Ni mwaka mmoja wa mafanikio DAWASA


Ni mwaka mmoja wa mafanikio DAWASA

• Ni baada ya kuunganisha shughuli za DAWASA na DAWASCO • Miradi 15 yatekelezwa katika maeneo ambayo hayakuwa na maji • Wananchi lukuki waunganishiwa huduma ya Maji.

Tunaweza kusema ni Mwaka mmoja wa mafani-kio kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) tangu kuunganishwa kwa DAWASA kwa DAWASCO. Aidha Menejimenti ya Mamlaka hii ilizinduliwa rasmi Septemba 8, 2018. Ilikuwa ni jambo la busara kuun-ganisha taasisi hizi mbili ili kuunda Mamlaka kubwa na yenye nguvu miongoni mwa Mamlaka za Maji nchini.

Nini siri ya mafanikio haya kwa muda mfupi?

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange anabainisha kuwa siri ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi hiki kifupi ni uongozi IMARA uliokuwa na malengo ya kufikisha huduma kwa wananchi wengi zaidi pamoja na utayari wa watumishi wa Mamlaka katika kutoa huduma bora ya Majisafi na Majitaka.

“Katika yote tunajivunia utayari wa watumishi wetu katika kuandaa mipango endelevu na kutekeleza kwa vitendo maagizo ya viongozi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya majisafi na majitaka,”alisema Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

Mwaka mmoja wa DAWA-SA mpya kwangu mimi kama Mwenyekiti wa Bodi na wajumbe ndani ya Bodi ninayoiongoza inatupa faraja ya kuona Mamlaka tunayoisimamia inafanya kazi nzuri inayoonekana na wananchi tunaowahudumia.

Katika kipindi cha mwaka mmoja, miradi mingi iliyoleta ahueni kubwa kwa wananchi ndani ya eneo la huduma la DAWASA imetekelezwa. Miradi ipa-tayo 15 imekwisha kamilika nayo ni pamoja na Mradi wa Maji Tabata Bonyokwa, Tabata Kisukuru, Mradi wa Maji Kiwalani awamu ya pili na ya tatu, Mradi wa Maji Saranga, Kiembeni, Kitopeni, Kilimahewa, Lulanzi, Salasala, Zinga na Mradi wa Maji Zinga Moto.

Hivi sasa wananchi katika maeneo hayo wanaendelea kupata huduma.Vilevile aliainisha Miradi kumi ya maji inayotarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni ambayo ni pamoja na Mradi wa Maji Minazi minane, Makurunge awamu ya pili, Mingo awamu ya pili, Mabwepande, Kilindoni, Kidunda, Zegereni, Disuny-ala, Kibaha Tamco/ Pangani na kazi ya kuweka mtandao wa Maji eneo la Buza.“Tulipoanza usimamizi wa Bodi hii, Mamlaka ilitenga asilimia 30 ya mapato yake katika utekelezaji wa miradi. Sasa imeongeza kiwango na kutenga asilimia 45 ya mapato yake katika usimamizi na utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya majisafi na majitaka itakayoweza kufikisha lengo la asilimia 95 ya upatikanaji majisafi na 30% ya huduma ya majitaka ifikapo 2020,” alimalizia Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja anasema hadi sasa Mamlaka imefanikiwa kusambaza maji safi na salama kwa asilimia 85 jijini Dar es Salaam.“Zawadi yetu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dk. John Magufuli hadi kufikia Dis-emba 9 mwaka huu ni kukamilika mradi wa Maji wa Chalinze- Mboga utakaohu-dumia wananchi takribani 125,000,” anasema Mhandisi Luhemeja, na kuongeza kuwa katika kipindi hicho ana hakika kuwa mradi wa Kisarawe nao utakuwa umekamilika. Mradi wa Kisarawe ni agizo la Mheshimiwa Rais wakati akizindua mtambo wa Ruvu Juu, Juni 21, 2016.Mhandisi Luhemeja anabainisha kuwa awali mwaka 2015 Jiji la Dar es Salaam lilikuwa linapata maji kwa asilimia 68 na jum-la ya maunganisho ilikuwa 123,000.“Kwa wakati huo upotevu wa maji ulikuwa asilimia 53 na Shirika la DAWASCO ilikuwa inakusanya kiasi cha Tsh Bil 3.2 kwa mwezi.

Leo hii tunapoongea hali ya upatikanaji maji Jijini ime-panda hadi asilimia 85 na maunganisho ya maji yameongezeka kutoka 123,000 hadi kufika 326,000. Aidha upotevu wa Maji kwa mwezi Agosti tunapomalizia mwaka mmoja tunaweka rekodi ya kufikia asilimia 39 ya kiwango cha Maji yasiyolipiwa,” anasema Luhemeja. Ameahidi kuwa jitihada hazitaishia hapo hadi pale ambapo huduma zinazotolewa na DAWASA zitakapokuwa kiwango cha kimataifa.

Aidha, Mhandisi Luhemeja anasema kiwango cha mapato ndani ya mwaka mmoja na kuungana kimekuwa kutoka wastani wa makusanyo ya Sh. Bil 9.2 kwa mwezi hadi sasa wanakusanya wastani wa Sh. Bil. 11.2 kwa mwezi. “Kwa mwaka wa fedha uliokwisha DAWASA ilikusanya Sh. Bil. 135 sawa na asilimia 95 ya lengo,” alisema Mhandisi Luhemeja.
Mhandisi Luhemeja anabainisha kuwa kwa upande wa huduma kwa wateja imefanikiwa kuboresha namna ya ulipaji wa Ankara. “Wateja wetu wanalipia kupitia mtandao, hiyo imewarahisishia wananchi kulipia huduma,” alisema na kuongeza kuwa wateja pia wamekuwa wakikumbushwa mara kwa mara njia za malipo ili kuweza kulipa kwa wakati huduma muhimu ya Maji.
Akishukuru wateja wote kwa uaminifu waliouonyesha kwa Mamlaka katika kipindi cha mwaka mmoja
Afisa Mtendaji Mkuu aliahidi kuboresha utendaji wa Mamlaka kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili huduma iendelee kupunguza gharama za uendeshaji.
“Nichukue fursa hii kusema katika kipindi ambacho serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani DAWASA haijapandisha bili ya maji pia niseme DAWASA haina mpango wa kupandisha bili za maji katika kipindi chotecha uongozi wa serikali ya
awamu ya tano,” anasema Mhandisi Luhemeja.
Mhandisi Luhemeja anasema DAWASA inaendelea na mpango wake wa kuunganisha wateja kwa mkopo ambapo wengi sasa wanajitokeza. “Nitumie fursa hii kuwajulisha
wananchi kwamba maunganisho ya huduma za maji ya DAWASA ni kwa
mkopo kwa yeyote anayehitaji kuunganishiwa huduma,”alisema na kuwataka
wananchi kutoa ripoti kwa vyombo vya dola kwa yeyote atakayekuwa anatoza fedha
kwa ajili ya maunganisho. Katika kuendeleza azma yake ya kuboresha huduma,DAWASA inaendelea kutekeleza Jumla ya miradi 23 ya Majisafi katika Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya miji ya Mkoa wa Pwani. Miradi hiyo ni pamoja na Mradi
wa Maji Kibamba- Kisarawe, Jet- Buza, Kisarawe- Pugu, Mradi wa Maji Maneromango, Mradi wa Maji Mkuranga, Mradi wa Maji Gezaulole, Tungutung, Kiharaka, Mpiji, Stakishari, Majumba sita, Vingunguti, Kipawa, Sanzale, Ukuni, Ujenzi wa tanki la kuhifadhia Maji mji wa Bagamoyo, Mradi wa Maji Nyakasangwe, Mradi wa Maji Nia njema na Mradi wa ulzaji wa bomba kubwa la Majisafi kutoka Mlandizi hadi Maneromango.

Kwa mujibu wa Mhandisi Luhemeja, miradi mingine
mipya 10 inatarajiwa kutekelezwa na lengo ni kwenda kujibu kero za wakazi hao wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Utekelezaji wa Miradi hii ni ishara na dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kuwaondolea wananchi changamoto ya upatikanaji wa huduma ya Majisafi jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani.