Wataalam wasisitiza ulinzi wa wateja kwanza


Wataalam wasisitiza ulinzi wa wateja kwanza

Wataalam wa huduma za fedha walifundwa kuhusu kuwalinda wateja wao dhidi ya udanganyifu na wizi wakati ambao matukio hayo yanachochewa na uwepo wa teknolojia.

Arusha. Wataalam wa huduma za fedha walifundwa kuhu-su kuwalinda wateja wao dhidi ya udanganyifu na wizi wakati ambao matukio hayo yanachochewa na uwepo wa teknolojia.

Mkurugenzi wa benki ya UBA Tanzania, Osman Isiaka ambaye aliongea kwenye mkutano wa kimafunzo unaowaku-tanisha wataalam wa benki kutoka nchi za Afrika Mashariki alisema pamoja na kuwepo sheria na taasisi za kulinda wate-ja, bado benki zenyewe zinatakiwa kuchukua hatua.

“Hizi taasisi na sheria zipo lakini njia nzuri zaidi ni sisi wataalam wa benki kuzingatia maadili na weledi wetu. Benki pia zinatakiwa kuchukua hatua kama vile kuanzisha sera na madawati maalum ya kushughulikia kero za wateja,” alisema Isiaka wakati akiwasilisha mada yake kuhusu ulinzi kwa watumiaji wa huduma za kibenki.

Isiaka anasisitiza kujikita katika huduma kwa mteja pia alisema pamoja na kuwepo sheria na taasisi, bado hakuna sheria maalum kwa ajili ya kulinda wateja wa huduma za fedha huku akizitaka benki kutoa mikopo kwa uwazi na uaminifu.

“Kuna baadhi hutoa mikopo lakini masharti hawayaweki wazi. Matokeo yake unakuta mteja anatozwa riba na makato makubwa kuliko alivyotarajia….Tutoe mikopo responsibly,” aliongeza.

“Siku hizi kuna mitandao ya kijamii ambayo ina nguvu sana, ukimdhulumu mteja atakupeleka huko na hiyo inaon-doa uaminifu wetu kabisa. Cha msingi ni kuwapa wateja haki zao,” alisema.

Mkutano huo wa siku tano uliisha Ijumaa iliyopita baada ya mafunzo na majadiliano kuhusu uzingatiaji wa maadili katika kutoa huduma benki hasa katika kipindi hiki ambako huduma nyingi za kibenki zinatolewa kwa mifumo ya kidigitali.

Yusto Tongola kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tira) aliwaongoza wataalam hao katika kuonyesha hatua mbalimbali zilizochukuliwa na wasimamizi wa sekta hiyo kulinda wateja.

Alitaja sheria za benki kuu na taasisi kama mahakama za usuluhishi na tume ya ushindani ambazo zipo kwa ajili ya kulinda watumiaji wa huduma mbalimbali nchini.

“Hata hivyo, bado kuna changamoto ya kuwaelimisha wateja ambao baadhi hawajui haki zao,” alisema.

“Bado pia taasisi za fedha hazitumii ipasavyo taasisi za kutadhmini wakopaji (credit reference system),” alisema.

Baadhi ya wachangiaji walisisitiza kuwajibika kwa watoa huduma kwa kuzingatia haki na maadili.

Mjadala huu unakuja siku chache baada ya naibu gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk Bernard Kibese kusema kwamba benki hiyo iko hatua za mwisho kukamilisha kanuni za kulinda watumiaji wa huduma za kifedha.

Teknolojia

Mtaalam wa masuala ya usalama mtandaoni Gregory Almeida aliwaambia wataalam hao kwamba teknolojia haikwepeki na kwamba wajiandae kwendana na hali hiyo.“Makampuni ya teknolojia ndiyo yatakayoendesha huduma za fedha lakini ni fursa kwa benki kuyapa mikopo maana yanahitaji fedha za mitaji,” alisema.“Pia ni wakati kwa benki kuanza kutafuta ujuzi unaohi-tajika. Wataalam wa data, wanasaikolojia na watu kama hao watawasaidia sana. Tabia za wateja zinabadilika kulingana na mabadiliko ya teknolojia hivyo wanasaikolojia watahita-jika kuwasoma wateja,” alisema Gregory.