Kampuni zilizong’ara kwenye tuzo za umahiri katika sekta ya bima 2019


Kampuni zilizong’ara kwenye tuzo za umahiri katika sekta ya bima 2019

Tuzo za umahiri katika sekta ya bima ni mkakati wa kuimarisha na kuongeza kiwango cha uelewa wa umma kuhusu sekta ya bima ambao unafanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Tuzo za umahiri katika sekta ya bima ni mkakati wa kuimarisha na kuongeza kiwango cha uelewa wa umma kuhusu sekta ya bima ambao unafanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Tuzo hizi zimefanikiwa kutokana na udhamini wa kampuni ya bima mtawanyo Tanzania (Tan-re) pamoja na Chama cha makampuni ya bima Tanzania (ATI).

Lengo la tuzo hizi ambazo kwa mwaka huu zilizinduliwa rasmi Mei 21 ni kuzawadia na kutoa motisha kwa viongozi na watendaji waliofanya vizuri katika sekta ya bima Tanzania; kutambua na kuhamasisha uvumbuzi kwenye sekta ya bima; kuhamasisha ukuaji endelevu wa mchango ya bima katika uchumi wa nchi na kuleta ushindani katika sekta ya bima.

Tuzo hizo ambazo zilikuwa na vipengele 6 zilitolewa Septemba 26 kwenye maadhimisho ya siku ya bima katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza.

Washindi wa kila kipengele kwenye tuzo hizo walikuwa kama ifuatavyo;

Tuzo ya mjasiriamali kijana (Young Achievers Entrepreneurship)

Mshindi wa tuzo hii ni kampuni ya ITL Imatic Technologies Limited. Mshindi katika kipengele hiki alipatikana baada ya jopo la majaji kutoa alama za juu kutokana na wasilisho lake ambalo limeonyesha jitihada za Watanzania vijana katika kurahisisha utoaji wa huduma za bima kupitia TEHAMA.

Imatic Technologies imeajiri idadi kubwa ya wanafunzi wahitimu katika nyanja za bima na Teknolojia ya Habari. Kampuni hiyo imetengeneza sera ya ubunifu wa bidhaa (Jukwaa la bima la mahitaji ya kiutendaji ya wadau mbalimbali wanaohusika katika tasnia ya bima). Kupitia jukwaa hilo ni rahisi kukusanya tozo za bima na kutoa mikataba ya bima.

Tuzo za kijana aliyefanikiwa katika maendeleo ya Tafiti na Taaluma (Young Achievers Research Development and Ideas)

Mshindi wa tuzo hii ni Ledwina Daudi Msangi. Bi. Lwedina alipata ushindi huu kutokana na uwasilishaji wa utafiti aliyoufanya kuhusu namna bora ya kutumia teknolojia ya simu za mkononi katika kuwafikia wananchi wenye kipato cha chini na huduma za bima.

Majaji walithibitisha wazo lake, kuwa lina uhalisia na hali inayoaendelea katika jamii kwa sasa. Ledwina Daudi Msangi ni ofisa masoko kijana kutoka kampuni ya Phoenix of Tanzania Assurance Company. Utafiti wake ulieleza kuhusu fursa za kiteknolojia ambazo zinaweza kuongeza uelewa wa bima nchini Tanzania.

Utafiti huo pia ulitoa takwimu kuhusu ukuaji wa sekta ya bima na njia mbalimbali za kiteknolojia ambazo zinaweza kutumika katika kuongeza uelewa kwa wananchi.

Tuzo ya kampuni inayosaidia jamii (Corporate Social Responsibilities Award)

Mshindi wa tuzo hii ni; Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Ltd. Mshindi wa kipengele hiki alipatikana kutokana na uwasilishaji mzuri na uthibitisho wa kazi walizofanya kunufaisha jamii.

Majaji pia waliangalia namna kampuni hiyo ilivyosaidia jamii katika nyanja za elimu, afya, maji, hali za maisha n.k.Pia, jitihada mbalimbali kama vile kutoa vifaa vya huduma ya kwanza, kuchangia damu, kusaidia matibabu ya kina mama, miradi ya ukarabati wa shule. Ufanyikaji wa jitihada hizi ulithibitishwa.

Nafasi ya pili ilikuwa kampuni ya Phoenix of Tanzania Assurance Company Limited. Kampuni hii imeweza kusaidia makundi mbalimbali kwenye jamii wakiwe-mo walemavu, kusaidia masuala ya michezo na mazoezi, kusaidia masuala ya elimu, kutoa msiaada kwenye majanga mbalimbali ya asili.

Pia, kuwa na sera madhubuti ya kusaidia jamii.

Nafasi ya tatu ilishikwa na kampuni ya Sanlam Life Insurance Tanzania. Wameonyesha mchango wao katika jamii kupitia ujenzi wa shule, mbio za hisani kwa ajili ya kuchangia matibabu ya moyo kwa watoto, mradi wa kupaua taasisi ya polisi Arusha, kutengeneza mahali pakulia chakula kwa wafanyakazi wa magereza, kudhamini michuano ya Darts chini ya chama cha Darts Tanzania (TADA), wana sera maalum kuhusu kusaidia jamii ambayo waliiambatanisha.

Tuzo ya kampeni bora ya utoaji wa elimu ya bima (Insurance Awareness Campaign)

Mshindi wa kwanza kwenye kipengele hiki ni kampuni ya Britam Insurance Tanzania Limited. Kampeni ya “Tupo na Wewe” ambayo ilianza Aprili mpaka Julai 2019 ni kampeni iliyokuwa na mafanikio kwa jamii kutokana na kutumia njia mbalimbali kuhama-sisha matumizi ya bima ikiwemo redio na mitandao ya kijamii. Pia, kutokana na mrejesho kutoka kwenye mitandao wa kijamii, kampeni hii ilieleweka vizuri.

Nafasi ya pili kwenye kipengele hiki ilikwenda kwa kampuni ya Jubilee Insurance Limited Company. Kampuni hiyo imefanya uhamasishaji wa matumizi ya bima katika kipindi cha mwaka 2018/2019. Imetoa elimu ya bima kwa jamii kupitia matukio mbalimbali ikiwemo, siku ya Mashujaa, Jukwaa la ushiriki wa mwanamke kwenye sekta ya bima na fedha, matangazo ya redio, mafunzo ya bima n.k.

Nafasi yab tatu ilishikwa na kampuni ya Phoenix of Tanzania Assurance Company Limited. Kampuni hii kupitia kampeni zake za uhamasishaji imeweza kusaidia katika kufikisha elimu ya bima kwa jamii.

Miongoni mwa jitihada zao ni kufanya matangazo ya nyumba kwa nyumba kwa lengo la kupata wateja wa kati. Pia, kampuni hiyo ilifankiwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali katika maonyesho.

Tuzo ya bidhaa bora ya kibunifu ya bima (Most Innovative Insurance Product)

Mshindi wa tuzo hii ni kampuni ya Ushauri na Udalali ya Milvik Tanzania Limited. Katika kipengele hiki majaji hakuakuangalia tu bidhaa ya bima bali ubunifu na msaada wa bidhaa hiyo kwa wananchi wa kawaida.

Pia, ni kwa namna gani bidhaa hiyo inayokwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia hapa nchini.Bidhaa ya Bima Mkononi kutokana kampuni ya Milvik Tanzania Limited sio tu kwamba ilionyesha kuwa ya kibunifu, lakini mrejesho kutoka kwa wateja ulieleza kwamba bidhaa hiyo ni ya bei ya chini na rahisi kupatikana.

Bidhaa hii hutumia Tigopesa, Resolution na Mo kama washirika ili kufanya malipo ya bidhaa hiyo kuwa na rahisi.

Tuzo ya kampuni bora ya mwaka ya bima (Insurance Company of the year)

Mshindi wa jumla wa tuzo za umahiri wa bima 2019 ni kampuni ya Jubilee Insurance Limited Company ambayo ilifanikiwa kutwaa tuzo ya kampuni bora ya mwaka.

Mambo mbalimbali kama vile kuisaidia jamii, bidhaa za kibunifu kama vile Safari Vocha na mambo mengine ni miongoni mwa vitu ambavyo vimeiwezesha kampuni hii kuwa bora kwa mwaka 2018.

Kwa kuongezea, kampuni hiyo imekuwa ikitoa bidhaa mbalimbali za bima ambazo zimekuwa zikipunguza uwezekano wa hasara, kufanya kampeni mbalim-bali za kuelimisha umma n.k.

Wito kwa ushiriki wa mwaka ujaoKwa sababu nia kubwa ya tuzo hizi ni kuleta ushindani miongoni mwa huduma za bima nchini na kuleta hamasa kwa wananchi kuelewa na kutumia huduma za bima, Mamlaka na Taasisi ya bima nchini inatarajia mwamko mkubwa wa ushiriki wa kampuni, wadau mbalimbali katika mwaka ujao. Tuzo hizi zitakuwa zikifanyika kila juma la mwisho la mwezi wa 9.