Siku mbili za mafunzo ya CDM zinatosha kukabiliana na mikopo isiyolipika na madeni sugu


Siku mbili za mafunzo ya CDM zinatosha kukabiliana na mikopo isiyolipika na madeni sugu

Mbali na kukusanya madeni kampuni hii inajihusisha na utoaji wa mafunzo ya ukusanyaji wa madeni katika makampuni mbalimbali, sambamba na utoaji wa ushauri wa kitaalamu juu ya shughuli nzima za ukusanyaji wa madeni.

Credit and Debt Masters Company Limited (CDM) ni kampuni binafsi inayojishughulisha na ukusanyaji wa madeni kwa niaba ya wateja wake.

Mbali na kukusanya madeni kampuni hii inajihusisha na utoaji wa mafunzo ya ukusanyaji wa madeni katika makampuni mbalimbali, sambamba na utoaji wa ushauri wa kitaalamu juu ya shughuli nzima za ukusanyaji wa madeni.

Katika utekelezaji wa majukumu yake ya kimsingi, CDM inatarajia kuendesha mafunzo juu ya usimamizi wa mikopo isiyolipika na ukusanyaji wa madeni sugu yatakayofanyika Septemba 26 na 27 mwaka huu katika Hoteli ya Ramada Encore, iliyopo mtaa wa Ghana, Posta, Dar es Salaam.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa CDM, Patrick Mayige anaelezea kuwa, “Kozi itakayofundishwa katika mafunzo hayo, itakuwa na moduli tatu, ambapo moduli ya kwanza itabeba utangulizi, moduli ya pili itahusu usimamizi wa mikopo isiyolipika na moduli ya tatu itaangazia zaidi njia zinazotumika kudai na kukusanya madeni hapa nchini Tanzania.”

Kuhusu kauli mbiu ya mafunzo hayo Mayige anasema kuwa, “Mafunzo hayo yataongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Kwa nini ufikirie kuifuta mikopo isiyolipika mwisho wa mwaka wakati inawezekana kuidai na kuikusanya ndani ya siku 90 tu?” (Why write-off your NPL at year end if you can recover them in 90 days?).”

Anasema, kutokana miongozo mipya iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) juu ya usimamizi wa mikopo isiyolipika na ukusanyaji wa madeni, miongozo hiyo imeanza kufanya kazi rasmi ikizitaka taasisi nyingi za kifedha kuitekeleza kikamilifu.

Masharti ya kusafisha vitabu vya wakopaji na kuimarisha hali ya mali za benki na taasisi, kupunguza uwiano wa mikopo isiyolipika kutokuzidi zaidi ya asilimia 5, utengenezaji wa vitengo vya mikopo na utaratibu kwa ajili ya ukusanyaji wa mikopo, kwa pamoja haya yote yanachagiza umuhimu wa uwepo wa mafunzo haya yenye tija katika maeneo hayo mawili ya usimamizi wa mikopo isiyolipika na ukusanyaji wa madeni sugu hapa Tanzania.

Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Akademia ya Mafunzo ya CDM yameandaliwa katika viwango vya kimataifa yakiwasilishwa kwa kuzingatia muktadha wa Kitanzania. Mafunzo hayo hayataangalia usimamizi wa mikopo isiyolipika peke yake bali pia yataonyesha njia zilizothibitishwa kufanikiwa katika ukusanyaji wa madeni wa kitaalamu.

Kuhusiana na watu gani wanaotakiwa kuhudhuria mafunzo hayo Mayige anabainisha kuwa,  “Watu wanaotakiwa kuhudhuria mafunzo hayo ni pamoja  na maofisa wakusanya madeni na mameneja, watu wa mauzo na masoko, maofisa mikopo na wachanganuzi, maofisa wadai mikopo, wataalamu wa masuala ya fedha za makampuni, maofisa sheria na majanga mbalimbali, mameneja wa biashara, wamiliki wa biashara, na yeyote yule mwenye kupenda kufahamu zaidi kuhusu mchakato wa usimamizi wa mikopo isiyolipika na urudishaji wa madeni.”

Mafunzo haya ni muendelezo wa jitihada zinazochukuliwa na CDM ambayo hutoa mafunzo haya kila mwaka katika kuzijengea uwezo kampuni na taasisi mbalimbali katika kukabiliana na mikopo isiyolipika na ukusanyaji wa madeni sugu kitaalamu jambo ambalo limekuwa changamoto ya taasisi nyingi hapa nchini na kufikia hata kushindwa kujiendesha na hata kufungwa kabisa.”

“Mafunzo haya yanatolewa kwa gharama nafuu, Unaweza kuhifadhi nafasi yako ya ushiriki katika mafunzo hayo kupitia barua pepe: [email protected] ukituma pia kwa (cc): [email protected] au piga namba: 0754 058 904, 0784 201 332, 0763 200 332,” anasema Mayige.