Ushiriki wa Kampuni ya Starpeco katika utekelezaji wa miradi mikubwa nchini


Ushiriki wa Kampuni ya Starpeco katika utekelezaji wa miradi mikubwa nchini

Kampuni ya Starpeco ni kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2006 ikiwa inajishughulisha na uzalishaji wa vilainishi maalum (SWEPCO) na vya kawaida. Mwaka 2008 kampuni ya Starpeco iliingia kwenye uuzaji wa lami na mwaka 2012 ikaanza ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza lami ya maji (Bitumen Emulsion) pamoja na lami ya mafuta (Cutbacks).

Kampuni ya Starpeco ni kampuni ya Kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2006 ikiwa inajishughulisha na uzalishaji wa vilainishi maalum (SWEPCO) na vya kawaida. Mwaka 2008 kampuni ya Starpeco iliingia kwenye uuzaji wa lami na mwaka 2012 ikaanza ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza lami ya maji (Bitumen Emulsion) pamoja na lami ya mafuta (Cutbacks).

Mwaka 2014 kampuni hii iliingia moja kwa moja kwenye biashara ya kuagiza, kuzalisha na kusambaza bidhaa zote za lami. Kampuni hii pia iliungana na kampuni nyingine kwenye biashara ya bidhaa za ukaguzi (Scanner) ambazo zinafanya kazi ya kukagua mizigo na watu hasa bandarini na kwenye viwanja vya ndege.

Pia, mwaka 2008 Starpeco Limited iliagiza maabara ya kisasa OSA (On- SiteOil Analysis) inayotumika kukagua ubora wa mitambo ya magari na viwandani na oil.

OSA inawezesha kujua hali ya oil na mtambo katika muda mfupi na kutoa mapendekezo kipi kifanyike na bila kufungua mtambo husika. OSA inaleta mabadiliko katika utambuzi wa matatizo ya oil na mitambo.

Kampuni hii imekuwa ikifanya kazi na taasisi mbalimbali za Serikali ikiwa ndiyo wadau wao wakuu kwenye upande wa oil na OSA. Miongoni mwa taasisi hizo ni pamoja na GPSA, Wizara mbalimbali, Jeshi la Polisi n.k.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Starpeco Limited, Gratian Nshekanabo anaeleza namna kampuni hii inavyosaidia juhudi za kufikia uchumi wa viwanda kwa kushiriki miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, madaraja, viwanja vya ndege nchini n.k.

Ushiriki wa Starpeco Limited kwenye utekelezaji wa Miradi

“Ushiriki wetu kama Starpeco kwenye utekelezaji wa miradi hii upo kwa njia mbili. Njia ya kwanza ni ushiriki wa moja kwa moja. Njia ya moja kwa moja ni kuzalisha na kusambaza lami ya maji (Bitumen Emulsion) na lami ya mafuta (Cut backs) ambazo zinatumika kwenye utekelezaji wa miradi ya barabara,” anaeleza Nshekanabo.

Anasema, “Tangu tumefungua kiwanda cha kutengeza lami ya maji, (Bitumen Emulsion) na lami ya mafuta (Cut backs), lami hizi zimekuwa zikipatikana hapa nchini kwa ubora wa hali ya juu pamoja na bei nafuu ukilinganisha na zile ambazo zilikuwa zinaagizwa kutoka nje.”

“Kuna miradi mikubwa ambayo tumekuwa tukishiriki moja kwa moja kwa kusambaza lami na vilanishi mitambo. Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja la Mfugale (TAZARA) kuanzia mwanzo mpaka mwisho, ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya Ubungo, mradi wa upanuzi wa barabara ya Morogoro, upanuzi wa barabara ya Bagamoyo, uwanja wa ndege wa Tabora na Chato, ukarabati wa uwanja wa ndege wa KIA, mradi wa ujenzi wa jengo la tatu (Terminal Three) kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na miradi mbalimbali ya barabara,”anasema Nshekanabo.

Anasema, njia nyingine ya ushiriki ni ile isiyo ya moja kwa moja ambapo tunashiriki katika kutoa mafunzo,ushauri wa viwango na udhibiti wa ubora wa bidhaa za lami na vilainishi mitambo. Pia, tumekuwa tukitoa mafunzo ya Petro-Chemical Products kwa vitendo kwa wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo mbalimbali nchini kila mwaka.

Uzoefu ambao Starpeco Imeupata kutokana na kushiriki kwenye miradi hii

“Tumepata uzoefu mkubwa umetusaidia kuongeza imani kwa wateja hasa wakandarasi mbali mbali wa ujenzi. Unaposhiriki kwenye miradi mikubwa kama hii ambayo inatekelezwa na wakandarasi kutoka nje kama vile mradi wa daraja Mfugale, tulivyomaliza kazi walitupatia cheti cha huduma (Certificate of Service) ambacho kimeongeza sifa na hadhi ya kampuni yetu” anasema Nshekanabo.

Anasema kuwa, “Pia ushiriki kwenye miradi hii unapata nafasi ya kufahamika kwenye mataifa ambayo wakandarasi wanatoka kwasababu kampuni zile zikifika kwao zinasema kwamba Tanzania kuna kampuni fulani mbayo ndiyo iliyokuwa ikitusambazia Lami hivyo inakuwa rahisikuaminika na kupata kazi nyingine kubwa”

Sababu ya Starpeco kuaminika katika utekelezaji wa miradi hii

Nshekanabo anasema, “Sababu kubwa inatokana na mtazamo wa kampuni hii kwa sababu kama kampuni tumekuwa na mtazamo wa kutaka kufika kiwango cha juu kwa kila tunachokifanya. Hivyo katika kulitekeleza hili tumekuwa tukihakikisha kila tunachokifanya tunakifanya kwa weledi, uaminifu na ubora wa hali ya juu.”Hata Kauli Mbiu yetu ni “Reliability, our way of life” kuamimika ndiyo Maisha yetu

“Kingine ni ubora wa bidhaa na huduma zetu, teknolojia tunazotumia katika uzalishaji wa bidhaa zetu vinaleta utofauti na mabadiliko chanya katika utendaji wa kazi,” anasema Nshekanabo.

Changamoto katika ushiriki kwenye miradi

“Changamoto ziko nyingi lakini changamoto kubwa ni ucheleweshwaji wa malipo. Wakati mwingine wakandarasi wanachelewa kulipwa hivyo na wao huchelewa kutulipa. Nyingine ni kutozingatia muda kwa baadhi ya mamlaka za usimamizi, mfano; muda mrefu katika kupata cheti au vibali vya uthibitisho wa ubora, hali hii inachelewesha kasi ya kufanya biashara na uwekezaji,” anasema Nshekanabo.

Mikakati ya Starpeco Limited

“Mkakati mkubwa ni kuongeza nguvu katika teknolojia pamoja na kuangalia namna dunia inavyokwenda kwenye nyanja ya teknolojia, mfano; Tanzania inatarajia kuanza matumizi ya lami ngumu (Superpave Performance Grade) hivyo na sisi tuko kwenye mpango wa kuanza kuwekeza katika utengenezaji wa lami hii,” anasema Nshekanabo.

Anaongeza kuwa, “Tunataraja kushirikiana na kampuni mbalimbali kutoka nje, kuleta bidhaa mpya na aina mbalimbali za lami ambazo ni rafiki wa mazingira, imara na za bei nafuu kama Bitumen Emulsion ambayo tunaizalisha sasa.”