TUDARCo ni chuo kinachotoa kozi zinazotambulika kitaifa na kimataifa


TUDARCo ni chuo kinachotoa kozi zinazotambulika kitaifa na kimataifa

Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo) ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Makumira na kilianzishwa toka mwaka 2003. TUDARCo ilipatiwa cheti cha usajili kama chuo kikuu rasmi na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) mwaka 2007. Chuo Kimekuwa kikipiga hatua tangu kuanza na wanafunzi 150 miaka ya 2002/2003 kufikia kuwa na wanafunzi zaidi ya 2,000.

Katika dunia ya leo, ili kila mtu aweze kuboresha maisha yake ni lazima awe na elimu. Elimu ndiyo inayo muwezesha mtu kujitambua na kujimiliki yeye mwenyewe, pia kuzikabili changamoto zinazo msonga, kuyatawala na kuyatumia mazingira yanayo mzunguka ili kuboresha maisha yake.

Ili elimu iweze kuleta mabadiliko ya kweli kimaendeleo ni lazima iwe elimu bora ambayo inalenga kumbadilisha mtu nakumuwezesha kufikiri, kubuni, kujitambua, kuhoji, kudadisi, kupenda kazi, kuwa na mwenendo mwema na kuboresha afya na maisha yake binafsi na ya Jamii.

Elimu ni ukombozi iwapo italenga kumpatia mtu uwezo wa kupambana na changamato zinazoikabili jamii na taifa kwa ujumla. upatikanaji wa elimu bora hapa nchini unatokana na uwepo wa taasisi bora za elimu ikiwemo vyuo vikuu.

Chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo) nimoja ya taasisi kubwa za elimu ya juu nchini ambazo zinatoa elimu bora inayomuandaa kijana wa kitanzania kukabiliana na changamoto katika jamii.

Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo) ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Makumira na kilianzishwa toka mwaka 2003. TUDARCo ilipatiwa cheti cha usajili kama chuo kikuu rasmi na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) mwaka 2007. Chuo Kimekuwa kikipiga hatua tangu kuanza na wanafunzi 150 miaka ya 2002/2003 kufikia kuwa na wanafunzi zaidi ya 2,000.

Kabla ya mwaka 2011, TUDARCo hakikuwa na jengo maalumu na kililazimika kupanga na hii ndiyo inayosemekana kuwa ni miongoni mwa changamoto kubwa sana.

Ingawa baadaye TUDARCo ilifanikiwa kumiliki majengo yake yenyewe yaliyopo Mwenge ambapo kwa sasa chuo kinajivunia kuwa na jengo la ghorofa ambalo linaweza kukidhi idadi ya wanafunzi 2,500 katika mkao mmoja. Jengo limesheheni zana za kisasa za kufundishia na kujifunza ukijumuisha studio ya utangazaji.

TUDARCo inatoa kozi zinazotambulika kitaifa na kimataifa kuanzia ngazi ya Shahada za juu hahada za awali, Stashahada, na cheti katika kada mbalimbali za elimu. Zifuatazo ni kozi zinazotolewa hapa TUDARCo:

Kwa ngazi ya cheti, tuna kozi katika taaluma ya:

1.   Sheria (Law)

2.   Uhasibu na Utawala wa Biashara (Accounting and Business Adminstration)

3.   Utunzaji wa Kumbukumbu (Records management)

4.   Christian ministry

Kwa ngazi ya Stashahada tuna kozi katika taaluma ya:

1.   Sheria (law)

2.   Uongozi wa Biashara (Business Admnistration)

3.   Mahusiano Baina ya watu wa Tamaduni Tofauti (Intercultural Relations)

4.   Christian ministry

Kwa ngazi ya Shahada, tuna kozi katika taaluma ya:

1.   Sheria (Laws)

2.   Utawala wa Biashara (Business Adminstration)

3.   Utawala wa Rasilimali Watu (Human Resources Management

4.   Mawasiliano ya Umma (Mass Communication)

5.   Elimu (Education)

6.   Ukutubi na Taaluma ya Habari (library and Information Studies)

7.   Uratibu wa Habari (Information Management)

Wastani upi wa kiwango cha chini cha ufaulu unaohitajika kwa mtu anayetaka kuomba kozi hapo chuoni?

Vigezo vya chini kabisa vya udahili wa wanafunzi kwa ajili ya kozi za shahada za awali zinatolewa na TCU kama ifuatavyo: Kwa ngazi ya degree anatakiwa awe amemaliza kidato cha sita na kupata angalau principal mbili yaani D mbili au awe amemaliza Diploma NTA level 6 yenye GPA ya tatu au diploma daraja la pili.

Je, chuo chenu kinadahili wanafunzi ambao hawana elimu ya kidato cha sita? Na viwango vyake vya udahili vipo vipi?

ndiyo chuo chetu kinadahili wanafaunzi ambao hawajahitimu elimu ya kidato cha sita kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada ikiwa tu mtu huyo amefaulu mitihani yake ya kidato cha nne na sita katika viwango vinavyomruhusu kusoma kozi za ngazi ya Astashahada au Stashahada kama ifuatvyo,

i.    Kwa nga ziya diploma

Mwombaji awe na credit tatu O’Level, Principal moja na subsidiary moja A’level Au awe na cheti kinachoendana na kozi anayoomba kutoka katika chuo kinachotambulika na NACTE au TCU.

ii.   Vigezo kwa ngaziya certificate

-Mwombaji awe na PASS NNE au zaidi O’Level

Je, ni namna gani muombaji anaweza kufanya maombi ya kozi anayoipenda?

Mwombaji anachoweza kufanya ni kupakua fomu ya maombi kutoka katika tovuti yetu (www.tudarco.ac.tz) au anaweza kuomba moja kwa moja mtandaoni kupitia osim. tudarco.ac.tz.

TUDARCO nimiongoni mwa vyuo vikubwa na vikongwe hapa nchini. Je kina ushirikiano na taasisi za ndani na nje vikiwemo vyuo rafiki?

Ndio. TUDARCo ni Moja vyuo vishiriki vya Chuo kikuu chaTUMAINI MAKUMIRA, vingine ni Kilimanjaro Christian Medical College (KCMCo) na Stefano Moshi Memorial University College,

TUDARCo inashirikiana kwa karibu na Chuo cha Turku University of Applied sciences (TUAS) kilichopo Finland, uhusiano huu umeanza toka 2012 wakiwa wameanza na mradi wa maktaba na utunzaji wa kumbukumbu  ikiwa imehusisha vyou nane vya Afriaca na Ulaya. Na mwaka 2017 TUDARCo na TUAS wameanza project nyingine ya kuboresha mbinu za ufundishaji- ikilenga Zaidi katika ufundishaji shirikishi. mafunzo yamekua yakifanyika hapa Tanzania na Finland ambapo walimu na wanafunzi wamekuwa wakishiriki.

Vilevile chuo kinachirikana na Youth International Challenge Shirika linalofadhiliwa na wakanada. Mwezi wa sita mwaka huu wanafunzi sita kutoka hapa chuoni walishinda shilling milioni 7.2 baada ya kushiriki katika mashindano ya kiujasiriamali yanayofadhiliwa na shirika hilo. Mashindano kama haya yanawapa wanafunzi wetu fursa ya kuwa wabunifu na kujifunza kwa matendo yale wanayoyasoma darasani.

Ni vitu gani vinawatofautisha TUDARCO na vyuo vikuu vingine kihuduma?

Kwanza TUDARCo ni chuo cha dini na kinalea wanafunzi katika maadili mema bila ubaguzi wa aina yeyote. Wanafunzi wakiwa hapa TUDARCo wamekuwa wakisaidiwa kwa namna tofauti. Kila mwanafunzi hapa amekabidhishwa kwa washauri wa kitaaluma ambao wanakuwa wanawasaidia katika masuala yote yanayohusu taaluma.

Kwa sasa Tanzania ina azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati unaondeshwa na viwanda. Ni ipi nafasi ya TUDARCO katika kusaidia azma hii?

TUDARCo inajikita katika kuandaa mitaala itakayomsaidia mwanafunzi kuwa mbunifu na kuwa na uwezo wa kutambua nafasi yake katika jamii katika utatuzi wa matatizo yanayomzunguka kwa kutumia teknologia ndogo na inayopatikana katika mazingira anayoishi.