Chuo Kikuu cha Iringa fahari ya vyuo vikuu binafsi Tanzania


Chuo Kikuu cha Iringa fahari ya vyuo vikuu binafsi Tanzania

Mnamo tarehe 30 Desemba mwaka 1997, historia ya vyuo vikuu binafsi nchini ilianza kuandikwa pale Kihesa mkoani Iringa, baada ya Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini Iringa) kusajiliwa na kuwa Chuo Kikuu binafsi cha kwanza nchini Tanzania.

Mnamo tarehe 30 Desemba mwaka 1997, historia ya vyuo vikuu binafsi nchini ilianza kuandikwa pale Kihesa mkoani Iringa, baada ya Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini Iringa) kusajiliwa na kuwa Chuo Kikuu binafsi cha kwanza nchini Tanzania.

Chuo hiki kilianzishwa mwaka 1993 wakati huo kilijulikana kama Chuo cha Kilutheri Iringa, huku kikitoa Stashahada ya Theolojia na Stashahada ya Juu ya Utawala wa Biashara.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Ndelilio Urio ame-liambia gazeti hili kuwa, mwaka 1997 Chuo kilibadilishwa jina na kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Tumaini, kabla ya kupanda had-hi kutoka Chuo Kikuu Kishiriki kuwa Chuo Kikuu kamili mnamo mwaka 2013, na kuanzia hapo kikaitwa Chuo Kikuu cha Iringa. Chuo Kikuu cha Iringa ambacho kina vitivo sita sasa, kimeweka rekodi kubwa katika kutoa elimu bora, pamoja na kuandaa viongozi na wataalamu bora wa kada mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika ustawi wa maendeleo ya nchi ya Tanzania.

Prof. Urio anasema vitivo hivyo ni pamoja na Kitivo cha Theolojia, Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii, Kitivo cha Say-ansi na Elimu, Kitivo cha Biasha-ra na Uchumi, Kitivo cha Sheria na Kitivo cha Saikolojia. “Chuo hiki kimetunukiwa cheti cha Baraza la Ithibati la Elimu ya Juu (HEAC), ndiyo maana kinatoa mafunzo ya ngazi zote kuanzia Astasha-hada, Stashahada, Shahada ya Kwanza na Shahada ya Uzamili,” anasema Prof Urio.

Mhadhiri Mkongwe na mwan-zilishi wa Idara ya Uandishi wa Habari, Essau Ntabindi ame-liambia gazeti hili kuwa, Chuo Kikuu cha Iringa kimekuwa ni Chuo cha kwanza kutoa shahada ya Uandishi wa Habari (Bache-lor of Arts in Journalism) nchini Tanzania.

Shahada hiyo ime-anzishwa mnamo mwaka 1997. “Sisi ndiyo wa kwanza kutoa Shahada ya Uandishi wa habari hapa Tanzania, wakati huo vyuo vingine vyote vya uandishi wa habari nchini vilikuwa vikitoa elimu kwa kiwango cha Astasha-hada, Stashahada na Stashaha-da ya Juu ya uandishi wa habari, na siyo shahada,” Anafafanua zaidi Ntabindi.

Chuo hiki kinajivunia mbinu bora kabisa za ufundishaji na utafiti kwa kutoa wahitimu walio bora kabisa, ambao wamepata mafanikio makubwa ya ajira pindi tu wanapomaliza na kuhimili soko lenye ushin-dani mkubwa wa ajira nchini.Mkuu wa Idara ya Uandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha Iringa, Aloyce Geofrey anabaini-sha, “Mtangazaji nguli wa radio na televisheni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe maarufu ‘Double G’, na miamba wengine wa tasnia ya habari hususan wahariri wengi wa magazeti wame-soma hapa.”

Akizungumza kwa kujiamini, Geofrey ameongeza kuwa aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Seri-kali, Asah Mwambene, Mhe. Mbunge Amina Mollel, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msa-lala, Simon Berege, Watangazaji wa TCB kama Anna Mwasyoke, Oscar Urasa, Esero Mafuru na wengine wengi, ni hazina iliyopikwa vizuri katika mikono hodari ya Idara ya Uandishi wa Habari ya Chuo hiki.

Mkuu huyo ameongeza kuwa, idara yake imeimarisha vizuri uwanja wake wa mafunzo kwa kujenga radio ya kisasa kabisa Hope FM 98.0, televisheni ya kisasa UoI TV na magazeti ya The Campus Eye na Iringa Kwetu kama sehemu ya mafunzo kwa Vitendo. Katika kipindi cha miaka kumi sasa, Chuo kimeanzisha safari ya kuwa Chuo Kikuu cha uja-siriamali. Hii inaongozwa na maono na dira inayosema “To become a Centre of Excellence for training Competent, Competitive, Ethical, Spiritual and Entrepreneurial Leaders and for Quality Research and Public Service of a third generation University,” hivyo kukifanya Chuo hiki kuwa cha pekee ambacho kinatoa mafunzo ya namna hii katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki.Katika kufikia dira hiyo, Chuo kimeanzisha Kituo cha Ujasiriamali na Uvumbuzi yaani “Centre for Entrepreneurship and Innovation” (CEI) kwa lengo la kukuza ujasiriamali katika programu zote za elimu chuoni hapo, pamoja na kubadili mtazamo wa jamii kuhusu mambo ya ujasiria-mali hususan katika Nyanda za Juu Kusini.

Sambamba na hilo, ndani ya kituo cha ujasiriamali ipo atamizi inaitwa “Kiota Hub”. Hapa wanafunzi na wajasiria-mali kutoka sehemu mbalimbali ya nchi hukutana na kubadilis-hana uzoefu katika mambo ya ujasiriamali. Kupitia atamizi hii, vijana wengi wamefanikiwa kupata uzoefu na ushauri wa kibiashara hivyo kupata mafanikio makubwa katika biashara zao. Aidha, kituo cha ujasiriamali kimeanzisha program mpya iju-likanayo kama ‘Team Academy’ ambayo inatumia mbinu na teknolojia ya kisasa kufundisha ujasiriamali kwa vitendo huku wakiongozwa na wakufunzi ambao wamebobea katika ujasiriamali.

“Kwa njia hii, Chuo Kikuu cha Iringa kimeonyesha njia katika nchi yetu kwa kuifanya elimu ya ujasiriamali kwa vitendo. Tuna-taka kuwa namba moja Afrika kwa kujitofautisha na vyuo vingine ili kuwajenga wanafunzi wetu kuwa na ujuzi, maarifa ya kiteknolojia na ubunifu katika ujasiliamali,” alisema Deo Sabokwigna, Mratibu wa pro-gramu hiyo.Kwa upande wa Kitivo cha Saikolojia, kitivo hiki kinafundi-sha kozi za ushauri nasihi kuanzia ngazi ya cheti mpaka Sha-hada ya Uzamili kikiongozwa na wahadhiri waliobobea katika masuala ya saikolojia. Kitivo hiki pia kina kituo cha mafunzo visiwani Zanzibar.Kitivo kimejenga maabara maalumu ya ushauri, (Special Laboratory and Therapy Rooms) na kukifanya Chuo pekee Afrika Mashari kuwa na maabara ya ushauri.

Ukifika chuoni hapo, utaona maabara hizi zikitumika kufundishia wanafunzi kwa nad-haria na vitendo, ili kuwaandaa kuwa washauri na wanasaikolo-jia waliobobea katika nyanja hizo.Wataalamu hawa wanaandal-iwa kwa ajili ya kutoa huduma za jamii katika maeneo mbalimbali kama vile vitengo vya ustawi wa jamii, shule za msingi na sekondari, vyuo vikuu, dawati la jinsia, magereza, jeshini na hata hospitalini. Nayo Idara ya Anthropolojia na Utalii imewekwa kwenye mpango wa serikali wa kutangaza na kukuza utalii wa Nyanda za Juu Kusini kupitia programu ya Karibu Kusini, chini ya mradi wa Fahari Yetu.

“Wahitimu wengi wa idara hii wameaminiwa na serikali na hata kushika nyadhifa kubwa kabisa katika Wizara ya Utalii na bodi ya utalii, na wengine wakifanya kazi katika makam-puni makubwa ya utalii nchini Tanzania,” anasema Mkuu wa Idara hiyo, Jimson Sanga. Chuo hiki kinatoa jumla ya Shahada 15 bora kabisa nchini Tanzania kama zinavyoonekana katika tangazo lake.