Davis & Shirtliff yaongoza soko la bidhaa za maji na nishati nchini


Davis & Shirtliff yaongoza soko la bidhaa za maji na nishati nchini

Davis & Shirtliff inaamini kuwa bidhaa nzuri ni muhimu kwa kila mafanikio ya kampuni na inajidhatiti kuendelea kuwa wavumbuzi wakiwa na lengo la bidhaa za teknolojia za hali ya juu. Baadhi ya mifano ni pamoja na masuluhisho ya bidhaa za kudhibiti kasi za mabomba ya maji, udhibiti na ufuatiliaji wa mabomba ya maji yaliyo mbali, matibabu ya maji ya njia ya uchujaji (Ultra Filtration), vyombo vya kisasa vya uchujaji na uzalishaji mseto wa nishati ya jua  ambayo pamoja na upanuzi ulioendelea wa bidhaa zake unaipa kampuni hii sifa za hali ya juu.

Davis & Shirtliff hushiriki katika sekta mbalimbali, eneo muhimu zaidi likiwa ni pampu za maji. Kampuni huchukua sampuli kutoka kwa baadhi ya wazalishaji wanaoongoza ulimwenguni ikiwa na zaidi ya sampuli 600 zinazopatikana kwa minajili ya kutoa suluhisho kwa kila mahitaji yanayohusu pampu. Wasambazaji wakubwa wa bidhaa hizi ni pamoja na Grundfos iliyoko Denmark, Pedrollo ya Italia na aina nyingine nyingi za pampu za kampuni aina ya Dayliff, ambazo zote zinatumika na kuheshimiwa sana nchini Tanzania.

Mafanikio ya Davis & Shirtliff yanategemea mambo mengi; tukianzia na bidhaa zenyewe ambazo hutoa thamani na ufanisi wake sokoni zikipewa nguvu na maelezo ya kina ya bidhaa, vipuri vilivyokamilika, msaada wa matengenezo, upatikanaji wa bidhaa, ushauri wa wataalam kutoka kwenye timu ya kampuni ya wahandisi wenye sifa na ujuzi wa mauzo.

Davis & Shirtliff pia husambaza bidhaa mbalimbali zinazohusiana na maji, miongoni mwa bidhaa ambazo zimejizolea umaarufu zaidi ni vifaa vya mabwawa ya kuogelea na vifaa vingine vya ziada. Mtazamo zaidi ukiwa kuwa na bidhaa bora zaidi, bidhaa kama pampu, machujio (filters), vifaa vya kuunganishia, kemikali na vifaa vya kufanyia usafi.

Matibabu ya maji ni shughuli nyingine kubwa inayofanywa na kampuni hii ambapo hutoa bidhaa mbalimbali za kutibu hali mbalimbali za maji ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa mabaki, kuondoa maambukizi ya bakteria, mifumo ya reverse Osmosis, ulainishaji wa maji na matibabu ya maji taka. Thamani uhakikishwa kwa kuchanganya teknolojia ya utengenezaji bidhaa hizo za ndani na teknolojia za hali ya juu kutoka nje ya nchi na kampuni yetu hivi  sasa imeweza kutengeneza aina mbalimbali za vifaa vya matibabu ya maji vilivyo na ubora usiotiliwa shaka katika Ukanda huu.

Kampuni pia imetengeneza misingi bora kwa upande wa sekta ya nishati, likiwa ni eneo la fursa za kimaendeleo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, tukijikita zaidi katika masoko yote ya bidhaa za nishati ya jua na jenereta.

Kutokana na ukweli kwamba bei ya nishati inayotokana na jua imepungua hivi karibuni kwa kiasi kikubwa, hasa Photo Voltaic modules, kumekuwa na ufanisi mkubwa katika matumizi ya jua na kwa kweli kwa kuwa bado kuna changamoto ya kuwa na umeme usio wa kuaminika na viwango vya juu vya upepo wa jua Afrika ni mahali pazuri kwa ajili yake.

Bidhaa hizo zinajumuisha masuluhisho ya aina mbalimbali ya nishati ya jua, mifumo ya kuzalisha nguvu ya nishati ya jua, mifumo saidizi ya umeme, taa za jua na aina mbalimbali za vichemsha maji kwa nishati ya jua. Jenereta pia ni biashara muhimu kwa Davis & Shirtliff zikiuzwa kwa ukubwa kutoka 1 hadi 1000kVA. Kampuni hii kwa sasa inaongoza katika kutoa huduma za bidhaa mbalimbali za suluhisho la nishati nchini Tanzania na Afrika.

Mipango ya hivi karibuni, yote ikiwa inahusiana zaidi na maji ambayo ndiyo biashara kuu, ni umwagiliaji na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya matone, makazi na kilimo zilizoingizwa sokoni. Jambo muhimu hasa limekuwa ni kuanzishwa kwa uhusiano na Kampuni ya Umwagiliaji ya Hunter iliyoko Marekani ambayo ni miongoni mwa viongozi wa dunia katika vifaa vya ujumla vya umwagiliaji.

 Pia, ushirikiano wa hivi karibuni na Kampuni ya Bioliff Water Technologies unakamilisha aina mbalimbali za masuluhisho ya matibabu ya maji taka na uchakataji ili kuchakata maji ya kijivu na meusi kwa viwango vinavyokukubalika.

Davis & Shirtliff inaamini kuwa bidhaa nzuri ni muhimu kwa kila mafanikio ya kampuni na inajidhatiti kuendelea kuwa wavumbuzi wakiwa na lengo la bidhaa za teknolojia za hali ya juu. Baadhi ya mifano ni pamoja na masuluhisho ya bidhaa za kudhibiti kasi za mabomba ya maji, udhibiti na ufuatiliaji wa mabomba ya maji yaliyo mbali, matibabu ya maji ya njia ya uchujaji (Ultra Filtration), vyombo vya kisasa vya uchujaji na uzalishaji mseto wa nishati ya jua  ambayo pamoja na upanuzi ulioendelea wa bidhaa zake unaipa kampuni hii sifa za hali ya juu.

Kampuni pia imejidhatiti kuongeza uwepo wake wa kidijitali kwa mifumo ya ndani na pia kwa kuongeza urahisi wa wateja. Maelezo kamili ya bidhaa pamoja na vifaa vya upimaji, huduma na msaada wa kufunga vipuri hupatikana mtandaoni kupitia tovuti ya www.davisandshirtliff.com na www.dayliff.com na pia hivi sasa kupitia programu ya D & S FLO ambayo  ni application inayopatikana bila malipo kwenye mfumo wa Android kupitia Google Playstore na kwa mfumo wa iOS hupatikana kwenye App Store.

Davis & Shirtliff Tanzania imetoka mbali sana na katika miaka yake 20 ya ufanyaji kazi inajivunia sana mchango mkubwa ambao imeutoa kwa nchi kupitia ushiriki wake katika maendeleo ya sekta muhimu za maji na nishati wakati huu. Ikiwa na wafanyakazi wake wenye utaalam uliotukuka, kampuni hii ipo vizuri pia kwa ajili ya siku zijazo na inatarajia kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.