Mafanikio ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu [TPRI] katika kipindi cha awamu ya tano (2015 - 2019)


Mafanikio ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu [TPRI] katika kipindi cha awamu ya tano (2015 - 2019)

Shughuli za utafiti zilipanuka na kuongeza viuandege waharibifu, viuakupe, viua-panya, utafiti wa madhara ya viuatilifu kwa afya ya binadamu na uchafuzi wa mazingira.Miaka kumi baadaye mnamo mwaka 1977 Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika na TPRI ikawekwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais hadi hapo mwaka 1979 ilipoundiwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria Namba 18.

Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kudhibiti Visumbufu katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) ilianza mwaka 1945 chini ya Ofisi ya Utawala wa Kikoloni wa Kiingereza. Kulikuwa na kikundi cha wataalamu huko London, Uingereza kilichojishughuli-sha na unyunyiziaji wa viuatilifu vilivyotengenezwa kiwandani kwa ajili ya kudhibiti visumbufu wa ukanda wa tropiki. Kikundi hiki kilianzia shughuli zake Entebbe nchini Uganda wakiwa wamejikita katika utafiti wa ndorobo na mbu.

Mnamo mwaka 1950 kikundi hiki kilihamia Arusha kikiwa chini ya utawala wa kikoloni na kuanzisha kituo kilichoitwa “Colonial Insecticides Research Unit (CIRU)”. Mwaka 1962 CIRU ili-unganishwa katika shughuli za kitafiti za Shirika la Pamoja la nchi za Afrika ya Mashariki (East African Common Services Organisation (EACSO). Baada ya muda mfupi shughuli hizi zilipanuka na kuongezeka kutoka kusimamia utafiti wa wadudu hadi viuagugu, viuakuvu na viuakonokono waenezao kichocho.

Kwa wakati huo watafiti walikuwa wachache kwenye nyanja za biolojia ya wadudu na mimea katika nchi za Afrika Mashariki. Mwaka 1967 Jumuiya ya Afrika Mashariki iliundwa ili kuchukua nafasi ya EAC-SO na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticides Research Institute TPRI) ikawa mojawapo ya Taasisi za utafiti ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Shughuli za utafiti zilipanuka na kuongeza viuandege waharibifu, viuakupe, viua-panya, utafiti wa madhara ya viuatilifu kwa afya ya binadamu na uchafuzi wa mazingira.Miaka kumi baadaye mnamo mwaka 1977 Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika na TPRI ikawekwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais hadi hapo mwaka 1979 ilipoundiwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria Namba 18.

Sheria hii ilianzisha rasmi TPRI kama mojawapo ya Taasisi za Umma yenye malengo yafuatayo:i) Kufanya utafiti, kutathmini na kusambaza matokeo yanayohusu matumizi ya viuatilifu na tabia zake katika kudhibiti visumbufu vya nchi za Ukanda wa Kitropiki kwa kutumia njia za angani na ardhini; kudhibiti visumbufu vya kilimo, magonjwa ya mimea, ndege waharibifu, panya, ndorobo, mbu, konokono, kupe, madhara ya viuatilifu kwa afya ya binadamu, kemia ya viuatilifu, fizikia ya viuatilifu, uhandisi wa mabomba, sayansi ya mimea pamoja na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira.ii) Kuanzisha Karantini ya Kitaifa ya Mimea (National Plant Quarantine Station  NPQS).iii) Kuanzisha kitengo cha utambuzi na utunzaji wa sampuli kavu za mimea kwa ajili ya rejea (National Herbarium of Tanzania).iv) Kusimamia na kudhibiti utengenezaji, uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya viuatilifu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. v) Kuendeleza Kitengo cha Kitaifa cha kuhifa-dhi nasaba za mimea “National Plant Genetic Resources Center”.

Dhima ya TPRI

Matumizi sahihi na salama ya viuatilifu yenye kujali Afya za watu na Mazingira kwa kilimo endelevu.

Maono ya TPRI

Kuwajengea wakulima na Jamii kwa Ujumla uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya namna ya kudhibiti visumbufu vya mimea na kufanya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu na kupata taarifa sahihi kuhusu mimea na mazao yake kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae kwa kilimo endelevu.

Salamu kutoka kwa Mwe-nyekiti wa Baraza la Waku-rugenzi TPRI Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi TPRI

Prof. Raphael T. Chibunda ni Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi TPRI ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo. Anaeleza kuwa baada ya Baraza la Wakurugenzi kuteuliwa mwaka 2016, liliweza kuainisha changamoto mbalimbali zilizokuwa zinaikabili Taasisi na kutoa maelekezo mbalimbali kwa Menejimenti ya TPRI ya namna ya kuboresha utendaji kazi ili kuweza kutatua changamoto hizo. Kwa kutambua umuhimu na mchango wa Taasisi ya TPRI kwenye kukuza sekta ya Kilimo, Baraza la Wakurugenzi liliagiza kuwa Taasisi iboreshe maabara zake kwa kununua mshine mpya na za kisasa kama vile High Performance Liquid Chromatograph (HPLC), Gas Chromatograph (GC) na Gas Chromatograph Mass Spectrometry (GC-MS) kwa ajili ya uchambuzi wa viuatilifu ili kudhibiti ubora ikiwa ni jitihada za kuongeza tija katika kilimo kwa kuwapa-tia wakulima viuatilifu vilivyo bora.

Aidha, vifaa hivyo vinatumika kwenye utambuzi wa masalio ya viua-tilifu kwenye mimea, bin-adamu, maji na mazingira kwa ujumla. Katika jitihada zake za kuongeza ufanisi wa shughuli za Taasisi, Baraza lilielekeza kuendelea kutoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu kwa wadau wake mbalimbali ili kuzuia athari zozote kwa binadamu, viumbe wengine na mazingira. Aidha, walisisitiza kuwa huduma ya kupima madhara na kiwango cha sumu mwilini kinachotokana na matumizi yasiyo sahihi na salama ya viuatilifu kwa wadau wake yafanyike nchi nzima ili kulinda afya ya mlaji na mazingira.

Baraza limehimiza Taasisi iendelee kupima na kuhakiki masalio ya viua-tilifu kwenye mazao kwa ajili ya kuongeza usalama wa vyakula na pia kuongeza fursa ya Tanzania kuuza mazao yake katika masoko ya kimataifa. Sambamba na jukumu hilo la msingi, Baraza la Wakurugenzi limeitaka TPRI kuendeleza tafiti zake na kutoa huduma za kiufundi katika nyanja za kudhibiti Visumbufu vya mazao ya kilimo na vile vienezavyo magonjwa kwa binadamu na wanyama kama vile mbu, ndorobo na kupe.

Vitengo vingine vya Taasisi hii ambavyo vilitiliwa mkazo na Baraza ya Wakurugenzi ni pamoja na kitengo cha kuhifadhi sampuli kavu za mimea kwa ajili ya rejea za kisayansi (National Herbarium of Tanzania), kitengo cha kukusanya na kuhifadhi Nasaba za mimea nchini (National Plant Genetic Resources Centre) kwa ajili ya matumizi endelevu na kitengo cha karantini ya mimea na mazao (National Plant Quarantine Center).Prof. R. Chibunda anaishukuru menejimenti ya TPRI pamoja na wafanyakazi wote kwa ushirikiano waliompa yeye na wajumbe wenzake katika kipindi chote cha miaka mitatu waliyotumikia Baraza hili.

Neno kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPRI

Dkt. Margaret Mollel, anaeleza kuwa, madhumu-ni ya utekelezaji wa maju-kumu ya Taasisi ya TPRI ni kuleta tija katika sekta ya kilimo kwa kutumia viuatilifu vilivyo bora. Taasisi ya TPRI imepata mafanikio katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya utafiti wa viuatilifu, udhibiti wa biashara za viuatilifu (wauzaji, wachanganyaji (formulators), wafukizaji (fumigators) na waagizaji (importers) na wafungashaji (repackers) kwa njia ya ukaguzi pamoja na kutoa vibali vya kufanya biashara ya viuatilifu. Taasisi ya TPRI vilevile imetekeleza majukumu yake ya kutoa mafunzo kwa wadau ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu pamoja na mabomba ya kunyunyizia na vinyunyizi, kuhakiki ubora wa viuatilifu vilivyoingizwa nchini kabla havijasambazwa kwa wakulima, kupima masalia ya viuatilifu (Maximum Residues Limits - MRLs) kwenye mazao ya mbogamboga kwa madhumuni kulinda afya ya walaji ndani na nje ya nchi. Taasisi ya TPRI vilevile imefanikiwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ya udhibiti wa visumbufu vamizi, vikiwemo magugu, wadudu vamizi na wanyama waharibifu wa mazao kama ndege na mapanya.

Wadau 3,561 walipata mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu, mabomba ya kunyunyizia na vinyunyizi pamoja na udhibiti wa magugu na visumbufu vamizi vya mazao.b] Sampuli 3,500 za viuatilifu zilihakikiwa ubora wake kabla ya viuatilifu hivyo kuruhusiwa kusamba-zwa kwa wakulima nchini. c] Jumla ya maduka 3,000 ya wauzaji wa viuatilifu yalikaguliwa ili kuhakiki yanakidhi matakwa ya Sheria. d] Wafanyabiashara takribani 4,842 wa viuatilifu waliopata vibali vya kufanya biashara husika.e] Sampuli 3,225 za mbogambaoga zilipimwa ili kuhakiki masalia ya viuatilifu (MRLs) kwa kulinda afya za walaji.f] Wadau 6,837waliopata mafunzo ya kudhibiti magugu na visumbufu vamizi Mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi ya TPRI kunachangia kuleta tija katika kilimo kwa kuongeza wingi na ubora wa mazao. Mafanikio ya kuongeza tija katika kilimo ni matokeo ya Taasisi ya TPRI kuhakikisha kwamba wakulima wanapa-ta viuatilifu vyenye ubora, kutoa mafunzo ya matu-mizi sahihi ya viuatillifu, mabomba ya kunyunyizia na vinyunyizi

Mafanikio Ukaguzi wa biashara ya viuatilifu

Ukaguzi wa biashara ya viuatilifu ulifanyika kuhakikisha kwamba wafanya biashara wa viua-tilifu wanafuata na kukidhi matakwa ya Sheria ya Udhibiti wa Visumbufu vya Mimea Na. 13 ya Mwaka 1997. Jumla ya maduka 3,000 yalifanyiwa ukaguzi Tanzania bara katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu (maduka 10 yalifungwa); Kigoma, Tabora, Morogoro (maduka 15 yalifungwa); Njombe (maduka 14 yalifungwa); Iringa (maduka 8 yalifungwa); Katavi, Mbeya, Rukwa, Songwe. Dar-es-Salaam, Lindi, Mbeya, Nkasi, Sumbawanga, Kagera, Arusha, Mwanza. Maduka yaliyofungwa yalivunja she-ria ikiwemo uuzaji wa viuatilifu ambavyo vilipitwa na muda wake wa matumizi au kutosajiliwa.

Utoaji wa vibali mbalimbali vya kufanya biashara ya viuatilifu

Vibali vya wafukizaji (‘’fumigators) [905;] Wauzaji wa Viuatilifu [1,230], vibali vya uingizaji wa Viuatilifu nchini [2,697], na wachanganyaji (‘’formula-tors’’) [7].

Uhakiki wa ubora wa viuatilifu vilivyoingizwa nchini

Jumla ya sampuli 3,556 kutoka kwenye viuatilifu vilivyoingizwa nchini vilichambuliwa katika maabara ya TPRI. Sampuli za viuatilifu vilivyopimwa vilikidhi ubora unaotakiwa. Viuatilifu aina sita havikudhi ubora wa viwango vinavyotakiwa na vilirudhishwa nchi zilikotoka kwa mujibu wa Ibara ya 41 ya Sheria ya Udhibiti wa Visumbufu vya Mimea Na. 13 ya Mwaka 1997 na kanuni zake za Mwaka 1999.

Upimaji wa masalia ya viuatilifu (MRLs)

Jumla ya sampuli 3,225 za mbogamboga kutoka mikoa ya Iringa, Morogoro, Dar es Salaam, Arusha na Manyara zilipimwa. Masalia ya viuatilifu kwenye sampuli zote zilikuwa ndani ya viwango vinavyokubalika Kimataifa [Acceptable Maximum Residue Limits – MRLs]. Jumla ya wanyunyiziaji 1,325 wa viuatilifu katika mashamba ya Kahawa, Chai, na Maua Mikoa ya Iringa, Songwe, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Manyara walipimwa kwa kutumia kipimo maalumu kijulikanacho kama AChE. Wanyuny-iziaji 101 (asilimia 20) waligundulika kuathirika na viuatilifu na walipewa ush-auri nasaha ili kurekebisha afya zao.

Mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu

Katika kipindi husika Taa-sisi iliandaa Kongamano la Kisayansi la Kitaifa lili-loshirikisha Watafiti, Wana-sayansi, Wakulima, Wanataaluma kutoka Vyuo Vikuu, Wafungashaji, Wafanyabi-ashara na Wauzaji wa Viua-tilifu nchini na kufunguliwa na Mhe. Waziri wa Kilimo, Ndg. Japhet Hasunga (MB) tarehe 27 – 29 Machi, 2019, Arusha, Tanzania.

Mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu pamoja na mabomba ya kunyunyizia na vinyunyizi

Mafunzo yalitolewa kwa wadau wa viuatilifu (Wauzaji, Wakulima Wawezeshaji, Maafisa ugani, Wanyunyiz-iaji wa zao la korosho, pamba, mbogamboga, n.k).Jumla ya wadau 3,561 walipata Mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu wakiwemo wakulima, Maafisa ugani, na wau-zaji wa viuatilifu.[a] Eneo ya Mafunzo ni pamoja na Lindi na Tunduru, Dar es Salaam, Nyangao, Lindi , TPRI-Arusha , Lushoto , Kilimanjaro, Mwanza, Ndanda, Mtwara , Nyakanazi, Biharamulo, Mwanza , Lukozi, Tanga, Mkalama na Songea.[b] Maeneo ya pamba ni pamoja na Kahama, Kishapu, Shinyanga, Bukombe, Mbog-we, Igunga, Nzega, Urambo, Kaliua, Uyui, Iramba, Bariadi, Itil-ima, Busega, Maswa, Meatu, Bunda, Muso-ma, Butiama, Seren-geti, Kwimba, Magu, Misungwi, Buchosa, Sengerema, Chato, Nyangw’hale na Kibondo.

Wadau waliopata mafunzo ya kudhibiti magugu na visumbufu vamizi ni 6,837

Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Wadau wa Kilimo na Ufugaji, Wauza Viuatilifu, Viongozi wa Serikali na Maafisa Kilimo na Mifugo Na Mashirika yasiyo ya Kiseri-kali kuhusu Utambuzi, Madhara na Udhibiti wa Gugu Vamizi Linalojulikana kwa Jina La Gugu Karoti (Parthenium hysterophorus) June, 2017 hadi June, 2019.

Matokeo ya Kazi za Kitafiti, Kisayansi na Kiufundi.

Kituo cha kitaifa cha kukusanya, kutambua na kuhifadhi mimea mbalim-bali nchini “National Her-barium of Tanzania” ambacho hutumika kama rejea ya mimea yenye asili ya dawa za tiba, viuatilifu na matumizi mengine kwa ajili ya jamii; kimeweza kukusanya na kuhifadhi aina mbalimbali za mimea ipatayo 5,000. Kati ya hizo zipo sampuli 50 zenye viuatilifu vya asili vitumikavyo na wakulima wa mboga mboga mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro. Sampuli nyingine ni za uoto wa asili kutoka Misitu ya Kalambo na Bonde la Uzondo Mkoa wa Rukwa na Katavi. Pia sampuli 400 zilikusanywa kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyama ya Ngorongoro. Kituo pia kimeingiza sampuli zaidi ya 3000 katika mfumo wa Kidigitali.2. Kitengo cha udhibiti wa uingizaji na utoaji wa mazao mbali mbali kimeweza kufanya ukaguzi kwenye mashamba 132 na shehena za mimea na mazao ya mimea zilizo ingizwa nchini zipatazo 3,007 ndani ya kip-indi cha miaka 5.3. Taasisi kupitia Kitengo cha udhibiti wa uingizaji na utoaji wa mazao imeshiriki katika kutafiti na kuutambua ugonjwa hatari wa mahindi ujulikanao kama “Maize Lethal Necrosis”. Huu ni mchango mkubwa katika kulinda kilimo cha zao la mahindi ili kuongeza tija.

Udhibiti wa wadudu waene-zao magonjwa ya binadamu na mifugo

Taasisi kupitia kitengo chake cha utafiti wa wadudu waenezao magonjwa kwa binadamu na mifugo (Livestock and Human Disease Vector Control - LHDV) kinafanya uchunguzi wa usugu wa wadudu hao kwa viuatilifu. Usugu wa wadudu kwa viuatilifu (Insecticide Resistance) ni hali ambayo inajitokeza kwa wadudu ambapo mdudu husika haumizwi au kuuliwa na kiuatilifu kilichokuwa kinatumika kumdhibiti vizuri awali. Wadudu wengi wanapokutana na viuatilifu mara kwa mara katika maeneo ya mashambani na majumbani ambapo viuatilifu vinatumika sana, miili yao hubadilika kijenetiki na kuweza kujikinga na madhara ya viuatlifu.

Hali hii ikijitokeza, inaleta hasara kwa wakulima, wafu-gaji. Ili kudhibiti hali hii, TPRI imekuwa inakusanya wadudu husika kutoka mikoa mbalimbali nchini, na kuwafanyia majaribio ya kimaabara ili kuona kama kuna dalili za kujenga usu-gu. Kwa upande wa mbu, kazi zimefanyika katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimajaro, Singida, Tabora na Kigoma. Kwa upande wa kupe, kazi hizi zimefanyika mikoa ya Rukwa, Tabora, Iringa, Morogoro, Dodoma, Simiyu na Pwani. Ushauri unatolewa kila ikionekana dalili za kujenga usugu kama kubadilisha au kutumia viuatilifu mchanganyiko.

Ili kudhibiti mbung’o waenezao magonjwa ya nagana kwa mifugo na malale kwa binadamu, Taasisi ilishiriki-sha wafugaji katika wilaya ya Simanjiro kuandaa na kuweka mitego inayotumika kudhibiti mbung’o kwenye maeneo ya malisho. Mradi huu ambao ulipata udhami-ni wa mfuko wa maendeleo wa kilimo kanda ya kaska-zini (ZARDEF) ulisadia wafugaji kupata technologia rahisi inayoweza kutumika maeneo ya vijijini. Aidha, katika wilaya ya Monduli, Taasisi ilifanya tathmini ya hali halisi ya uwepo na mtawanyiko wa mbung’o (Tsetse population and distribution).

Katika mradi huu ulioshirikisha wafugaji katika vijiji 10, ilibainika kuwa mbung’o wapo kwa wingi katika vijiji vilivyopo pem-bezoni mwa mbuga za wanyama. Taarifa hii itasaidia wafugaji kuepuka maeneo yenye mbung’o wengi, lakini pia katika kupanga mikakati endelevu ya udhibiti wa mbungó. 4. Kadhalika mwaka 2015, watafiti wa kitengo cha Udhibiti wa Visumbufu vya Mimea (PPD) waligundua na kutambua kuwepo kwa gugu la aina ya karoti (Parthenium Hysterophorus) katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.

Gugu hili lina athari za kiafya kwa binadamu na wanyama. Pia gugu karoti husababisha madhara kati-ka uzalishaji wa mazao hasa ngano, mahindi, mtama na maharage kwa kuzuia mbegu za mazao zisiweze kuota na kudumaza ukuaji wa mazao na mimea ya asili sehemu gugu hilo linapoota, na kuharibu mazingira.5. Kitengo cha Taifa cha Hifadhi ya Nasaba za Mimea kiliweza kupata miradi kumi na tano (15) ya nje ndani ya miaka 10 iliyofadhiliwa na mashirika mbalimbali kama Global Crop Diversity Fund, Program for Biosafety Systems (PBS – USAID), DAN-IDA, ICRISAT, ITPGRFA, COSTECH, Royal Botanic Gardens Kew, FAO, Bioversity International and Gatsby Foundation.

[i].Uhifadhi wa nasaba za mimea nje ya mazingira ya asili (Ex situ Conservation of plant genetic resources)

Jumla ya sampuli 2334 za mimea ya aina mbalimbali zilikusanya na kuhifadhiwa katika benki ya mbegu kati-ka kipindi cha 2015 – 2019. Zikiwemo sampuli 583 za mpunga zilizotokana na mradi wa kuhifadhi nasaba za mpunga uliofadhiliwa na GATSBY foundation, sampuli 122 za jamii ya mazao ya kunde, Ulezi na Uwele zilizotokana na Mradi wa Global Trust.

[ii].Uanzishwaji wa Maabara ya Bioteknolojia

Kitengo cha Kitaifa cha Hifadhi ya Nasaba za Mimea (NPGRC) kwa kushirikiana na wafadhili (DANIDA na FAO) kiliweza kuanzisha maabara ya bioteknolojia ambayo itasaidia kitengo, TPRI na wanasayansi wa Tanzania kufanya shughuli mbalimbali za kisayansi zinazohusu biotechnolo-jia kama kutambua sifa mbalimbali za mimea. Kutumia vijinasaba (Molecular characterization of PGR), Kuzalisha mimea kwa kutumia viini tete (Plant micro propagation), kuzalisha mimea isiyo na magonjwa (Screening and elimination of diseases in vegetatively propagated material), kuc-hunguza uwepo wa vijinasaba vilivyo badilishwa kijenetiki (screening of crops for GMO introduction) na kadhalika.

[iii]. Uhifadhi wa mimea katika mazingira ya asili (In situ/ On farm conservation of Plant Genetic Resources (PGR) Kitengo kilitekeleza mra-di wa uhifadhi wa mbegu za mazao yaliyosahaulika kama Mtama, Ulezi, Fiwi, maboga na Viazi vikuu uliofadhiliwa na ITPGRFA kwa lengo la kuendeleza mazao hayo kwa matumizi ya sasa na baadae katika kukabili-ana na athari za kimazingira ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi katika vijiji 8 vya mikoa ya Morogoro, Dodoma, Lin-di, Mtwara na Ruvuma. Kazi zilizofanyika ni pamoja na kukusanya taarifa za matu-mizi na njia za asili za uen-delezaji wa mimea husika, kuandaa jarida ya jinsi ya kutunza na kuzalisha mbe-gu, ukusanyaji wa mbegu (sampuli 231) na tathmini ya mbegu mbalimbali na kutoa mafunzo kwa wakulima jin-si ya kuzalisha na kutunza/ kuhifadhi mbegu husika

.[iv].Tathmini na uzalishaji wa mbegu (Regeneration, characterization and evaluation of conserved germ-plasm)

Katika kipindi cha miaka 5 Kitengo kilizalisha sampuli 143 za mazao mbalimbali ili kuongeza kiwango cha mbegu kwa ajili ya kuhifadhi za kuzigawa kwa wadau mbalimbali kama ifuatavyo (mahindi 71, Vibuyu 41, Mbaazi 22, na Uwele 9) zilifanyiwa tathmini ili kutambua sifa mbalimbali zilizomo katika mimea hiyo.6. Uendelezaji wa mbegu mbalimbali ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (Varietal Diversification to Manage Climate Risk in East Africa) Mradi huu ulianzishwa ili kufanya tathmini ili kufahamu athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa wakulima na kwa mimea kwa kutumia “models” mbalimbali, pia kutathmini uwezo wa aina mbalimbali ya mbegu za ulezi, mtama na maharagwe zilizohifadhiwa katika benki ya mbegu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Lengo likiwa ni kupata aina za mbegu zinazoweza kustahimili athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa maendeleo ya kilimo.

Kwa mawasiliano Zaidi

Anuani yetu ni:

Mkurugenzi MkuuTaasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Ukanda wa Tropiki (TPRI)

S.L.P 3024, Arusha

Barua pepe: [email protected]

Tovuti: www.tpri.go.tzUTAFITI WA VIUATILIFU Waziri wa