RAV 4 Adventure 2019 ni gari inayokupa uhuru wa nafsi wakati wa kuitumia


RAV 4 Adventure 2019 ni gari inayokupa uhuru wa nafsi wakati wa kuitumia

Gari hili ni toleo jipya la mwaka 2019 na tulilizindua rasmi Juni mwaka huu. Gari hizi zipo za aina mbili yaani RAV 4 Comfort pamoja na RAV 4 Adventure. Katika aina hizi mbili RAV 4 Adventure ndiyo ina kila kitu ukilinganisha na Comfort.

Teknolojia ni matumizi ya sayansi katika sekta za uzalishaji na sekta nyingine kama vile mawasiliano, hasa hasa kwa madhumuni ya kibiashara. Pia, tunaweza kusema kuwa, teknolojia zinahusisha njia za kisayansi pamoja na bidhaa zinazotumika kukamilisha madhumuni ya viwanda au biashara husika.

Ukuaji wa teknolojia umewezesha watu wengi kupata urahisi katika shughuli mbalimbali ikiwemo uundaji wa magari, kwani magari ya kisasa yamerahisishwa sana tofauti na magari ya zamani.

Ukuaji huu umefanya kampuni zinazotengeneza magari kubuni magari mapya ambayo yanakuja yakiwa na mifumo maalum inayomfanya mtumiaji kuwa katika hali ya kustarehe zaidi ukilinganisha na magari ya zamani.

Kampuni kongwe ya utengenezaji wa magari duniani ya Toyota imeendelea kuutumia vyema ukuaji wa teknolojia kwa kuunda gari la kisasa aina ya RAV 4 toleo jipya la mwaka 2019 lenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.

Gari hilo ambalo limezinduliwa Mwezi Juni mwaka 2019 limeanza kuuzwa kwenye nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

Meneja Msaidizi wa Mauzo wa Kampuni ya Toyota Tanzania, Abbas Simkoko anasema gari hilo limeundwa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ili kuongeza uhuru wa nafsi (Peace of Mind) kwa mtumiaji.

“Gari hili ni toleo jipya la mwaka 2019 na tulilizindua rasmi Juni mwaka huu. Gari hizi zipo za aina mbili yaani RAV 4 Comfort pamoja na RAV 4 Adventure. Katika aina hizi mbili RAV 4 Adventure ndiyo ina kila kitu ukilinganisha na Comfort,” anasema Simkoko.

Anafafanua kuwa, “RAV 4 Adventure ni gari ambalo linatumia lita 7.2 za mafuta kwa kila kilomita 100 kutegemea na aina ya uendeshaji na lina CC 2500, gari hili lina teknolojia inayoitwa Pitch and bounce ambayo inasaidia kupunguza mtikisiko kwa walioko ndani ya gari wakati linapita kwenye barabara yenye mashimo,”

Simkoko anaeleza kuwa, “Uwezo wa utendaji kazi wa injini ya gari hili ni mkubwa ukilinganisha na RAV 4 nyingine. Mfano; ukiwa unaendesha halafu gia ikawa kwenye kitufe cha ECO halafu ukabonyeza kitufe cha SPORTS na ukakanyaga mafuta mwendokasi wa gari unaongezeka na gari linakuwa na nguvu sana.”

Anasema, “RAV 4 Adventure ni gari ambayo ikiwa kwenye drive mode inakuwa kwenye gia 8 lakini ukiamua kubadili gia wewe mwenyewe unaweza kuzishusha zikafika mpaka gia 4 mpaka 5,”

“RAV 4 Adventure ina siti zenye kitambaa cha ngozi (Leather Seat) hivyo wakati mwingine husababisha mtumiaji kutoka jasho anapokuwa amekalia, kwa hivyo ili kuondoa changamoto hiii, RAV 4 Adventure ina mfumo wa kisasa wa kiyoyozi ambao unawamwezesha mtumiaji kuongeza ama kupunguza kiasi cha baridi kwenye siti yake.” Anaeleza Simkoko.

Anaeleza kuwa, “Gari hili lina mfumo ambao unamuwezesha dereva kufanya baadhi ya vitu akiwa kwenye kiti chake wakati wa kuendesha. Gari hii ni Asymmetric four wheel drive kwa sababu lina machaguo (Options) mawili, moja; kama gari imekwama kwenye matope kuna chaguo la mud and sand kwenye dashbodi ambayo ukiiweka inazuia Traction control kufanya kazi ili kuweza kuziruhusu tairi ziweze kuserereka ili utoke kwenye tope ama mchanga kwa urahaisi,”

“Pia, kuna chaguo lingine la rock and dust ambalo unafanya hivyo hivyo ili gari liweze kutembea vizuri kwenye eneo lenye taka ama mawe mawe mengi.  Gari hili likiwa kwenye barabara ya kawaida linakuwa kwenye mfumo wa two wheel drive lakini likiingia kwenye barabara zenye mashimo ama tope linajibadilisha lenyewe na kuwa kwenye mfumo wa four wheel drive,” alieleza Simkoko.

Simkoko anasema kuwa, “RAV 4 Adventure linatofautiana sana na aina nyingine za RAV 4 zilizopo sokoni katika maeneo mengi. Mfano idadi ya gia ambapo RAV 4 Adventure ina gia 8, ina eneo la kufungua na kufunga kwa upande wa juu (Panoramic moon roof), lina sehemu ya kuchajia simu isiyotumia waya (Wireless phone charging) ambayo huchaji simu zenye mfumo wa (Qi),”

Anaongeza kuwa, “Gari hili lina funguo za kisasa ambazo zinakuwezesha kufunga na kufungua gari kwa urahisi, gari hili ni refu kwa kwenda chini ambapo linazuia eneo la chassis kugusa chini kama utapita sehemu yenye mashimo, lina eneo pana kwa ndani ambalo huwawezesha watu kukaa kwa nafasi, lina mfumo wa kisasa wa mneso (Suspension) ambao huwafanya watumiaji kustarehe na kutosikia mtikisiko mkubwa gari linapopita kwenye mashimo.”

Anasema, RAV 4 Adventure ina buti la kisasa ambalo lina kitambuzi (sensor) inayosaidia kulifungua ama kulifunga kwa kusogeza mguu kwenye eneo iliyopo sensor hiyo.

Gari hili lipo kwenye rangi 9 tofauti ambazo ni; Pure White (040), Pearl White (070), Silver Metallic (1D6), Midnight Blue Metallic (8X8), Cyan Metallic (8W9), Urban Khaki (6X3), Gray Metallic (1G3), Attitude Black Metallic (218) pamoja na Red Metallic (3T3).”

Simkoko anasema, “Gari hili ni zuri sana kwa ajili ya matumizi ya mashirika na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali pamoja na watu binafsi, gari hili limezingatia mazingira ya Kitanzania kuanzia barabara mpaka hali ya hewa, kiwango cha ulaji wa mafuta kiko chini hivyo limezingatia uchumi wa mtanzania.”

Anaongeza kuwa, “Kwa sasa RAV 4 Adventure inapatikana sokoni ambapo mteja anatakiwa kufika kwenye maduka na yadi za Toyota popote pale Tanzania kwa ajili ya kujipatia gari hili. Mtu atakaponunua RAV 4 Adventure tunampatia hati ya dhamana (Warrant) ya miaka 3 ama kilomita laki moja (100,000). Pia mteja atapata huduma ya Value+ ambayo itamuwezesha kupata huduma ya matengenezo (Service) bila malipo kwa muda wa miaka au kilomita 75000.

“Kwa kuhitimisha niwaombe Watanzania kutumia gari hiii ili wajionee maana halisi ya mapinduzi na ukuaji wa teknolojia hususani kwenye utengenezaji wa magari. Maeneo yote ambayo magari haya yanapatikana hapa nchini kuna wataalam ambao watampatia mteja muda wa majaribio pamoja na maelekezo ya matumizi ya gari hilo bila gharama yoyote,” alieleza Simkoko.