Zitambue fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu 2019/20 zinazopatikana UAUT


Zitambue fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu 2019/20 zinazopatikana UAUT

Pamoja na kutoa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu, Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania kinahakikisha kutoa Shahada zenye ubora wa kimataifa kwa kuajiri Wahadhiri kutoka ndani na nje ya nchi wenye ujuzi na uzoefu mkubwa wa kufundisha.

Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (The United African University of Tanzania), ni Chuo kikuu binafsi kinachomilikiwa na taasisi ya kidini ya Kikristo iitwayo Korea Church Mission. Kilianzishwa mwaka 2011 na kupewa Cheti cha usajili Kamili na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, namba ya usajili: CR1/024. Chuo kipo Wilaya ya Kigamboni, kata ya Vijibweni, Kiwanja namba 772, Kitalu F, Mkoa wa Dar es Salaam.

Pamoja na kutoa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu, Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania kinahakikisha kutoa Shahada zenye ubora wa kimataifa kwa kuajiri Wahadhiri kutoka ndani na nje ya nchi wenye ujuzi na uzoefu mkubwa wa kufundisha.

Wahadhiri hawa wanatoka katika mataifa mbalimbali ikiwemo Korea Kusini, Ujerumani, Marekani, Canada na kipaumbele kwa wazawa.

Kwa sasa chuo kinatoa shahada kwa programu mbili (2) ambazo ni Bachelor of Science in Computer Engineering and Information Technology (BSc. CoEIT) kwa miaka 4 na Bachelor of Business Administration (BBA) kwa miaka 3. Chuo kina mpango wa kuongeza programu zingine kwa awamu kwa miaka ijayo.

Ada inayotozwa kwa hivi sasa ni nafuu sana na inalipwa kwa awamu ukilinganisha na vyuo vikuu vingine nchini.

Fursa zinazopatikana kwa watakaojiunga kwa mwaka wa masomo 2019/20

Fursa hizo ni pamoja na kulipiwa ada ya masomo, kulipiwa garama za malazi (Hostel), kulipiwa gharama za stationery, ufadhili wa kifedha kwa wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu, kutafutiwa taasisi ya kufanya mafunzo kwa vitendo na baadae kuajiriwa kwenye makampuni ya Korea Kusini yanayofanya kazi hapa nchini Tanzania, kutafutiwa taasisi ya nje ya kufanya mafunzo ya kazi kwa vitendo (Internship), kutafutiwa kazi nchini Korea Kusini kwa watakaofanya vizuri katika masomo, kupatiwa ajira hapa chuoni baada ya kumaliza masomo.

Chuo kinatoa fursa ya kujifunza lugha ya Kikorea inayokupatia nafasi ya kusoma na kufanya kazi Korea Kusini. Pia mafundisho ya kujiweka imara kiafya na kuweza kujilinda (Taekwondo) kwa miaka 2.

Maono ya Chuo

Ni kuandaa wanafunzi bora wenye uaidilifu wakiongozwa na Mungu.

Utume wa Chuo

Ni kutumikia jamii kubadilisha mtazamo na mawazo kuendana na wakati. 

Ili kufikia hayo, chuo kinakusudia kuwafundisha na kuwainua viongozi bora watakaolitumikia Taifa na dunia  kwa uadilifu wakiongozwa na ufahamu, hekima, na hofu ya Mungu.

Chuo kimeandaa sera sahihi na utekelezaji wake, usimamizi na mwongozo wa ufundishaji unaolenga kukidhi matakwa ya uendeshaji wa Elimu ya Juu kulingana na maelekezo ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU Standards, Guidelines and other Operational Tools).

Kuna mazingira rafiki ya malazi kwa wanafunzi yakiwemo mabweni ya kutosha kwa jinsia zote mbili, maktaba yenye vitabu zaidi ya 30,000, majarida mbalimbali, E-resources, Mtandao wa internet wa bure (free Wi-Fi), stationari na huduma nzuri za chakula.

Ufadhili wa Shahada ya Uzamili (Master’s degree)

Chuo kinatoa ufadhili wa shahada ya uzamili kulingana na ufaulu katika mitihani. Chuo kinagharamia usafiri, malazi, chakula, ada pamoja na stationery kwa kipindi chote cha masomo nchini Korea Kusini.

Wanafunzi wetu wanapelekwa kusoma kwenye vyuo vinavyotambulika duniani na vyenye viwango vya kimataifa.

Tunawakaribisha sana wahitimu wa kidato cha sita na waliomaliza Diploma kuchangamkia fursa hii adhimu ya elimu ya juu.