Benki ya Uchumi yatoa gawio la asilimia 8 kwa wanahisa

Benki ya Uchumi yatoa gawio la asilimia 8 kwa wanahisa

Benki ya Uchumi imetoa gawio la asilimia 8 sawa na Shs 80 kwa kila hisa kwa wanahisa wake ikiwa ni sehemu ya faida ya benki hiyo kwa mwaka 2019.

Benki ya Uchumi imetoa gawio la asilimia 8 sawa na Shs 80 kwa kila hisa kwa wanahisa wake ikiwa ni sehemu ya faida ya benki hiyo kwa mwaka 2019.

Akizungumza ofisini kwake, Meneja Mkuu wa benki ya Uchumi, Angela Moshi amesema benki imetoa gawio hilo kutokana na ongezeko la faida kwa mwaka 2018 kufikia Shs 709 million ukilinganisha na Shs 474 million kwa mwaka 2017 ambayo ni ongezeko la asilimia 49.5.

Aidha Meneja Mkuu huyo amesema kuwa, wanahisa wamepitisha gawio la asilimia 8 kwa mwaka huu ukilinganisha na gawio la asilimia 7 kwa mwaka jana.