TCAA katika kuchochea maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga SADC


TCAA katika kuchochea maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga SADC

Huduma za usafiri wa anga ni jicho pevu lililogusa hisia za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Huduma za usafiri wa anga ni jicho pevu lililogusa hisia za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Rais Magufuli alikabidhiwa kijiti cha kuongoza mtangamano huo kwa mwaka mmoja kuanzia Julai 17 mwaka huu na Rais wa Namibia, Hage Geingob kupitia Mkutano Mkuu wa 39 wa SADC uliofanyika Jiji-ni Dar es Salaam.

Kiitifaki, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari anabeba ndoto za Rais Magufuli katika kufanikisha malengo ya mtangamano huo kupitia Kamisheni ya Usafiri wa Anga Kusini mwa Afrika (SADC-CAC), inayounganisha mamlaka za nchi wanachama.

Hamza Johari ndiye Mwenyekiti mpya wa Kamisheni hiyo kwa mwaka mmoja akipokea kijiti hicho kutoka Namibia. Mamlaka hiyo inahusika na shughuli za usimamizi na udhibiti wa huduma za usafiri wa anga kuanzia operesheni za mashirika ya ndege, viwango vya ubora wa ndege, sifa za marubani na wahandisi wa ndege, ubora wa karakana za ndege na vyuo vya mafunzo, ubora wa viwanja vya ndege na ujenzi wake, usalama wa anga, huduma za ardhini, huduma za uongozaji ndege na mitambo yake na mambo ya kiuchumi ya usafiri wa anga.

SADC-CAC, inatekeleza majukumu yake chini ya mwenyekiti kwa kushirikiana na wajumbe ambao ni wakurugenzi wa mamlaka pamoja na watalaamu wa wizara za uchukuzi.

Johari anataja hatua nne katika kuchochea utekelezaji wa mipango ya SADC CAC ndani ya ngwe yake ya uongozi. Uwakilishi wa ICAOKwanza, Johari anasema anawajibika kuhakikisha SADC inapata mwakilishi atakayekuwa mmoja wa wajumbe wa Shirika la Usalama wa Anga Duniani (ICAO) linalotunga sera, sheria na kanuni zinazosimamia usafiri wa anga duniani.

“Wanachama wa ICAO ni nchi 193 duniani na shirika hilo linaongozwa na Baraza lenye wajumbe kutoka nchi 36. Kwa sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi 36 zinazounda Baraza hilo kiti ambacho ilikitwaa mwaka 2016 na jukumu la Johari ni kuhakikisha nchi za SADC zinapata tena kiti hicho pindi Tanzania itakapomaliza muda wake mwezi Oktoba 2019.

Nchi za SADC zimekubaliana Zambia ishindanie kiti hicho katika Mkutano unaondelea nchini Canada kwa sasa na endapo Zambia itashinda itachukua kijiti hicho kutoka Tanzania rasmi tarehe 04 Oktoba 2019. Kwa sasa Johari yuko nchini Canada katika zoezi hilo muhimu kwa SADC. Mkutano wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani ulianza tarehe 23 Septemba 2019 na uta-malizika tarehe 05 Oktoba 2019. Johari anasema bila juhudi, nafasi hiyo inaweza kuchukuliwa na ukanda mwingine.

“Kwa nafasi yangu nitahakikisha SADC inaendelea kuwa na sauti ndani ya ICAO. Hii ni fursa kwa Watanzania na heshima,”anasema Johari.Usalama wa angaJohari ambaye pia ni mhadhiri katika sheria za anga, uchukuzi na kimataifa (part time lecturer) katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, anasema hatua nyingine katika utekelezaji wa majukumu ndani ya tume hiyo ni kuimarisha usalama wa anga katika nchi 16 za SADC.

“Tunataka kuwa na udhibiti wa pamoja wa kusimamia sekta ya usafiri huo katika SADC, tumeanzisha taasisi ya watalaamu inaitwa SASO, lengo ni kuwa na watalaamu kwa hiyo kazi itakayoanza kufanyika hapa ni kukusanya watalaam wa kutosha kwa ajili ya kuongeza nguvu katika ukaguzi wa ndege na mashirika ya ndege, viwanja vya ndege, vyuo vya mafunzo, uchunguzi wa ajali za ndege,” anasema Johari. Johari anasisitiza akise-ma lengo ni kuwa na maz-ingira ya kulishughulikia changamoto mahali popote pale ndani ya SADC.

“Kwa kufanya hivyo tut-akuwa tumeunganisha rasilimali na kupunguza gharama za matumizi. Hatua iliyopo ni kukamilisha azimio la pamoja kwa hiyo katika awamu yangu nimejipanga kuhakikisha tunafanya taasisi hiyo hiyo ianze kazi,”anasema.

Kuhusu usalama, Hamza anasema hali ni nzuri katika eneo la SADC, kutokana na ukaguzi uliofanywa na ICAO, kupitia kipimo cha ‘Hali hatarishi ya Kiusalama ndani ya Mfumo wa Usafiri wa Anga duniani’. “ICAO wanafanya kaguzi mamlaka zote duniani kuangalia uwezo wao wa kiusalama na uwezo wao wa kuthibiti katika kusimamia sekta ya anga.

Kila ukaguzi una alama zinazotakiwa kuanzia asilimia 60 kwenda juu, Tanzania tuko asilimia 64.35 na hatuna hali hatarishi ya kiusalama (Significant Safety Concern) Johari anasema alama hatarishi inaashiria tatizo kubwa la kiusalama katika kudhibiti na kusimamia sekta ya anga, akisema kwa nchi za SADC, Malawi ndiyo ilikuwa na hali hiyo lakini walifanikiwa kuiondoa mwaka 2018 baada ya kufanyia kazi kasoro zilizobainishwa.

“Nilipoingia mwaka 2016 nilikuta Tanzania tukiwa na alama 37 ilibidi nifumue sheria zote, tukajipanga na kutoa maelekezo kwa taasisi tunazosimamia haya mashirika ya ndege, tukaongeza bidii na walipokuja kukagua tena mwaka jana ndiyo tukapata alama 64.35,” anasema Johari.

Ufanisi wa anga la SADCKatika hatua nyingine, Johari aliyebobea katika masuala ya sheria za anga na kimataifa anasema eneo la tatu ni kuhakikisha eneo la anga la SADC linakuwa na huduma bora za anga pale ndege ya nchi mwana-chama inaporuka hadi nchi nyingine ndani ya SADC.

“Ndege ziongozwe na watalaamu wazuri, tuwe na sheria na taratibu sawia za anga, siyo kila ukiingia Zambia, Malawi au Afrika Kusini kuna taratibu tofauti, tunaboresha mifumo, siyo kila nchi inakuwa na mtambo wake huyu wa Kichina, yule wa Kikorea kwa hiyo mitambo inakuwa haisomani,” anasema.

Akitolea mfano wa kasi ya matumizi ya teknolojia ya matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones), Johari anasema kamisheni ya SADC itatengeneza kanuni za udhibiti zinazofanana kwa nchi zote, kuoanisha sera na sheria ili kuwa na mazingira sawa. Johari anasema nchi ambazo tumeshakamilisha kanuni za ndege zisizo na rubani hadi sasa ni Tanzania, Afrika Kusini, Namibia, Botswana, nyingine ziko katika hatua za maandalizi, tunatarajia watakamilisha ili kufanikisha hatua hiyo.

Eneo la kiuchumiKatika eneo hili la kichumi nchi za SADC zimejikita katika malengo ya kuwa na soko la pamoja katika usafiri wa anga kwa maana ya kuondoa vikwazo vya mashirika ya ndege kutoa huduma katika anga ndani ya nchi hizo za SADC.

“Kwa sasa kuna vikwazo na huwezi kuruka katika nchi nyingine bila makubaliano, kwa mfano uruke mara ngapi kwa wiki au ulete ndege yenye ukubwa gani, hili ni eneo ambalo bado ni changa sana,”anasema. “Hofu ya kibiashara ni kawaida kwa sababu ni biashara, kila nchi mwanachama anadhani kwamba nchi fulani ikileta ndege itaathiri soko lake. Kwa hiyo ni eneo nyeti sana linalohitaji umakini mkubwa,” anasema Johari.

Johari anasema hatua kwa hatua zitaanza kufanyika kwa umakini zaidi ili kue-puka athari zinazoweza kuathiri mashirika yanayoendelea kukua ndani ya mtangamano huo. Johari anasisitiza katika mahojiano haya akisema hatua ya kwanza itakayofanyika chini ya makubaliano ya mamlaka hiyo ni kuon-doa vikwazo vya ukomo wa idadi ya safari pamoja na ukubwa wa ndege zinazoweza kuingia katika nchi mwanachama wa SADC baa-da ya kubaini hakuna athari kibiashara.

“Tatu tunaweza kuon-doa kikwazo cha mashirika mangapi yatoke au yaingie nchi mwanachama, hakuna sababu ya kuwa na kikwazo hicho, Tanzania tumeshain-gia makubaliano na nchi zote za SADC kinachojitokeza ni changamoto ya utekelezaji,” anasema Johari. Maeneo ya tahadhali Pamoja na ushirikiano wa maeneo hayo,

Johari anasema Kamisheni ya SADC inalazimika kuchukua tahadhari katika eneo la mikataba inayohusu haki za matumizi ya anga kupitia Itikafi ya Single African Air Transport Martket (SAA-TM) Itifaki hiyo inahusisha haki namba moja hadi namba tisa kwa nchi zote za Afrika na nchi za Afrika zinalazimika kusaini ili kukubaliana nazo ndani ya nchi yake.

“Haki namba moja ni mashirika ya nchi ya mwa-nachama kukatisha anga la nchi moja hadi nyingine bila kutua, anapita anga la Tanzania kwenda nchi nyingine anaomba huduma ya kukatiza anga letu

Haki namba mbili ni kukatiza katika anga na kutua kwa dharura katika nchi nyingine,” anasema. Akitumia mifano ya nchi wanachama, Johari anasema;

“Haki namba tatu ndiyo biashara inaanza kuzaliwa, mfano ni haki ya kupeleka vifurushi au abiria nchini Kenya na kisha kurudi Tanzania bila abiria. Haki namba nne unaruhusiwa kupeleka abiria Kenya kubeba tena abiria wengine kuleta Tanzania.”

Haki namba tano Tanzania kwa kawaida hatuitoi kwa sababu ya kutokuwa na maslahi kwa nchi. Ni haki ya Shirika la Ndege la kigeni linabeba abiria wa Tanzania kuwapeleka nchi ya tatu moja kwa moja. Mfano Shirika la Kenya lichukue abiria Dar es Salaam na kuwapeleka Zambia moja kwa moja ambako ATCL anapeleka abiria hao hao kutoka nchi yake.

Kuhusu haki namba sita, inataka Ndege ya shirika kutua kwanza katika nchi yake kabla ya kuendelea na safari, mfano Afrika Kusini inayoenda Zimbabwe inabidi ipitilize Zimbabwe hadi Afrika Kusini kisha warudi tena Zimbabwe, ukiomba hii tunakupa kwani abiria yuko tayari kupanda ATCL moja kwa moja.”Haki namba saba hatuikubali pia, ni haki inayoruhusu shirika la ndege kuingia Tanzania kushidania abiria wa nchi nyingine.

Kwa mfano ATCL iwe na kituo Kenya halafu ianze tena kuruka kutoka Kenya hadi Sudan. Hii pia inatishia uhai wa soko la ndani.

Haki namba nane ambayo pia Tanzania hatuitoi inaruhusu Shirika la kigeni kubeba abiria wa kimkoa katika nchi inapokuwa kwenye safari yake. Mfano KLM inapokuja na kuanza kutua Kilimanjaro basi ibebe abiria wa kimkoa kutoka Kilimanjaro kuleta abiria Dar es Salaam.

Hii inaua mashirika ya ndani kwenye ruti hizo. Haki namba tisa ambayo pia hatuitoi ni shirika la kigeni kama KLM au Kenya Airways kutoa huduma za kimkoa katika nchi yetu.

“Kwa hiyo Tanzania haijasaini itifaki ya Single African Air traffic ambayo inataka nchi mwanachama mpeane tu haki zote hizo 9 bila vikwazo. Tathmini ya kina inahitajika na kuangalia athari za kibiashara na uchumi. Nchi za Afrika ambazo zimesaini ni zile zenye mashirika makubwa ya ndege na nchi zisizokuwa na mashirika ya ndege kabisa,” anasema Johari.

“Nchi ambazo hazijasaini ni nchi zenye mashirika machanga yanayokuwa na mipango ya kukuza mashirika yake kwa sababu ni biashara. Sasa hii itifaki iko katika majadala. Kwa malengo ya kutathmini mapungufu yake na hilo ni muhimu sana. Kwa hiyo hayo ndiyo maeneo ambayo tumejipanga kuwekea mkazo zaidi ndani ya mwaka wangu mmoja kama mwe-nyekiti wa Kamisheni ya Usafiri wa Anga ya SADC.”