MoCU ni Chuo pekee kinachotoa huduma za elimu na ushauri wa kitaalamu katika masuala ya ushirika nchini


MoCU ni Chuo pekee kinachotoa huduma za elimu na ushauri wa kitaalamu katika masuala ya ushirika nchini

Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kimetokana na kupandishwa hadhi kwa kilichokuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi. Kihistoria,kilianzishwa rasmi kwa Sheria ya Bunge Namba 32 ya mwaka 1964 (iliyofutwa) kama Chuo cha Ushirika Moshi. Mwaka 2004 Chuo cha Ushirika Moshi kilipandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi (MUCCoBS) chini ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kimetokana na kupandishwa hadhi kwa kilichokuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi.

Kihistoria,kilianzishwa rasmi kwa Sheria ya Bunge Namba 32 ya mwaka 1964 (iliyofutwa) kama Chuo cha Ushirika Moshi.

Mwaka 2004 Chuo cha Ushirika Moshi kilipandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi (MUCCoBS) chini ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

Mwaka 2014, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi kilipandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU). Chuo hiki ni miongoni mwa vyuo vikuu vya umma vilivyo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kina Kampasi kuu iliyopo katika Manispaa ya Moshi na Kituo cha Kufundishia cha Kizumbi, Shinyanga.  Vilevile Chuo kina ofisi 13 ambazo hutoa huduma za elimu na ushauri wa kitaalamu katika masuala ya ushirika katika mikoa yote nchini.

Ofisi hizi ziko katika mikoa ya Kilimanjaro (hutoa huduma mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara), Pwani (hutoa huduma mikoa ya Pwani, Dar-es-Salaam na Visiwa vya Unguja na Pemba), Shinyanga (hutoa huduma mikoa ya Shinyanga na Simiyu),  Dodoma (hutoa huduma mikoa ya Dodoma na Morogoro), Iringa (hutoa huduma mikoa ya Iringa na Njombe), Mwanza (hutoa huduma mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera), Mbeya (hutoa huduma mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi) na Mtwara (hutoa huduma mikoa ya Mtwara na Lindi), Tanga, Singida, Ruvuma, Tabora na Kigoma.

MoCU ina vitivo viwili ambavyo ni  kitivo cha  Ushirika na Maendeleo ya Jamii (Faculty of Co-operative and Community Development), na Kitivo cha Biashara na Sayansi za Mawasiliano (Faculty of Business and Information Sciences) Pia kuna Taasisi ya Elimu Endelevu ya Ushirika (Institute of Continuing Co-operative Education), Kurugenzi ya Utafiti na Mafunzo ya Uzamili (Directorate of Research and Postgraduate Studies).

Kurugenzi ya Mafunzo ya Shahada za Kwanza (Directorate of Undergraduate Studies),Kurugenzi ya Huduma za Ushauri (Bureau of Consultancy Services) na Maktaba ya Ushirika  na Nyaraka za Kale (Co-operative Library and Archives).

Kurugenzi za Utawala ni Menejimenti ya Rasilimali watu na Utawala (Human Resource Management and Administration) na Mipango na Fedha (Planning and Finance).

Majukumu makuu ya chuo

Majukumu makuu ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ni

Kutoa mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya astashahada, stashahada na shahada za awali na shahada za uzamili. Vile vile kutoa mafunzo ya muda mfupi katika sekta ya ushirika na biashara;

Kufanya utafiti katika maendeleo ya ushirika na biashara kwa kuzingatia mbinu shirikishi;

Kuandika vitabu na majarida yanayohusu maendeleo ya ushirika na biashara na kuhakikisha kwamba yanawafikia walengwa;

Kutoa huduma za ushauri unaohusiana na maendeleo ya ushirika na biashara kwa wadau wa ushirika, asasi za biashara na watu binafsi; na

Kuchapisha matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanyika kwa matumizi ya jamii ili kujenga uchumi na kupunguza umaskini.

 Programu zinazotolewa na Chuo kikuu cha Ushirika Moshi

a. Certificate Programmes (Astashahada) (Mwaka mmoja)

·       Certificate in Accounting and Finance

·       Certificate in Coffee Quality and Trade

·       Certificate in Enterprise Development

·       Certificate in Management and Accounting

·       Certificate in Microfinance Management

·       Certificate in Information Technology

·       Certificate in Human Resource Management

·       Certificate in Library and Information Sciences

Applicants should be form four certificate holders with at least four passes at d grade and above

b. Diploma Programmes (Stashahada) (Miaka miwili)

Diploma in Co-operative Management and Accounting

Diploma in Microfinance Management

Diploma in Enterprise Management

Diploma in Library and Archival Studies

Diploma in Business Information and Communication Technology

Applicants should be form six leavers with at least one pass and a subsidiary or holders of relevant one year or more certificate qualifications from any accredited academic institution

c.  Bachelor Degree (Shahada ya Kwanza) (Miaka mitatu)

·       Bachelor of Arts in Accounting and Finance

·       Bachelor of Arts in Business Economics

·       Bachelor of Arts in Co-operative Management and Accounting – (Fulltime and Evening)

·       Bachelor of Arts in Community Economic Development

·       Bachelor of Arts in Human Resource Management

·       Bachelor of Arts in Marketing and Entrepreneurship

·       Bachelor of Arts in Microfinance and Enterprise Development

·       Bachelor of Arts in Procurement and Supply Management

·       Bachelor of Science in Business Information and Communication Technology

·       Bachelor of Laws

Applicants should be form six leavers with two principal passes from two relevant subjects with a total of 4.0 points or diploma of at least 3.0 GPA verified by NACTE.

d. Postgraduate Diploma (Stashahada ya Uzamili)(Mwaka mmoja)

·       Postgraduate Diploma in Accounting and Finance – (Fulltime and Evening)

·       Postgraduate Diploma in Community Development – (Fulltime and Evening)

·       Postgraduate Diploma in Co-operative Business Management – (Fulltime and Evening)

·       Postgraduate Diploma in Savings and Credit Co-operative Societies Management – (Fulltime, Evening and Distance)

Applicants should possess relevant advanced diploma or bachelor degree from a recognized institution

e. Master’s Degree (Shahada ya Umahiri) (Miaka miwili)

Master of Arts in Co-operative and Community Development – (Fulltime and Evening)

Master of Arts in Procurement and Supply Management

Master of Business Management – (Fulltime and Evening)

Applicants should have at least second class bachelor degree or postgraduate diploma from a recognized institution

f.  Doctor of Philosophy (PhD) (By Research only) (Shahada ya Uzamivu)

Applicants should possess relevant Masters Degree

g. Distance learning programmes (Programmu za Masafa)

·       Foundation Certificate in Savings and Credit Co-operative Management

·       Professional Certificate in Savings and Credit Co-operative Management

·       Programu ya Utunzaji wa Vitabu vya Hesabu za Vyama vya Ushirika vya Msingi

·       Programu ya Ushirika, Uongozi na UsimamiziwaVyama vya Ushirika

·       Programu ya Menejimenti Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo.