Kifahamu Chuo cha Ardhi Morogoro na kozi kinazotoa

Chuo kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia mpango mkakati wake ambao umejikita katika maeneo ya kuongeza udahili wa wanafunzi, kuboresha taaluma, kufanya mapitio ya mara kwa mara ya mitaala, kutoa mafunzo ya muda mfupi, kuendeleza wafanyakazi kitaaluma, kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na kuanzisha kozi mpya ili kuendana na mahitaji ya wataalamu katika Taifa letu.

Chuo cha Ardhi Morogoro kilianza mwaka 1978 kwa Sheria ya Bunge Na. 35 ya Chuo cha Ardhi ya mwaka 1974, kikiwa tawi la Chuo cha Ardhi kilichokuwa Dar-es-Salaam kwa lengo la kutoa elimu ya taaluma ya ardhi, kutoa huduma kwa jamii na kufanya tafiti.

Chuo kimeendelea kufanya maboresho katika kozi na mitaala kukabiliana na changamoto za kiteknolojia na mahitaji ya soko.

Chuo cha Ardhi Morogoro kinao usajili kamili (Full Registration) pamoja na ithibati kamili (Full accreditation) ya Baraza la Taifa la Elimu a Ufundi yaani ‘NACTE’.

Usajili huu na ithibati vinakifanya Chuo kuwa na uwezo wa kujipanua kwa kuanzisha kozi mbalimbali zenye tija kwa Taifa na jamii kwa ujumla.

Chuo kinatoa mafunzo katika fani ya Upimaji Ardhi “Geomatics” na Mipango Miji “Urban and Regional Planning” kwa kutumia mitaala inayozingatia zaidi utendaji kazi mahili yaani “Competence-Based Curricula” chini ya “NACTE”.

Chuo kinafanya miradi mbalimbali ya Upimaji Ardhi katika Halmashauri mbalimbali za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya.

Kwa sasa Chuo kinaendelea na miradi ya Urasimishaji Makazi katika Halmashauri za Jiji la Dar es salaam, Arusha na Manispaa ya Morogoro, Iringa na Moshi.

Kwa mwaka huu wa masomo 2019/2020 Chuo cha Ardhi Morogoro kina nafasi na kinakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo katika fani mbalimbali za Ardhi kama ifuatavyo:

Astashahada ya Awali ya Upimaji Ardhi na Mipango Miji (Basic Technician Certificate in Geomatics/Urban and Regional Planning) – NTA LEVEL 4, mwaka mmoja.

Stashahada ya Upimaji Ardhi na Mipango Miji (Technician Diploma in Geomatics/ Urban and Regional Planning) – NTA LEVEL (5-6) miaka miwili.

Sifa za mwombaji: -

Astashahada ya Awali ya Upimaji Ardhi: Awe amefaulu kidato cha nne (4) angalau kiwango cha alama ya ‘‘D’’ katika masomo ya Fizikia au Hisabati, Jiografia na Kiingereza.

Diploma ya Upimaji Ardhi: Awe amemaliza kidato cha sita (6) na kufaulu angalau kiwango cha alama ya (Principle pass) ‘‘E’’ katika Hisabati (Advanced Mathematics) na kiwango cha alama ya (Subsidiary pass) ‘‘S’’ katika Fizikia au Jiografia; au awe na Astashahada ya Awali ya Upimaji Ardhi; au Astashahada/Stashahada ya kozi zinginezo zinazotambuliwa na NACTE zinazoshabihiana na masomo ya Upimaji na Ramani.

Astashahada ya Awali ya Mipango Miji: Awe amefaulu kidato cha nne (4) angalau kiwango cha alama ya ‘‘D’’ katika masomo manne miongoni mwa yafuatgayo: Fizikia, Hisabati, Jiografia, Kingereza, kemia, bailolojia, biashara na historia.

Diploma ya Mipango miji na vijiji: Awe amemaliza kidato cha sita (6) na kufaulu angalau Principle pass ‘‘E’’ katika masomo yoyote ya sayansi au awe na Astashahada ya Awali ya Upimaji Ardhi, uchoraji ramani, uhandisi majengo, uhandisi madini, uhandisi wa mazingira au au Astashahada/Stashahada ya kozi zinginezo zinazotambuliwa na NACTE zinazoshabihiana na masomo ya Upimaji na Ramani.

Gharama za fomu: - Gharama ya fomu ya kujiunga na Chuo ni TSh. 10,000/=.

taratibu za kuomba nafasi

Jaza Fomu ya Maombi ya Kujiunga na Chuo inayopatikana Chuo cha Ardhi Morogoro; Ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dar es Salaam na Dodoma na Tovuti ya Chuo www.arimo.ac.tz.

Tuma Fomu ya Maombi ya Kujiunga na Chuo kupitia anwani ifuatayo:

Mkuu wa Chuo,

Chuo cha Ardhi Morogoro,

S.L.P 155,

Morogoro

Au baruapepe:  [email protected]

Muda wa kutuma maombi: Kuanzia tarehe 15.05.2019 – 08.09.2019

Tarehe ya kufungua chuo: Tarehe 14.10.2019

KWA MAWASILIANAO: piga Simu 0784 538 338 (Kaimu Mrajisi), 0768 589 994 (Kaimu Mkuu wa Idara ya Spatial Planning and Management) na 023 2603061 (Simu ya Ofisi).