Wataalam wa fedha Afrika Mashariki wanavyokimbizana na teknolojia, watahadharisha


Wataalam wa fedha Afrika Mashariki wanavyokimbizana na teknolojia, watahadharisha

“Ni muhimu na zinarahisisha maisha lakini zinakuja na changamoto, tunatakiwa kuchukua tahadhari.” Huu ni ujumbe ambao baadhi ya wataalam wa benki na huduma nyingine za fedha waliutoa katika mkutano wao wa mwaka uliomalizika wiki iliyopita.

Arusha. “Ni muhimu na zinarahisisha maisha lakini zinakuja na changamoto, tunatakiwa kuchukua tahadhari.” Huu ni ujumbe ambao baadhi ya wataalam wa benki na huduma nyingine za fedha waliutoa katika mkutano wao wa mwaka uliomalizika wiki iliyopita.

Mkutano huu wa 19 ulikusanya takriban wataalam 100 wanaotoka benki na taasisi zingine za fedha za Afrika Mashariki ili kujadili umuhimu wa kuzingatia maadili ya utoaji huduma katika ambao mifumo ya kidigitali imeenea katika taasisi za fedha.

Licha ya kurahisisha utoaji huduma na kuongeza ufanisi, mifumo hiyo imekuja na changamoto kadhaa ikiwemo wizi wa kim-tandao, kuingiliwa kwa faragha za wateja pamoja na uhuishaji wa sheria na kanuni maalum za kusimamia mifumo ya kidigitali ambayo inaongezeka kila kukicha.

Makampuni ya kiteknolojia yanajitahidi kurahisisha utoaji wa huduma za fedha kwa njia ya kidigitali, hali ambayo inawa-furahisha wateja wa kizazi cha sasa ambao hawana muda wa kupanga foleni kwenye benki.

Hata hivyo, wataalam hao wa fedha wanasema mifumo hii inatakiwa kupokele-wa kwa umakini wa hali ya juu ili kuhakiki-sha kuwepo kwa usalama.Kwa mfano, Kampuni ya utafiti ya Financial Insights inakadiria kwamba benki kubwa duniani zinaokoa hadi $15 bilioni kwa mwaka kwa kutumia mifumo ya kutunza taarifa mawinguni (cloud adoption).

Hata hivyo, safari ya kidigitali sio salama sana kutokana na mifumo ya kidigitali kudukuliwa na wakati mwingine ikichangiwa na wafanyakazi wa benki wasio waaminifu.

Kampuni ya utafiti ya Cybersecurity Ventures inakisia kwamba uhalifu wa mtandaoni utagharimu kampuni kiasi cha $6 trilioni kwa mwaka duniani kote kutoka $3 trilioni mwaka 2015.Wataalam wa fedha wanasema teknolojia haikwepeki na kwamba ina umuhimu mkubwa lakini wakatoa tahadhari kwamba ni lazima kujiridhisha na usalama kabla ya kukubali mfumo wowote mpya.

“Teknolojia inakua haraka sana na taasisi zetu haziwezi kukwepa. Lakini ni muhimu kuhakikisha wanaotoa huduma hizi wako salama kiasi gani na mifumo yao inadhibitiwa na mamlaka za udhibiti,” alisema Wycliffe Momanyi, mkuu wa kitengo cha usalama cha benki ya KCB Kenya.Msimamo wake ni kwamba sio kila mfumo unapokuja uchukuliwe haraka.“Unajua kuna vitu kama cryptocurrency ambavyo havina udhibiti wa kisheria katika nchi zetu.

Lakini pia taasisi zetu nyingi za fedha hazimudu kuweka vitengo maalum vya kuzuia uhalifu wa kimtandao. Tusiharakie kila kitu,” alisema Momanyi.“Suala la usalama wa kimtandao ina-bidi lijadiliwe kwenye vikao vya bodi na ni muhimu kuwa na wataalam wa mambo hayo kama wajumbe wa bodi ili walisi-mamie vizuri,” aliongeza.Kwa upande wao wataalam wa masuala ya teknolojia wanatabiri kwamba mstakabali wa huduma za fedha upo mikono-ni mwa kampuni za teknolojia ambazo zinakuja na ubunifu wa kurahisisha huduma kila wakati.

Mwanzilishi na mshauri mkuu wa kampuni ya Swordfish Security ambayo hutoa ushauri kuhusu usalama wa mifumo ya kompyuta Gregory Almeida anasema kam-puni za teknolojia ndizo zitakazoendesha huduma za benki baadae.

“Hizi kampuni za teknolojia ya fedha ndizo zitakazotawala katika utoaji huduma ambazo sasa zinahamia kwenye mifumo ya kidigitali. Lakini hiyo ni fursa pia kwa benki kuzikopesha kampuni hizi maana zinahitaji kuwekeza Zaidi kwenye mifu-mo ya kutolea huduma za fedha,” alisema Almeida ambaye alitoa mada katika mkutano huo.“Huu pia ndio muda mzuri kwa taasisi za fedha kuandaa ujuzi utakaohitajika baadae. Watu kama wataalam wa teknolojia ya habari, sayansi na hata wanasaikolojia watahitajika.

Wanasaikolojia watasaidia taasisi za fedha kujua mabadiliko ya tabia za wateja ili huduma ziendane kile wanachokitaka watumiaji,” aliongeza.Baadhi ya wataalam wa fedha wao wan-aona bado watu na mifumo ya analojia inahitajika licha ya kuwepo mifumo ya kidigitali.“Mimi nafikiri tunatakiwa kwenda na vyote.

Tusijikite sana kwenye mifumo ya kidigitali halafu tukasahau wafanyakazi ambao ni muhimu sana kwa ajili ya kuleta mabadiliko,” alisema mkurugenzi wa BOA Bank Tanzania Joseph Iha.

MaadiliNaye meneja uendeshaji katika Benki ya TPB Kolimba Tawa aliwakumbusha wataalam hao kwamba kuzingatia maadili ya kazi ni muhimu sana ili kuifanya mifumo ya kidigitali iwe salama.

“Sisi watu wa benki hatupaswi kuho-fia teknolojia bali tukakikishe mabadiliko haya yana udhibiti wa kisheria kwa ajili ya usalama wetu na wa wateja. Lakini ili tufanikiwe Zaidi, tuzingatie maadili na uaminifu.

Hatua za kuhakikisha maadili na uami-nifu vinakuwepo katika taasisi za fedha zimekuwa zikichukuliwa lakini bado kuna changamoto ya ushirikiano.“Wakati fulani tuliwaambia wakurugenzi wa benki kwamba wawe wanatupatia ripoti na orodha za watu wanaofukuzwa kwa sababu ya kukiuka maadili kwa kujihusisha na wizi kwa mfano ili tuhakikishe hawapati ajira taasisi zingine.

Lakini halikufanikiwa maana wakati mwingine uhalifu hufanywa kwa ushirikiano na viongozi wa juu wa taasisi,” alisema Tuse Joune kutoka chama cha wataalam wa benki Tanzania (TBA).Wengine walisema taasisi za fedha zijikite Zaidi kuwaridhisha wateja ili kusiwepo na vitendo kama wizi wa kimtandao ambao ni kinyume cha maadili na uhalifu kisheria.“Kampuni za teknolojia ya fedha zinawafikiria zaidi watumiaji wa huduma zao. Sisi watu wa benki tunatakiwa kuwa hivyo pia ili wateja wetu waongeze imani na sisi tuwatendee haki,” alisema James Manyama kutoka benki ya NMB.

Maadili ya utendaji kazi yalichukua nafasi kubwa katika mijadala ya watalam hao ambao walisema yatasaidia kufanya huduma za benki ziwe salama.Dk Irene Isaka ambaye ni mhadhiri kati-ka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) alisema kuna haja ya maadili kufundishwa kwa umakini katika ngazi ya familia.“Maadili ni mada nyeti sana wengine hujiuliza kama mtu anazaliwa nayo au yanafundishwa.

Nafikiri kuna haja ya kuwafundisha watoto maadili ili wawe wataalam waaminifu,” alisema.Naye Neema Mssussa kutoka kampu-ni ya ushauri ya EY alisema kuna haja ya viongozi wa taasisi za fedha kukaa na wafanyakazi na kuwakumbusha maadili kila mara ili iwe sehemu ya maisha yao.“Tunasaini viapo vya maadili lakini wafanyakazi wanavikubali kutoka moyoni na kuishi maisha hayo?

Lazima tukumbushane kila wakati tena hata mmoja mmoja ili kuhakikisha inakuwa sehemu ya maisha,” alisema.“Viapo hivi vipo pamoja na sheria siku nyingi lakini bado uhalifu unaendelea na unaongezeka hasa kipindi hiki cha digi-tali,” aliongeza.