen­da katika bandari ya Mtwara. Iwapo mipango ya Serikali ya kujenga reli ya Ukanda wa Kusini kuelekea Mtwara itatimia, ita­ongeza mauzo ya nje na hivyo kuiingizia nchi fedha za kigeni.

Ukuzaji wa shughuli za uchimba­ji wa makaa ya mawe Tanzania

Pongezi nyingi ziende kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kufuatia katazo lake la uingizaji wa makaa ya mawe nchini na tangu hapo nchi ime­kuwa ikishuhudia ukuaji wa shu­ghuli za uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe.

Tancoal sio kampuni pekee ya madini ya makaa ya mawe nchini, kuna makampuni men­gine, madogo na ya kati ambayo yanafanya uchimbaji huo. Kwa hivyo marufuku hiyo ya uagi­zaji wa makaa ya mawe, sio tu imeisaidia Tancoal, lakini hata makampuni mengine ambayo sasa tunatoa nayo huduma kati­ka soko moja.

Tancoal imeongeza uzalishaji wake wa makaa ya mawe na mauzo kwa zaidi ya mara mbili katika miaka minne (4) iliyopita. Kiasi cha makaa ya mawe kili­chouzwa kati ya Juni 2014 hadi Julai 2015 kilikuwa 237,735.93. Tancoal iliuza jumla ya makaa ya mawe 520,950.00 kuanzia Juni 2018 mpaka sasa (miezi kumi). Hii ni zaidi ya mara mbili ya makaa ya mawe yaliyouzwa mwaka 2014/2015. Ongezeko hili la mahitaji na mauzo ni lime­sababishwa na uamuzi wa Rais Magufuli, uliotajwa mapema.

Mapato na Kodi za Serikali

Tancoal imelipa kwa Wiz­ara ya Madini tangu mwaka wa 2016 hadi leo, jumla ya shilingi 5,312,998,094,57 ikiwa ni kodi ya mrabaha, ada ya ukaguzi na vibali vya mauzo ya nje ya nchi.

Kulingana na ongezeko la mauzo na uwezekano wa kuon­gezeka kwa masoko zaidi ya kuuza nje, kiasi hiki kitaongeze­ka kwa siku za usoni. Tancoal ililipa tena Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) kodi kuanzia 2016 hadi sasa kama ifuatavyo:- PAYE Tshs 4,717,335,991.63, Kodi ya zuio Tshs 1,756,336,429.03, ushuru wa maendeleo ya ujuzi (SDL) Tshs 1,094,096,922.23, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Tshs 11,478,546,081.38, Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa bidhaa zinazoingiz­wa nchini : Tshs 650,429,995.00, Kodi ya makampuni AMT: Tshs 398,217,239. Pia, Tancoal ime­lipa ushuru wa huduma kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga kutoka 2016 mpaka sasa kiasi cha Shs 622,942,104.11. Wateja wa Tancoal, kwa upande mwingine, walilipa kodi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mbinga kutoka 2018 hadi leo hadi kiasi cha Tsh 1,288,506,860 / =.

Tancoal na ajenda ya Tanzania ya viwanda

Dhamana ambayo Tancoal imeibeba katika usambazaji wa Makaa ya Mawe imevifanya viwanda viwekeze hapa Tanza­nia, mfano Keda Tanzania. Pia, kampuni ya Hengyuan Cement ambayo inaweza kuwa mzal­ishaji mkubwa wa saruji nchini Tanzania iko mbioni kuwekeza. Tancoal inasambaza makaa ya mawe kwa viwanda vya saruji ambayo hutumiwa kutengeneza saruji ambayo pia hutumiwa kwa ajili ya ujenzi wa viwan­da vingine na katika miradi mikubwa katika nchi ambayo yote huimarisha viwanda. Kwa mfano Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Mradi wa Kufua Umeme wa Stiegler’s Gorge, Madaraja, barabara, nk.

Tancoal husambaza makaa ya mawe kwa viwanda vingine mbalimbali, kama vile vya jasi (gypsum) na viwanda vya vyom­bo vya udongo (ceramics) na viwanda vingine vya utengenez­aji wa bidhaa, ambapo vyote kwa pamoja vinaunga mkono ajenda ya viwanda na kusaidia uchumi wa nchi.

Kuziunga mkono bidhaa za ndani

Tancoal ilikuwa inatumia na inaendelea kuunga mkono bid­haa za ndani, hata kabla ya mahi­taji haya ya kutumia bidhaa za ndani kuingizwa katika sheria. Tancoal hushirikiana na watu wa ugavi nchini / au makandarasi katika shughuli zake zote kadri iwezekanavyo. Ni kwa bidhaa tu ambazo hazipatikani au haziten­genezwi ndani ya nchi ndiyo Tancol huagiza nje ya nchi kwa ajili ya shughuli za uendeshaji za Tancoal na asilimia kubwa ya bidhaa hizi ni vipuri kwa ajili ya vifaa na baruti/zana za mlipuko zinazotumika katika shughuli za mgodi.

Tancoal ina wafanyakazi 191 walioajiriwa moja kwa moja na kati ya hawa, wafanyakazi 189 ni Watanzania, na wawili ni wataalamu kutoka nje ya nchi. Tancoal inajivunia wafanyakazi Wakitanzania na inawasaidia sana. Watu wa ugavi na wakan­darasi wanaotoa huduma Tan­coal wameajiri moja kwa moja wafanyakazi 228, wengi wao wakiwa ni Watanzania. Idadi hii haihusiani na waajiriwa wasio wa moja kwa moja (vibarua na wanufaika kutokana na wafan­yakazi) zilizotengenezwa na Tancoal na makandarasi wake.

Tancoal huajiri zaidi kutoka kwa jamii zinazozunguka mgodi na ndani ya Mkoa na hivyo kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa watu wanaoishi jirani na mgodi.

Shughuli za kijamii (CSR)

Tancoal inafanya kazi kwa karibu na viongozi wa Vijiji na mamlaka nyingine za Seri­kali za Mitaa na Wilaya zilizo karibu na mgodi ili kufikia lengo la kusaidia jamii katika namna yenye tija. Mabadiliko ya she­ria za madini yalifanya shughuli za kusaidia jamii kuwa wajibu wa kisheria kwa makampuni ya madini na Tancoal inakubaliana na sheria na tayari mpango wa kushirikiana katika shughuli za kijamii umeshapitishwa na mamlaka husika. Shughuli za usaidiaji jamii zinajadiliwa kwa karibu na kuchaguliwa na mamlaka za mitaa huku Tancoal ikifuatilia kwa ukaribu na kusi­mamia miradi iliyoidhinishwa. Shughuli za usaidiaji jamii zime­onyesha kuwa zinafaa kutokana na matokeo yake katika kucha­giza athari chanya za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kwa jamii husika.

Tancoal inasaidia shirika la wanawake walioko karibu na mgodi linaloitwa Mbalawala Women Organization (MWO). Kwa msaada wa Tancoal, chama hicho pamoja na mambo men­gine, hutengeneza mkaa (Bri­quettes) wa makaa ya mawe ambao ni mbadala wa mkaa na kuni au kuni katika kupikia kwa taasisi mbalimbali na kwa matu­mizi ya majumbani. Mkaa wa makaa ya mawe huuzwa nchini kote na utakuwa unapatikana katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya SabaSaba huko Dar es Salaam, katika banda la Tancoal. Shirika hilo linaun­dwa na kuendeshwa na Wan­awake kutoka katika vijiji vili­vyozunguka mgodi na imeona mafanikio makubwa katika siku za hivi karibuni kuhusiana na kuwawezesha wanawake katika maeneo husika.

Dhana ya Tancoal ilikuwa kuwawezesha wanawake karibu na mgodi, kwanza kwa kuwa­fundisha shughuli mbalimbali na pia kuwawezesha kiuchumi ambapo itawapa sauti katika familia na jamii zao. MWO pia huusika na shughuli za kilimo na utengenezaji bustani ambazo uhudumia mgodi kwa kuwauzia mboga mboga zinazohitajika na mazao mengine yanayotakiwa na mgodi. Shirika hili pia hutoa huduma ya chakula na usafi kwa mgodi wa Tancoal pamoja na wakandarasi wake. MWO pia hutoa huduma za chakula na usafi kwa Mgodi wa Tancoal na wakandarasi wake kwenye maeneo ya mgodi na vituo vya mauzo.

Tancoal na mazingira

Tancoal inaendeleza sera kali na taratibu linapokuja suala la mazingira na inafanya kazi kari­bu na mamlaka zinazohusika ili kuhakikisha shughuli za kam­puni hazidhuru mazingira. Shu­ghuli za uchimbaji zinafanywa kulingana na mipango ya madini ili kuhakikisha kuwa kuna utend­aji kazi mzuri maeneo hayo.

Maji kutoka katika mgodi hud­hibitiwa na maji ya chini na maji ya kwenye mkondo hupimwa ili kuhakikisha kwamba yanaba­kia salama kwa matumizi. Tan­coal ina maabara katika mgodi ambayo inafanya iwe rahisi kuweka udhibiti mkali juu ya usalama wa maji.

Tancoal inatunza miti ambayo hutumiwa katika mipango ya ukarabati na mgodi. Miti pia hutolewa kwa mamlaka mbalim­bali na taasisi mbalimbali kwa ajili ya upandaji katika matukio mbalimbali ili kuhakikisha kwamba mazingira karibu na mgodi ni bora.

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya SabaSaba

Tancoal inashiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya SabaSaba huko Dar es Salaam chini ya mwavuli wa washirika wetu, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Tan­coal inashiriki kikamilifu katika Maonyesho hayo ya biashara ambayo ni nafasi kwa raia kuji­funza zaidi kuhusu shughuli za Makaa ya mawe na Tancoal. Wageni wanaotarajia kufika SabaSaba wanakaribishwa sana kwenye banda letu.