China ni rafiki wa kweli na mshirika mwaminifu wa Tanzania


China ni rafiki wa kweli na mshirika mwaminifu wa Tanzania

Ukifikiria miaka elfu tano ya kujengeka kwa ustaarabu wa China, miaka sabini inaweza kuonekana kuwa kipindi kifupi sana.

Ukifikiria miaka elfu tano ya kujengeka kwa ustaarabu wa China, miaka sabini inaweza kuonekana kuwa kipindi kifupi sana.

Lakini ukiangalia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho cha miaka sabini, unasisimkwa sana. Katika kipindi cha miaka sabini iliyopita, China imepitia mabadiliko makubwa.

Mabadiliko haya yamebadilisha maisha ya mamia na mamilioni ya Wachina, na kuiweka China miongoni mwa mataifa imara duniani. Moja ya tano ya watu wote duniani hivi sasa ni raia wa China ambayo ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani.

Kwa hakika, Global Innovation Index (GII) ilirejea ripoti ya World Intellectual Property Organization ya Julai 24, 2019, ambayo ilipima uchumi wa nchi 129 kwa kuzingatia vigezo 80, na kuonyesha kuwa China imepanda kwa nafasi tatu hadi nafasi ya 14 miongoni mwa nchi zenye ubunifu mkubwa duniani mwaka huu.

China iliendelea kushika nafasi ya kwanza kwa nchi zenye ubunifu mzuri miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati kwa mwaka wa saba mfululizo, na ikawa nafasi ya kwanza kwa hati miliki, modeli ya huduma, alama za biashara na ubunifu wa viwandani wa asili na pia teknolojia ya hali ya juu ya ubunifu wa bidhaa zinazouzwa nje.

China pia ilishika nafasi ya pili nyuma ya Marekani ikishika nafasi ya 18 katika kundi la nchi 100 katika eneo la sayansi na teknolojia.

Mabadiliko haya ni ya msingi sana na yanapaswa kuwa hamasa kwetu wakati tukipambana kujenga uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Yanatukumbusha kufanya kazi kwa juhudi, kujitoa na juu ya yote kuheshimu ubinadamu wakati tukiendelea kuimarisha uchumi wetu. Historia na miongo saba ya China imeshuhudia mafanikio makubwa ambayo yanapaswa kushere-hekewa.

Kama ningetaka kuoro-dhesha mafanikio yote, makala yangu hii ingechukua nafasi ya toleo hili lote maalum. Kwa hiyo, naomba mniruhusu nitaje mambo makubwa matatu ambayo kwa maoni yangu yanawakilisha kwa ujumla mafanikio yaliyofikiwa na China katika kipindi cha miaka 70 iliyopita.

Jambo la kwanza ni maendeleo yasiyo na mpaka. Tangu kuanzishwa kwa China Mpya, maendeleo ya China yamegusa zaidi maisha ya watu na yamelenga kufaniki-sha matarajio ya watu ya kuwa na maisha bora. Huku ikijenga uchumi imara, China imeendelea kuhakikisha maendeleo yanapatikana sawia katika nyanja zote.

Jambo la pili ni kujikita katika kujifunza mambo mapya na kub-adilishana uzoefu. Jambo hili linaimarisha ustaarabu. Kupitia miradi kadhaa, hasa Belt and Road Initiative (BRI) na Mkutano wa Pamoja wa Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC), uzoefu mkubwa na mafunzo vimeendelea kupatikana kwa watu wa China na duniani kote.

Hakuna ubishi kuwa mambo haya mawili yameitikisha dunia yakilenga kuweka mrengo wa ushirikiano wenye manufaa kwa nchi zote zinazoshiriki.

Jambo la tatu ni ujenzi wa mfumo unaonufaisha pande zote. Sote ni mashahidi wa uwazi wa China katika kujenga mfumo unaonu-faisha kila upande bila ubaguzi.

Jambo hili lilijidhihirisha miaka 41 iliyopita kwa China kukumbatia mabadiliko na kufungua uchumi wake na hivyo kutoa fursa kwa dunia nzima kunufaika na mambo yanayofanywa na China.

Tunaposherehekea miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, pia tunasherehekea miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China.

Uhusiano huu wa kidiplo-masia umepitia hatua mbalimbali muhimu kama iliyoelezwa sawa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa na Rais Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kuwa, “Jamhuri wa Watu wa China ni rafiki maalum na muhimu na sasa tuna rafiki ambaye ni rafiki mkubwa na wa kweli ambaye tulizuiwa kuwa naye katika kipindi cha ukoloni.”

Uhusiano wa karibu unaohusi-sha watu kati ya Tanzania na China umeimarisha maisha ya watu wa nchi zetu hizi. Huu ni mfano mziri wa uhusiano unaonufaisha pande zote.

Nina uhakika kuwa jinsi inavyozidi kupata maendeleo, China itaendelea kufungua fursa nyingi sana na maeneo mapya ya nchi zetu kushirikiana.

Serikali ya Jamhuri ya Muun-gano ya Tanzania na watu wake mara zote wameichukulia China kama rafiki wa kweli na mshirika mwaminifu. Tunaendelea kuiunga mkono China katika sera yake ya “Nchi Moja, Mifumo Miwili”. Hali kadhalika, tunaamini kuwa China itaendelea kusimama na nchi za Afrika kuhakikisha kuwa maslahi ya nchi zinazoendelea zikiwamo za Afrika yanazingatiwa na kuharakishwa katika mabadiliko ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Udumu urafiki na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania!

Mhe. Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi (MB) ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.