Mafanikio na uzoefu wa China kwa Miaka 70 iliyopita


Mafanikio na uzoefu wa China kwa Miaka 70 iliyopita

Jamhuri ya Watu wa China ilianzishwa Oktoba 1, 1949. Katika kipindi cha miaka 70, China imepita safari ndefu ya kujiendeleza kutoka nchi maskini na dhaifu na kuwa nchi yenye neema na yenye nguvu.

Jamhuri ya Watu wa China ilianzishwa Oktoba 1, 1949. Katika kipindi cha miaka 70, China imepita safari ndefu ya kujiendeleza kutoka nchi maskini na dhaifu na kuwa nchi yenye neema na yenye nguvu.

China sasa ni nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani, nchi kubwa zaidi ya kiviwanda, nchi kubwa zaidi kwa biashara ya bidhaa na ni nchi yenye akiba kubwa zaidi ya fedha za kigeni.

Katika muda wa miaka 70 iliyopita, uchumi wa China umekuwa na ongezeko la kasi na endelevu. Tangu ilipoanza kutekeleza sera ya mageuzi na uwazi mwaka 1978, wastani wa ongezeko la pato la ndani la taifa GDP kwa mwaka lili-kuwa karibu 9.5%.

Wakati huo huo, wastani wa pato la taifa kwa kila mtu umeongezeka kutoka chini ya dola za kimarekani 240 na kufikia takribani dola za kimarekani 10,000, na mwaka 2018 pato la ndani la China GDP lilifikia dola za kimarekani trilioni 13.

Katika muda wa miaka 70 iliyo-pita, sayansi na teknolojia nchini China imepiga hatua. Chombo cha safari kwenye anga ya juu chenye binadamu, utafiti wa sayari ya mwezi, sayansi ya Quantum, utafiti wa bahari yenye kina kirefu, kompyuta zenye kasi kubwa na satelaiti za uongozaji zimeanzishwa moja baada ya nyingine, huku mafanikio kadhaa ya kisayansi na kiteknolojia yamefikia viwango vya kuongoza duniani.

Katika muda wa miaka 70 iliyopita, kiwango cha maisha na ustawi wa jamii ya watu wa China vimekuwa vikiongezeka bila kukoma.

Wastani wa pato linaloweza kutumiwa na mtu kwa mwaka umeongezeka kutoka chini ya dola za kimarekani 25 kwa mwaka 1978 na kuwa dola za kimarekani zaidi ya 4,000 leo, zikiwa zimeongezeka mara 160. Katika muda wa zaidi ya miaka 40 ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na uwazi, China imewaondoa watu milioni 740 kutoka kwenye umaskini, na wastani wa muda wa kuishi wa wachina umeongezeka na kufikia miaka 77.

China imekuwa inahimiza kujen-ga jamii yenye mustakabali wa pamoja kwa binadamu. Wazo la kimsingi la jamii hii, ni kuwa waka-ti tunakabiliana na masuala na changamoto za dunia, tudumishe amani badala ya vita, maendeleo badala ya umaskini, ushirikiano badala ya migongano na kunufaishana badala ya kujinufaisha.

Uzoefu wa miaka 70 wa China unaonyesha kuwa, ni pale tu usiposahau ulipoanzia, ndio unaweza kufanikisha lengo lako. Kutafuta furaha kwa watu wa China na ustawishaji mkubwa wa taifa la China ni nia yetu thabiti na lengo letu lisiloyumba.

Mwaka kesho, China inatarajia kutimiza lengo la kwanza la karne la kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, na watu milioni 16 waliobaki kwenye umaskini wataondolewa kwenye umaskini.

Uzoefu wa miaka 70 wa China unaonyesha kuwa mwelekeo unadhamiria siku za baadaye huku njia ikidhihirisha mustakabali.

Tumepita kwa mafanikio kwenye njia ya ujamaa wenye tabia za kichina, wachina sasa wameinuka na kuweza kujitetea, na kujitajirisha na kuwa na nguvu. Dunia ina rangi mbalimbali, na hakuna njia moja ya maendeleo.

Njia inayofuatwa na nchi inatakiwa kuwa ile inayoendana na mazingira ya taifa, inayohimiza maendeleo na inayoleta manufaa endelevu kwa watu wake.

Miaka 70 ya uzoefu wa China inaonyesha kuwa uwazi unaleta maendeleo na kujitenga kunarudisha nyuma. Sera ya mageuzi na uwazi ni ufunguo muhimu kwa China kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii.

Katika siku za baadaye, China itakuwa na uwazi zaidi na kushirikiana kwa karibu zaidi na nchi nyingine duniani, na kuleta maendeleo na neema zaidi kwake yenyewe na kwa dunia kwa ujumla.

Ningependa kutumia fursa hii kuonyesha shukrani zangu za dhati kwa marafiki zetu wa Tanzania na wa kimataifa wanaoiunga mkono China kwenye mageuzi na uwazi na kazi ya kuunganisha taifa letu. Wakati huo huo, naitakia Tanzania ipate maendeleo makubwa kwe-nye nia yake ya kuleta maendeleo ya viwanda chini ya uongozi wa Rais Magufuli. Tanzania ina uwezekano mkubwa wa kuwa na maendeleo, hii ni nchi nzuri iliyojaa matumaini.

Wang Ke ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania