TYC inavyoadhimisha siku ya kimataifa ya vijana mwaka 2019


TYC inavyoadhimisha siku ya kimataifa ya vijana mwaka 2019

Siku ya kimataifa ya vijana ni siku maalum iliyobuniwa na kuaanzishwa na Umoja wa Mataifa (UN) mnamo miaka ya 1999 na kuanza rasmi kuadhimishwa tarehe 12 mwezi wa nane 2000, lengo kuu la siku ya kimataifa ya vijana ni  kutoa fursa kwa Serikali na wadau wengine  kuvutia na kuyatilia maanan maswala mbalimbali ya kimaendeleo yanayo wagusa vijana duniani.

Tanzania Youth Coalition (TYC) ni shirika la vijana lisilo la kiserikali lenye lengo la kuhakikisha sauti ya kijana inasikika katika majukwaa ya utoaji maamuzi na sera katika ngazi ya kata, wilaya, taifa na kimataifa.

TYC inawezesha usambazaji, upatikanaji na ubadilishanaji wa taarifa, uchambuzi wa sera, mafunzo kwa vijana, ushawishi na utetezi wa masuala ya vijana katika sera.

Kwa miaka mingi shirika la vijana TYC limekua likiwawezesha na kuwajengea uwezo vijana ili waweze kushiki kikamamilifu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika nyanja za uchumi, siasa na kijamii kupitia program na miradi mbalimbali yenye kujumuisha utolewaji wa elimu, maarifa na taarifa kwa vijana.

TYC inafanya kazi katika maeneo makuu matano ambayo ni kuwezesha vijana kupata ajira na kipato, upatikanaji wa kipato kwa vijana kutoka rasilimali za kimazingira, afya ya kijana na ujinsia, uongozi wa vijana na kujenga demokrasia.

Siku ya kimataifa ya vijana

Siku ya kimataifa ya vijana ni siku maalum iliyobuniwa na kuaanzishwa na Umoja wa Mataifa (UN) mnamo miaka ya 1999 na kuanza rasmi kuadhimishwa tarehe 12 mwezi wa nane 2000, lengo kuu la siku ya kimataifa ya vijana ni  kutoa fursa kwa Serikali na wadau wengine  kuvutia na kuyatilia maanan maswala mbalimbali ya kimaendeleo yanayo wagusa vijana duniani.

Kuelekea siku ya kimataifa ya Vijana nini mchango wa TYC kwenye kuleta mabadiliko ya kielimu nchini

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Vijana iliyobeba kauli mbiu ya mabadiliko ya kielimu, TYC kama shirika lisilo la kiserekali limekuwa na mchango mkubwa kwa jamii ya Tanzania kuelekea siku hii ya kimataifa kutokana na utekelezaji wa program mbali mbali za kimaendeleo hususan zile zinazowahusu vijana pamoja na utoaji wa  taarifa zakimaendeleo kwa vijana.

TYC imekuwa ikitekeleza miradi na programu mbalimbali katika Nyanja tofautitofauti kwa lengo kubwa la kuwajengea uwezo vijana lakini pia kutoa taarifa kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Katika kipindi cha miaka ya 2018 na 2019 TYC imefanya programu mbalimbali ambazo zimekua zikichangia katika maendeleo ya vijana hasa katika eneo la utolewaji wa taarifa, maarifa na elimu.

Miongoni mwa shughuli hizo ni pamoja na kuandaa kambi maalum ya shule yaani (school camping) zinazofanya programu za mabadilishano ya vijana kutoka nchini Tanzania, Kenya na Rwanda pamoja na nchi za Ulaya ikiwemo Ujerumani, Uingereza, Denmark na Urusi. Kambi hii pia imelenga kujadili kwa kina faida zitokazazo na programu za vijana katika mashule kama shughuli za ziada kwa wanafunzi ili kuweza kuwajengea uwezo wanafunzi lakini pia kuwapa wanafunzi na walimu fursa ya kubadilishana uzoefu ili kuweza kuboresha programu hizi za mabadilishano ya vijana.

TYC kama asasi ya kiraia inayofanya kazi na vijan pia ilifanya utafiti mdogo katika mikoa 11 ya Tanzania bara na Zanzibar katika shule na mashirika yanayofanya Programu za Mabadilishano baina ya nchi ya Tanzania, Ujerumani na nchi nyingine barani ulaya kwa lengo la kutambua changamoto, uzoefu na mbinu bora za mabadilishano ili kuboresha na kuleta tija si tu kwa vijana washiriki bali pia kwa jamii zinazowanzunguka.

Mbali na hayo TYC kama shirika linafanya kazi kubwa ya kuwakutanisha vijana waleta mabadliko kutoka Tanzania, nchi za Afrika Mashariki pamoja na Sudani ili kutambua mchango wa vijana katika utekelezaji wa maendeleo endelevu ya duniani (SDG’s) ambako ujumuishwaji na utolewaji wa elimu bora, usawa wa kijinsia na udumishaji wa amani ni mambo yanayojadiliwa kwa kiasi kikubwa.

Katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo endelevu duniani TYC kama shirika pia imekuwa ikitekeleza program maalum kwa vijana na wanawake ijulikanayo kwa jina la wypre, program hii, kama zilivyo program nyingine zinazotekelezwa na TYC inalenga zaidi katika kuongeza ushiriki wa vijana na wanawakeKatika maswala ya uongozi na maswala ya kidemokrasia kwa ujumla.

Katika eneo hili la utekelezaji TYC  ikishirikiana  na wadau TAWLA na WE EFFECT imefanikiwa kuandaa mtaala maalum wa elimu ya uraia nakutoa mafunzo ya elimu ya uraia kwa vijana,na wanawake zaidi ya elfu tatu (3000)  katika wilaya nne za mkoa wa tanga zikiwemo Muheza, Korogwe, Handeni na Lushoto  ili kuweza kuzitambua haki zao za msingi ikiwemo kupiga na kupigiwa kura.

Mchango wa Serikali katika kuleta mabadiliko ya kielimu nchini

Sote tunafahamu kuwa jukumu la kuleta mabadiliko chanya ya aina yoyote ile situ jukumu la upande mmoja  bali ni kazi shirikishi ambayo ili ifanyike kwa ufasaha basi Serikali, mashirika binafsi, na wadau mbalimbali hawana budi kushirikiana kwenye kulifikia jambo hilo.

Serikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi kama TYC na mengineyo imekuwa ikifanya jitihada mbali mbali ili kuleta maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali ikiwemi sekta ya elimu kwa kuanzisha mikakati mbali mbali kama mkukuta, dira ya maendeleo ya taifa n.k.

Serikali ya Tanzania ilianzisha dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 ambayo ilianzwa kutekelezwa mwaka 2000 ili kuongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha   Tanzania kufikia hadhi ya nchi zenye kipato cha kati na kuondokana na umasikini uliokithiri kufikia mwaka 2025.

Kama tunakumbuka vizuli kuwa Katika dira ya maendeleo ya taifa 2025 kulikuwa na malengo matano ambayo yalo ainishwa ili yaweze kufikiwa ifikapo 2025, malengo hayo ni: kuboresha hali ya maisha ya watanzania, kuwepo kwa mazingira ya amani, usalama na umoja, Kujenga utawala bora, kuwepo jamii iliyo elimika vema na inayojifunza pamoja na Kujenga uchumi imara unaoweza kukabiliana na ushindani kutoka nchi nyingine.

Ili kutimiza malengo hayo, Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuboresha viashiria muhimu vya uchumi kama vile kuchochea ukuaji wa pato lataifa, kushusha mfumuko wa bei, kuvutia wawekezaji kutoka nje, kupunguza ukosefu wa ajira pamoja na kuendeleza secta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Mkukuta

Ili kufikia malengo ya kimaendeleo ya nchi ikiwemo mabadiliko ya kielimu ambayo ndio kauli mbiu ya mwaka katika siku ya kimataifa ya kijana, serikali iliandaa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini, ili kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na pia kuweza kufikia Malengo ya Millennia ambayo ni malengo yaliyokubalika kimataifa kwa ajili yakupunguzaumaskini.  Mkakati huu umegusa masuala yote muhimu kama vile elimu, afya, ajira, makazi, mazingira na usawa wa kijinsia.

Mkakati wa tekeleza sasa kwa matokeo makubwa

Kwa kutambua umuhimu wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi, programu na mikakati ya maendeleo, sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Serikali kupitia wizara mbalimbali imeweka mkakati mpya uitwao ‘Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa’ ambao umejikita katika kuchambua kwa kina programu na miradi ya kipaumbele iliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, ambao umelenga katika kuainisha maeneo machache yatakayoweza kuleta matokeo makubwa kwa haraka ifikapo mwaka 2025.

Serikali imechagua sekta muhimu sita, ambazo zitaanza kutumia mfumo huo mpya ambazo ni kilimo, nishati, elimu, upatikanaji wa rasilimali fedha nausafiri.

Mikakati hii yote inayofanywa na serekali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserekali inafanywa kwa makusudi ili kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 yanafikiwa ikiwemo mabadiliko ya kielimu ambayo ndio yamebeba kauli mbiu ya mwaka katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kijana duniani.

Tembelea Tovuti yetu;  www.tzyc.org

Tuandikie maoni yako kupitia barua pepe zetu: [email protected] na [email protected]

Kurasa zetu za mitandao ya kijamii: Tanzania Youth Coalition